Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. Jamani mbona sielewe, nje ya muungano hakuna Zanzibar wala Tanganyika, why? Mbona kabla ya muungano nchi hizo zilikuwepo na ndio zilizogombania uhuru wa nchi zao, Tanganyika mpaka Mwalimu wetu alienda UN kuudai, wenzetu kwa mapinduzi matakatifu. Uzuri wenzetu mpaka leo wapo pamoja na kwamba tunaambiwa tuliungana ikawa nchi moja, why Zanzibar ipo mpaka leo? Nadhani tuseme ukweli jamani, ndani ya muungano Zanzibar ipo na nje itakuwepo vilevile ni nchi. ndani ya muungano Tanganyika haipo ila nje ya muungano itakuwepo. Huo ndio ukweli.

    ReplyDelete
  2. sadakta umenene kweli tupu mdau wa mwanzo sina hata la kuongezea. tanganyika yetu ipo wapi?kila siku tunachekwa na wazanzibari kwa kutokuwa na tanganyika yetu sasa tutafute tanganyika yetu tumechoka danganya toto

    ReplyDelete
  3. mwalimu nyerere na karume fufukeni mtuambiyie huu muungano ukojeee tumeshachoka nao kizazi hiki kipya kinataka ukweli na haki na amani

    ReplyDelete
  4. Kuna watu mwanzoni walikua wakijifichaficha weee sasa hivi wameamua kua wazi na kuonesha hisia na misimamo yao.......

    ReplyDelete
  5. Mdau wa kwanza uko sahihi nje ya muungano Tanganyika itakuwepo lakini unasahau baada ya Tanganyika kuwepo, tutaanza kusema Tanganyika ni muungano wa kanda tano yaani kanda ya mashariki, magharibi, kusini, kaskazini na kati.

    Vile vile kwa Zanzibar, nje ya muungano, wataanza kusema Zanzibar ni muungano wa Pemba, Unguja na sijui na visiwa gani vile.

    So, argument hapa ni kuwa tutaendelea kubaguana, na kubaguana mpaka hata jirani yako utaanza kujiuliza ni wa kanda ipi.

    Tatizo wanasheria wanatuharibia mambo, wenyewe argument zao ziko kwenye maneno wanayoandika kwenye makaratasi, wakati social au political scientist yeye anaangalia real world events....

    ReplyDelete
  6. Tuliona Crimea ikitaka kujitenga Ukraine tukajua kuna mtu pembeni mara gafla wakajiunga Russia tukajua kuuuumbeee kuna watu wamewatumia wanasiasa wa Crimeaaa??!!! Ok sasa ukiona mwanasiasa wa Zanzibar au Bara anapiga kelele mpaka kuwatukana Wazee wetu basi ujue kwamba kuna mtu kajificha na kawatuma hawa watu wafanye hivyo!!!!

    Mwenye macho aone na aamke mapema ila tunasema tutapigana mpaka mwisho na Muungano wetu tutaulinda kwa vyovyote ila hamtokuja kuipata Gas yetu wala mali za Tanzania Ovyo kama ilivyo kwa Kongo, Iraq, Libya, etc.

    ReplyDelete
  7. Muungano juuuuuuuu, Muungano udumu milele, wasiotaka Muungano washindwe na walegeee.

    ReplyDelete
  8. Ankal iweke hii post as back on demand ili tuendeshe kampeni vizuri maana hata kama hatujapata nafasi ya kuwa wajumbe wa bunge la katiba basi tutumie Utanzania wetu kuwaonesha ulimwengu kwamba tunaotaka Utanzania wetu na tunautaka Muungano wetu na tupo tayari kuulinda kwa gharama yoyote ile.

    ReplyDelete
  9. Mimi husikitishwa watu wakakaa wakasema waarabu watarudi halafu wao wanakuja kuomba pesa huku arabuni misaada wewe njoo uone dunia huku choo cha muarabu nikizuri kuliko nyumba yako mimi watoto wangu nikiwambia twendeni mukatembee tz jibu kuchafu baba

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...