THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.


Share Michuzi Blogyale yaleee...

Mabasi yakipimana ubavu katika barabara kuu kuelekea Morogoro hivi karibuni.  Kwa mtaji huu ajali zitaisha kweli?


JK KATIKA MAZISHI YA ALIYEKUWA MKUU WA WILAYA YA KYERWA LUTENI KANALI BENEDICT KITENGA (MSTAAFU) MKOANI MOROGORO


Mikoa mitano kushiriki mashindano ya mchezo wa vishale "Darts" Taifa

Na Mwandishi Wetu.

MASHINDANO ya mchezo wa Darts Taifa yamezinduliwa rasmi leo jijini Dar es Salaam katika Hoteli ya Moshi iliyopo Manzese kwa kushirikisha mikoa mitano ya Tanzania.

Akizindua mashindano hayo Katibu Tawala wa Wilaya ya kinondoni, Selestine Onditi ”kwanza aliwapongeza viongozi wa chama hicho kwa juhudi za pekee za kufanya mashindano hayo yafanyike kwa mwaka wa 2015,lakini zaidi aliwashukuru wachezaji kwa moyo wa kupenda mchezo kujigarimia kuacha kazi zao kutoka mikoani ikiwa pamoja na wenyeji Dar es Salaam kuja kushiriki mashindano hayo ya Taifa kwa kujilipia gharama zote za ushiriki hiyo inatia moyo sana kuwa ni dhahiri mnaopenda mchezo”.
Alisema Onditi michezo ni afya,michezo ni furaha na michezo ni kufahamiana basi aliwataka washiriki wote watumie nafasi hii ya kukutana katika kuyafanikisha haya yote.

Onditi alitoa wito kwa wafadhili kuwa wasiegemee kwenye mpira wa miguu tu kuna michezo mingi kama Darts na mingine wajitokeze wadhamini kwani kwa kutumia wapenda michezo kama hawa waliojitolea kutoka mikoani kwa gharama zao kuja kushiriki mashindano ya Taifa ni nafasi ya pekee wewe mfanyabishara kutangaza biashara yako.

Mwisho aliwatakia mashiondano mema yenye amani kuwa waanze salama na wamalize salama na mwisho warejee majumbani salama salimini.
Nae Mwenyekiti wa Chama cha Darts Taifa, Gesase Waigama alizitaja zawadi kuwa ni Vikombe na Pesa taslimu kwa mfumo wa mashindano utakaotumika ni wa Singles(mmoja mmoja), Doubles(wawili wawili) na Timu.

Mwisho Katibu wa Chama cha Darts Taifa, Kalley Mgonja aliitaja mikoa iliyofanikiwa kufika jijini Dar es Salaam kwa ushiriki wa mashindano ya Taifa kuwa ni Mbeya, Morogoro, Dodoma, Arusha na wenyeji Dar es Salaam.


Elimu ya uongozi bora yatolewa kwa viongozi wa vikundi vya vijana Kata ya Selela

Mhamasishaji kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi. Ester Riwa katikati akizungumza na Vijana wa Kata ya Selela (hawapo pichani) wakati wa semina ya Ujasiriamali, Ujuzi, Stadi za Maisha na Mfuko wa Maendeleo ya Vijana jana katika Kata ya Selela Halmashauri ya Wilaya ya Monduli Mkoani Arusha. Kushoto ni Mkuu wa Kituo cha Vijana Sasanda Mbeya Bw. Laurean Masele na kulia ni Afisa Maendeleo ya Vijana kutoka Wizara hiyo Bi. Amina Sanga.
Afisa Maendeleo ya Vijana kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Monduli Bi. Mesha Singoyo akifafanua jambo kwenye semina ya vijana wa Kata ya Selela kuhusu Ujasiriamali, Ujuzi na Mfuko wa Maendeleo ya Vijana iliyofanyika jana katika Halmashauri ya Wilaya ya Monduli Mkoani Arusha.
Afisa Maendeleo ya Vijana kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bi. Amina Sanga (kulia) akizungumza na wanakikundi cha Naisho wanaomiliki mradi wa kunenepesha ng’ombe na kuziuza wakati wa kutembelea miradi ya vijana wa Kata ya Selela Halmashauri ya Wilaya ya Monduli Mkoani Arusha. Wapili kushoto ni mhamasishaji kutoka Wizara hiyo Bibi. Ester Riwa na wanne kushoto ni Mkuu wa Kituo cha Vijana Sasanda Mbeya Bw. Laurean Masele.

BOFYA HAPA KUONA PICHA ZAIDI


NEWS ALERT: WATANZANIA 26 WALIOKUWA AFRIKA KUSINI WAREJEA NYUMBANI, 20 WENGINE KUHAKIKIWA NA KUREJESHWA

Kundi la Watanzania 25 limerejea nyumbani kutoka Afrika Kusini leo tarehe 26 Aprili, 2015 kufuatia mashambulizi ya wazawa dhidi ya wageni. Kundi hilo la kwanza kurejea nyumbani liliwasili katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere saa 11 alfajiri na Ndege ya Fast Jet.

Watanzania hao walikuwa wanaishi katika kambi za dharura za Isipingo na Phoenix zilizopo jijini Durban. Walisindikizwa kurudi nyumbani na Afisa wa Ubalozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini, Bw. Elibahati Lowassa. Zoezi la kuwarejesha wananchi hao lilisimamiwa na kuratibiwa na Ubalozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini.

Wakati huo huo, Ubalozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini umepata taarifa kuwa kuna Watanzania wengine wapatao 20 wanaishi kwenye Kambi ya Hillbrough jijini Johannesburg. Ubalozi umetuma Afisa kwenda katika kambi hiyo ili kufanya uhakiki wa taarifa hizo kwa madhumuni ya kuwarejesha nyumbani Tanzania haraka iwezekanavyo.

Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali kwa Umma,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,
25 Aprili 2015


UTENDAJI KAZI WA FILIKUNJOMBE WAWAVUTIA WANANCHI WAKE LUDEWA

Mbunge  wa Ludewa Deo Filikunjombe akishirikiana,viongozi wa CCM , wananchi na mafundi  wa mradi wa umeme kubeba nguzo za  umeme katika  kitongoji cha Ngalawale Ludewa kijijini kama  sehemu ya kuhamasisha wananchi kushiriki maendeleo.
mbunge Filikunjombe akiwa  chini ya shimo akishiriki  kuchimba shimo la nguzo ya  umeme  kitongoji cha ngalawale  kijiji  cha ludewa wengine ni diwani wa kata ya  Ludewa MONICA MCHILO ,katibu mwenezi wa ccm mkoa wa Njombe Honoratus Mgaya na katibu mwenezi  wa CCM ludewa FELIX Haule  wakishirikiana na mbunge  wao.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI


Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi akutana na Viongozi wa Elimu nchini Singapore

Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Dkt. Shukuru Jumanne Kawambwa pamoja na viongozi wa elimu nchini wametembelea Singapore kujifunza jinsi nchi hiyo ilivyofanya mageuzi makubwa katika mfumo wa elimu na mafunzo.

Mfumo wa elimu wa nchi hiyo, unalenga kuendeleza wanafunzi katika kuwapatia stadi muhimu zinazohitajika kwa maendeleo ya nchi.

Mfumo wa elimu wa nchi hiyo, umeweka mkazo zaidi katika kutoa mafunzo ya ufundi stadi ambayo yanatoa ujuzi kwa mhitimu kuweza kufanya kazi katika kada ya kati. Takwimu za elimu zinaonyesha kuwa, asilimia 29.4 ya wahitimu wanajiunga na vyuo vikuu; asilimia 28.2 wanajiunga na vyuo vya elimu ya ufndi na asilimia 46.4 wanajiunga na vyuo vya utaalamu mbalimbali (Polytechnic).

Katika ziara hiyo Dkt Kawambwa na ujumbe wake walipata nafasi ya kutembelea chuo kikuu cha Taifa cha Singapore (National University of Singapore), Chuo cha Elimu ya Ufundi (Institute of Technical Education) na Chuo cha Ufundi stadi (Republic Polytechnic) ambapo katika vyuo hivyo walipata nafasi ya kuona shughuli mbalimbali zinazofanywa na wanafunzi pamoja na walimu.
Waziri wa Elimu na Mafunzo Dkt Shukuru Kawambwa akielezea Jambo katika Mkutano kati ya viongozi wa elimu kutoka wa Tanzania na Viongozi wa Wizara ya Elimu ya nchini Singapore.
Viongozi wa Wizara ya Elimu na Mafunzo kutoka Tanzania na Viongozi wa Elimu wa Singapore wakiwa katika mkutano wa pamoja katika kubadilisha mbinu na mikakati mbalimbali ambayo inaweza kuboresha na kuleta mageuzi katika mifumo ya elimu wa nchi hizi mbili.
Waziri wa Elimu na ujumbe wake wakiwa katika mkutano wa pamoja na viongozi wa Chuo kikuu cha Taifa Singapore. Ujumbe wa Tanzania ulitembelea chuo hicho ili kujionea na kujifunza ambavyo elimu ya ngazi ya chuo kikuu inavyotolewa nchini Singapore.


Dar City kukipiga na Kombaini ya Vikawe, Kibaha Mkoani Pwani

Kiungo mshambuliaji, Haruna Moshi ‘Boban’ na kipa, Juma Kaseja ni kati ya wachezaji watakaoiongoza timu ya Dar City kesho Jumapili Aprili 26,2015 kucheza mechi ya kirafiki dhidi ya Kombaini ya Vikawe iliyopo Mkoani Pwani.

Kwa mujibu wa mratibu wa mchezo huo, Athuman Tippo ‘Zizzou’, mchezo umeandaliwa maalum kwa ajili ya kuhamasisha michezo mkoani Pwani.

Tippo alisema kikosi cha Dar City kitajumuisha pia baadhi ya Waandishi wa Habari za Michezo na kubainisha kuwa mechi hiyo itachezwa kesho Jumapili kuanzia saa 10:00 jioni kwenye Uwanja wa Shule ya Msingi Vikawe uliopo Kibaha, Mkoani Pwani.

“Kikubwa tunataka kuhamasisha michezo huko Vikawe na katika kutimiza hilo, tumepanga kucheza mchezo mmoja wa kirafiki na wakazi wa huko kwa kuwatumia wachezaji, waandishi na watangazaji maarufu nchini,” alisema Tippo.

Kikosi cha Dar City kinaundwa na wachezaji kama Manyika Peter, Juma Kaseja , Athuman Idd "Chuji" , Haruna Moshi "Boban",Idd Moshi,Kahabuka, George Magere Masatu, Charles Palapala,Mwinchumu Babel, Tippo Athumani "Zizzou", Shaffih Dauda, Saleh Ally,Kamba Lufo,Mbwiga wa Mbwiguke, Ibrahim Massoud "Maestroal",Clifford Mario Ndimbo, Abou Amokachi,Shearer Pamoja na Juma Assey
BREAKING NYUZZZZ...: ZAIDI YA WATU 900 WADAIWA KUPOTEZA KWA TETEMEKO LA ARDHI NCHINI NEPAL

TETEMEKO la ardhi limetokea nchini Nepal muda mchache uliopita na na kupoteza maisha ya watu  ya 900 na kuangusha Mnara wa Karne ya 19 Mjini, Kathmandu pamoja na kusababisha maporomoko ya theluji kutoka katika milima. 

Taarifa zinadai kuna uharibifu katika maeneo ya nje ya kitovu cha tetemeko hilo lenye ukubwa wa kipimo cha richter cha 7.9 maili 50 kutoka Pokhara mji wa pili kwa ukubwa nchini Nepal. 

Tetetemeko hilo la ardhi ni kubwa kabisa kuwahi kuikumba nchi hiyo katika kipindi cha miaka 81 na pia limesababisha athari katika majimbo ya nchi jirani kaskazini mwa India na Bangladesh. 

Kunauwezekano vifo hivyo vinaweza kuongezeka katika Bonde la Kathmandu ambalo lina watu milioni 2.5.

Naibu balozi wa Nepal mjini New Delhi Prasad Pandey amesema inahofiwa kuwa mamia ya watu wamekufa na kuna ripoti ya kuwepo kwa uharibifu mkubwa kila sehemu kubwa na kwamba sio tu katika baadhi ya maeneo ya Nepal bali ni nchi nzima imeathirika. 

Nepal ilikumbwa na tetemeko kubwa la ardhi kuwahi kurekodiwa nchini humo hapo mwaka 1934 likiwa na kipimo cha 8.0 ambapo watu 8,500 walipoteza maisha yao.
Baadhi ya Waokoaji wakiwa wamsaidia mmoja wa waathirika wa Tetemoko hilo aliekuwa amefukiwa kwenye kifusi ya moja ya majembo yaliyoporokoma kutokana na tetemeoko hilo.
Sehemu ya athari za tetemeko hilo.
Jitihada za kuokoa waliofunikwa na kifusi zikiendelea.
Wananchi wa Nepal wakishitikiana kwa pamoja kuvuta kamba. 

Ramani inayoonyesha sehemu iliyokumbwa na tetemeko hilo.
Picha zote kwa hisani ya Mtandao wa Daily Mail


MBOWE ALIPOUNGURUMA MKOANI SIMIYU

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe, akizungumza na halaiki ya vijana wa chama hicho muda mfupi baada ya kuifunga kambi ya mafunzo ya vijana hao iliyofanyika Kijiji cha Lagangabilili Wilaya ya Itilima mkoani Simiyu juzi.
Mamia ya wananchi wa Wilaya ya Itilima mkoani Simiyu, wakimshangilia Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe (hayupo pichani), katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye Uwanja wa Shule ya Sekondari Lagangabilili wilayani humo juzi.
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe, akihutubia mkutano wa hadhara katika Kijiji cha Lagangabilili Wilaya ya Itilima mkoani Simiyu juzi.
Wazee wa kabila la wasukuma wakimuombea kwa Mwenyezi Mungu, Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe, ili yeye na chama chake aweze kutawala nchi. Mbowe alisimikwa na kupewa zana za kitemi za kabila hilo na kuitwa jina la Mayego kabla ya kuanza kuhutubia mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye Kijiji cha Lagangabilili wilayani Itilima mkoani Simiyu juzi.


MECK SADICK :VYANDARUA VITUMIKE KWA MATUMIZI YALIYOKUSUDIWA SIO KUFUGIA KUKU

Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii.

SERIKALI  imeitaka jamii kutumia vyandarua  kwa malengo yaliyokusudiwa na sio vyandarua hivyo vitumike kwa ajili ya kufugia Kuku au kuvulia Samaki.

Hayo yamesemwa leo katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadick wakati wa maadhimisho ya siku ya Malaria Duniani ambayo hufanyika Aprili 25 kila mwaka.

Sadick amesema wafadhili mbalimbali wamekuwa wakiweka nguvu katika kupambana na Malaria hivyo ni wajibu jamii kutumia Vyandarua hivyo kwa malengo yaliyokusudiwa kwani kufanya hivyo kutaongeza uzalishaji wa uchumi katika nchi kutokana na kuwa na afya iliyo bora.

Katika maadhimisho hayo Mkuu Mkoa huyo amezindua mpango wa ugawaji wa Vyandarua milioni 24 kwa nchi mzima ikiwa ni jitihada za Serikali na wadau mbalilmbali kupambana na ugonjwa wa Malaria.

Amesema tangu kuanza kampeni hiyo ya kupambana na Malaria utafiti unaonyesha Malaria imepungua kutoka asilimia 18 mwaka 2012 na kufikia asiliamia 10 mwaka huu ambapo kupungua huko kumekwenda sambamba na kupungua kwa vifo vya wajawazito pamoja na vifo vya watoto chini ya miaka mitano(5).

Sadick amesema Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii na Wizara ya Kazi zinatakiwa kuweka utaratibu kwa makampuni mbalimbali kupambana na Malaria na sio kuwa sehemu ya hiari kwani kufanya hivyo kutaongeza ufanisi katika makampuni pamoja na viwanda.
Wananchi wa Mkoa wa Dar es Salaam wakiwa katika matembezi ya Maadhimisho ya siku ya Malaria Duniani ambayo hufanyika Aprili 25 kila mwaka, yaliyoanzia katika viwanja vya Msasani na kuishia viwanja vya
Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam leo.PICHA ZOTE NA EMMANUEL MASSAKA.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadick akikata utepe kuashiria uzinduzi wa ugawaji wa vyandarua katika maadhimisho ya siku ya Malaria Duniani yaliyofanyika leo katika viwanja vya Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam .
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadick akitoa hotuba yake katika maadhimisho ya siku ya Malaria Duniani katika viwanja vya Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam.
Mtoto Noel Peter akiwa amelala kwenye kitanda kilichowekwa Chandarua ikiwa ni ishara ya kampeni ya kupambana na Malaria katika maadhimisho ya siku ya Malaria duniani yaliyofanyika leo katika viwanja vya Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam leo.

BOFYA  HAPA KWA PICHA ZAIDI


KUSIMAMISHWA KWA SHINDANO LA UREMBO LA MISS TANZANIA KWA MISIMU MIWILI KUKO PALEPALE - BASATA

Katika siku za hivi karibuni kumekuwa na taarifa kwenye vyombo vya habari na mitandao mbalimbali ya kijamii kwamba shindano la urembo nchini maarufu kwa jina la Miss Tanzania limefunguliwa na Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) na kwamba Kampuni ya Lino International Agency LTD ambayo ni waendeshaji wa shindano hilo imewataka mawakala wake kuanza maandalizi ya shindano hilo.

Taarifa hizo za kufunguliwa shindano hilo zilienda mbali kwa kueleza kwamba mawakala wametumiwa kalenda ya mashindano hayo kwa mwaka huu.

Baraza linapenda kutoa ufafanuzi kama ifuatavyo:

1. Wananchi wapuuze taarifa hizo kwani kusimamishwa kwa shindano la Miss Tanzania bado kuko palepale kama ilivyoelezwa katika barua ya BASATA ya tarehe 22/12/2014 waliyoandikiwa Lino International Agency LTD ambayo pamoja na mambo mengine iliwataka warekebishe kasoro kadhaa zilizojitokeza. Walisimamishwa kwa misimu miwili ya mwaka 2015 na 2016 ili kujipanga upya na kurekebisha kasoro husika.

2. BASATA kama msimamizi na mratibu mkuu wa sekta ya Sanaa nchini ndilo lililolisimamisha shindano hilo baada ya kubaini mapungufu mengi. Kusimamishwa kwa shindano hili ilikuwa ni kwa njia ya kuufahamisha umma na kwa maana hiyo kama shindano litafunguliwa njia hiyo-hiyo ya  kutoa taarifa kwa umma itatumika na si vinginevyo. 

3. BASATA linatoa wito kwa Lino International Agency LTD kutumia muda wake mwingi kufanyia marekebisho mapungufu yaliyojitokeza ili mashindano haya yatakaporejea yawe na mikakati na hadhi kuliko ilivyo sasa. 

4. Aidha, Baraza linawataka wasanii na wadau wote kuzingatia sheria, kanuni na taratibu zilizopo katika kuendesha shughuli za Sanaa sambamba na kufuata mifumo sahihi ya mawasiliano.

Sanaa ni kazi, tuipende na kuithamini

Godfrey Mngereza
KATIBU MTENDAJI


DKT. SHEIN AFUNGUA JENGO LA AFISI KUU YA UHAMIAJI ZANZIBAR

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Kamishna Mkuu wa Uhamiaji Tanzania Sylvester Ambokile Mwakinyule wakati alipowasili kulifungua Jengo la Afisi Kuu ya Uhamiaji Zanzibar leo liliopo Kilimani Mjini Zanzibar akimuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akikata utepe kama ishara ya ufunguzi wa Jengo la Afisi Kuu ya Uhamiaji Zanzibar leo Kilimani Mjini Zanzibar akimuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete (kutoka kushoto) Kamishna Mkuu wa UhamiajiTanzania Sylvester Ambokile Mwakinyule na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Perera A.Silima.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akiangalia hatua za utengenezaji wa PassPort za Uraia wa Tanzania wakati alipotembelea sehemu mbali mbali baada ya kulifungua Jengo la Afisi Kuu ya Uhamiaji Zanzibar leo Kilimani Mjini Zanzibar akimuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete (kushoto) Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Perera A.Silima na (kulia) Inspekta wa Uhamiaji Hassan Suleiman Ameir.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (wa pili kulia) akipata maelezo kutoka kwa Asistance Inspekta Khamis Ali Haji (katikati)wakati alipotembelea katika chumba cha kumbukumbu za picha kwa Wananchi walioomba Passpoti za Uraia baada ya kulifungua Jengo la Afisi Kuu ya Uhamiaji Zanzibar leo Kilimani Mjini Zanzibar akimuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete. [Picha na Ikulu].


MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AKABIDHI TUZO YA UMAHIRI WA UANDISHI WA HABARI (EJAT) JIJINI DAR ES SALAAM

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia wakati wa hafla ya Utoaji Tuzo za Umahiri wa Uandishi wa Habari, iliyofanyika jana usiku April 24, 2015 kwenye Ukumbi wa Mlimani City, jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi mfano wa Hundi ya Sh. Milion tatu na Laki Nane (M.3.8) mshindi wa jumla katika kinyang’anyiro cha Tuzo za Umahiri wa Uandishi wa Habari (EJAT), Mwandishi wa habari wa Gazeti la Mwananchi, Mkinga Mkinga, wakati wa hafla hiyo ya utoaji tuzo iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Mlimani City, jijini Dar es Salaam, jana usiku Aprili 24, 2015. Kushoto ni Rais wa Baraza la Habari Tanzania, Jaji Mstaafu Robert Mihayo na Generali Ulimwengu.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi mfano wa Hundi ya Sh. Milioni kumi (M. 10) Mwandishi wa habari wa siku nyingi mkongwe, Generali Ulimwengu, wakati wa hafla hiyo ya utoaji tuzo iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Mlimani City, jijini Dar es Salaam, jana usiku Aprili 24, 2015. Kushoto ni Rais wa Baraza la Habari Tanzania, Jaji Mstaafu Robert Mihayo na (kulia) ni Mke wa Generali Ulimwengu.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi Tuzo mshindi wa pili wa jumla katika kinyang’anyiro cha Tuzo za Umahiri wa Uandishi wa Habari (EJAT), Mwandishi wa habari wa Gazeti la The Citizen, Lucas Liganga, wakati wa hafla hiyo ya utoaji tuzo iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Mlimani City, jijini Dar es Salaam, jana usiku Aprili 24, 2015.Mtoto Angel Machellah apokea Sakramenti ya Kipaimara katika Parokia ya Kimara

Askofu msaidizi wa Kanisa Katiloki Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Titus Mdoe (Kulia) akizungumza na Watoto waliopata Sakramenti ya Kipaimara katika Kanisa Katoriki la Kimara jijini Dar es Salaam jana.
Mtoto Angel Machellah (mbele) akiwa na watoto wenzie wakijiandaa kuingia kanisani wakati wa kupokea Sakramenti ya Kipaimara iliyofanyika katika Kanisa Katoriki Parokia ya Kimara Dar es Salam jana.


Wanasubiri kuvuka Barabara

Watoto ambao majina yao hayakupatikana mara moja wakiwa wamesimama kando ya Barabara ya Chang'ombe kusubiri kupungua kwa magari ili wavuke, kwenye makutano ya barabara Mandela na Chang'ombe jijini Dar es salaam leo. 


VIKOSI VYA ULINZI NA USALAMA MKOANI DODOMA VYAFANYA MAZOEZI YA PAMOJA


Na DORICE Kigombe wa Jeshi la Polisi Dodoma.

Jeshi la Polisi Mkoani Dodoma kwa kushirikiana na Idara mbalimbali za Serikali na wadau wa Amani Raia ,wamefanya matembezi/Routmatch ya pamoja kuzunguka mitaa mbalimbali ya mji wa Dodoma .Matembezi yaliongozwa na Mkuu wa Mkoa Dodoma Capt. Mstaafu CHIKU GALAWA.

Washiriki wa zoezi hilo ni Jeshi la Polisi, Jeshi la Wananchi (JWTZ), Jeshi la Magereza, Uhamiaji, Watumishi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Ofisi ya Mkuu wa Wilaya, Wafanya biashara, Raia wema na watumishi raia wa Vyombo vya ulinzi na Usalama Mkoani Dodoma.

Lengo la zoezi hili la pamoja ni kudumisha ushirikiano, mahusiano mema ya idara mbalimmbali za serikali na raia wema. Akiongea na washiriki wa zoezi hilo, Mh. Mkuu wa Mkoa Capt. Mstaafu CHIKU GALAWA alisema “mazoezi ni afya, ushirikiano ni furaha na kukuza Udugu. Aliwapongeza wote walioshiriki zoezi hilo na kuagiza kuwa litakuwa zoezi endelevu na litashirikisha Idara nyingi zaidi.
Mwenyekiti wa Kamati ya ulinzi na usalama Mkoa wa Dodoma,  Mkuu wa Mkoa Dodoma Capt. Mstaafu Chiku Galawa akiwa na wajumbe wakuu katika Routmatch leo.

Askari polisi wa Mkoa wa Dodoma wakiwa katika Routmatch leo.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Capt. Mstaafu Chiku Galawa akizungumza na washiriki wa Routmatch baada ya kuhitimisha zoezi katika viwanja vya bwalo la Polisi Dodoma leo.


UFAFANUZI WA TUME YA UCHAGUZI KUHUSU SWALA KURA YA MAONI KUHUSISHWA NA UCHAGUZI MKUU - PT 2


UFAFANUZI WA TUME YA UCHAGUZI KUHUSU SWALA KURA YA MAONI KUHUSISHWA NA UCHAGUZI MKUU - PT1


Waziri Membe apokea Nakala za Hati za Utambulisho kutoka Mabalozi Wateule wa Urusi na Algeria

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb), akipokea Nakala za Hati za Utambulisho za Balozi Mteule wa Urusi nchini Tanzania, Mhe. Yuri Fedorovich Popov.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb), akipokea Nakala za Hati za Utambulisho za Balozi Mteule wa Algeria nchini Tanzania, Mhe.Saad Belabed.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI


WAZIRI WA NCHI AKUTANA NA VIONGOZI WA WALEMAVU WA NGOZI NCHINI

Waziri wa Nchi ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge) Mhe. Jenista Mhagama (Mb) akisikiliza kwa makini hoja kutoka kwa Mkurugenzi Msaidizi Sera Wizara ya Mambo ya Ndani Bi. Joyce Momburi (hayupo pichani) wakati wa Kikao cha Pamoja na Viongozi wa Taasisi ya Watu wenye Ulemavu wa Ngozi (AKUAT)Ofisini kwake Aprili 24, 2015.
Waziri wa Nchi ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge) Mhe. Jenista Mhagama (Mb) akiwa na Viongozi wa Taasisi ya Watu wenye Ulemavu wa Ngozi walipomtembelea Ofisini kwake Aprili 24, 2015 kuzungumza masuala ya msingi yanayohusu ulinzi na usalama Woa. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).