Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 19 mpaka sasa

  1. Shida ya hawa wanaomtukuna Nyerere na Karume ni kweli kukosa adabu, lakini pia ni kutoelemika. Wamesoma lakini hawakuelimika. Wao wanadhani ni bora kuliko Nyerere na Karume?
    Au na akina Mfaume Kawawa? Wana uchungu gani bwana!!
    Wanaweza kuchangia maendeleo bila kutukana hawa wazee.
    Waulize wao wanaweza kutukanwa na watoto wao? Matusi si ustaarabu wa mtanzania. Elimu yao wameipata wapi?
    Nawapa pole, asiyefunzwa na mama ye hufunzwa na ulimwengu.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Wapo greed na no value or morals zamani wabunge walikuwa wasomi haswa na wanaeleweka ukiwaona unatetemeka .sasa vi movie star bloggers mtu tuu na njaa yake anawekwa bungeni matokeo yake ndio Haya .Nilizaliwa 1974 ila kitu kimoja Nakumbuka ni jinsi nilivyolelewa kinidhamu wazazi wangu followed the rules masters degree walimakiza wakarudi Tanzania.Mshahara wa mtu wa masters I will never forget mzazi wangu alikuwa analipwa shillingi 20,000 hiyo 1982 hiyo ila safari za hapa na pale tuliishi na cheo chake kilikuwa officer tu .Hakuwahi kulalamika wala kulia alikuwa na Imani na Serikali ya Nyerere.Alivumilia wewe akahamia world bank pesa ya kumwaga lakini Baada ya miaka miwili mzazi a kasema ngoja nirudi serikalini tu .Aliacha mshahara wa million 5 kwa mwezi akarudi kwa seriali ya Nyerere Akaja kuwa waziri katibu mkuu and all that .jamani tusiwe na tamaa tuwe na Imani na tukumbuke tulipotokea.Enzi za Nyerere watu tulikula yangu ,Mkatte wa siha ,ila ni nasema kila siku thank you God Nyerere was our first president .Hivi mngepata Ghadafi ingekuaje ? Au ndio mnataka wakina Idi Amini?angalieni Zimbabwe huko.Jamani Muwe waangalifu

      Delete
  2. Bwana michuzina uchungu moyoni mwangu sana sababu mimi ni mtanzania nileyekulia Tanzania na Uganda nashindwa kuelewa matatizo ya hawa jamaa sijui nini ni upumbavu au wamelaniwa au ni wanatumiwa na wazungu sijui kauli kama haziwezi kubadilika yaliyotokea Rwanda au Uganda au Burundi au Congo au somalia yako kwenye kona wapinzani hawana adabu ata kidogo hata kidogo unawezaje kuita watu itarahamwe Ndugu lipumba na elimu yake ya juu ameita watuitarahamwe inaafaa aombe msamaha kwa lugha aliyotumia kama amesoma na anajiheshimu afikirihe lugha ariyotumia siyo sawa kabisa ata kidogo hayo ni mazarau ya ali yajuu hapa mimi namuona yuko na ajenda ameificha ndani ya moyo wake.hili ni bunge ghani la katiba watu wanatukanana sawa sawa wenda wazimu watu hawana heshima kwa wasisi wa taifa letu hawaoni yaliyotokea nchi nyingine inasikitisha sana watu wanafirikiria maendeleo watu wanaleta ujinga na kujifanya wamesoma shame on you shame on you you dont deserve to represent the people of this land shame on you mr lipumba shame on you,
    Mr Musa

    ReplyDelete
  3. Yaani nina hasira mbaya sana na huyu mkosa adabu tundu lissu utafikiri J.Nyerere ni baba yangu...mtu kasomeshwa buree na shule ndio iliomleta mjini mzizima leo anajidai anajua zaidi kuliko watanzania millioni 45...anyway uroho wa madaraka na njaa ndio vinamsumbua nitashangaa sana kama huyu mtu ataweza kurudi tena mjengoni come 2015..Come on you CCM- COYC....mpelekeni mtu shupavu jimbo la huyu mkosa adabu ili asirudi tena huko kufanya vurugu mjengoni..
    mdau wa UK

    ReplyDelete
  4. Mimi sikusikia tusi lolote alilotukanwa muasisi yeyote. Walioongea wamesema ukweli mtupu, kuna mambo mengi yamefichika kwenye huu muungano. Tunataka tuuboreshe ili uende na wakati na usiwe na mapingano ya kikatiba kama ilivyo sasa. Nadhani jambo muhimu na kubwa ni kuboresha ili uwe mzuri, haya mambo mnayoongelea kuhusu kutukanana hayana tija wala umuhimu. Napata shaka nikiona kuwa rais wa jamhuri ya muungano akiwa hana sauti huko Zanzibar, kule siyo amiri jeshi mkuu wala hahusiki hata kugawa mikoa.....Huyo atakuwa rais gani wa muungano asiye na madaraka katika moja ya states yake? Tuujadili huu muungano na tuutafutie dawa ya moja kwa moja, kwa sababu hakuna aina hii ya muungano popote duniani. Tuwe wawazi jamani ndugu zangu...Tuelezwe pia mji mkuu wa nchi yetu ni wapi, maana hadi leo nashindwa kuelewa kama ni Dodoma au Dar es-Salaam.

    ReplyDelete
  5. mdau namba mbili unafurahisha sana.unataka kufananisha Libya na Tanzania?are you serious au unatania?

    ReplyDelete
  6. Hayo ndio mambo ya kwenda kijiushule shule na ushule ushule usioeleweka. Kusoma kwingi, kuandika kwingi, UZOEFU mwingi wa ulaini wa kuchambua masuala mbali mbali, ama kuchambua kwa ufanisi, ama bila ufanisi, ama kuchambua kwa kiufisadi nk. Lakini KUELIMIKA ni suala LINGINE NA TOFAUTI kabisa. Suala lililo JUU ya elimu ya aina yoyote ile tunavyoijua (aidha elimu ya juu au ya chini). Gumu tena gumu sana suala hili. Lakini. WALIOELIMIKA WAPO. KUELIMIKA (YAANI KUELIMIKA) INAWEZEKANA.

    ReplyDelete
  7. JK naona unasahau kuwa sisi ni binadamu , na ukikubali kuwa ni binadamu huwezi kuwa mtakatifu lazima utateleza ufanye makosa , na aliye mbora ni yule mwenye kukubali kosa na kuomba msamaha sio kutetea kosa lake, mwl nyerere na karume wote walikuwa na makosa yao,sio lazima wanachoacha waasisi lazima kiendelee ikiwa kuna njia ya kuboresha au hata kubadili mwendo kwa faida ya wengi basi ifanyike , kwa mfano unaweza ukarithi nyumba ya mzazi wako aliefariki lakini kutokana na haja ukaiuza au ukaivunja na kujenga nyengine , jee itakuwa umefanya kosa ?

    ReplyDelete
  8. Tena HUYU TUNDU Kasoma kwa hela ya serikali ya nyerere mpaka majuu kapanda kwa hela za CCM/NYERERE. HE GAT NO VALUES AT ALL. Ukiishaona mtu anaanza na matusi huyo si muungwana, halafu wanategemea TUMPE NCHI SI NDO ATATUNYEA MKONONI SIYE WALALA HOI. Mtu ukisoma lazima ujitofautishe na wale wasioenda shule!! HAYA UN IMETOA DOCUMENT YA MUUNGANO NA ILIPITISHWA 1964 NA CONTACT ZAO ZIMEWEKWA WAZI MWAMBIENI ASITUPOTEZEE MUDA NA KUPOTEZA PESA ZA WANANCHI LET HIM GO TO UN AND QUESTION MUUNGANO. UNITED REPUBLIC OF TANZANIA NI MOJA YA NCHI ZINAZOTAMBULIKA HATA UN KWENYE WATU WALIOSOMA.

    KAAAAAAAA YAANI HILI BUNGE LIMECHUSHA

    ReplyDelete
  9. Nakubaliana na mtoa maoni ambaye hakusikia tusi lolote, nami pia sikusikia wala kusoma tusi katika matamshi ya Tundu Lissu zidi ya ufafanuzi. Hali ilifikia hapa baada ya kuwepo sintofahamu ya wapi hati ya muungano ilipo, tukiwa open na mambo yetu ni rahisi kuondoa mikanganyiko, sasa ndiyo tunaona umuhimu wa kuweka copy makumbusho ya taifa. Kuhusu matumizi ya lugha isiyofaa aliyotuhumiwa Lipumba, mtoa maoni yuko bias, juzi Lukuvi amewaita CUF kuwa ni uamsho na amewatisha wananchi jeshi kuchukua nchi zikiruhusiwa serikali tatu, wajumbe kadhaa wa ccm toka Zanzibar wametumia kauli za kibaguzi dhidi ya Maalim Seif na watu wanaefanana naye, je hii si hatari inayopaswa kulaaniwa?

    ReplyDelete
  10. Nani aliyetutakana waasisi?ivi kuchambua baadhi ya mambo na kuyaweka hadharani ni kutukana?Yawezekana waasisi wanatukanwa kwa kutofanya waliyoyaacha.Nakumbuka juzi tu ktk video moja ya mafuriko pale jangwani kuna mkazi mmoja alisema, mara baada ya nyerere hakuna tena viongozi.....yule mtu nae ana tafsiri yake ya watu wanaomtukana mwasisi.....

    ReplyDelete
  11. Bwana Michuzi natumai Blog yako itakuja kuwekwa kwenye vitabu vya historia kwa michango yake juu ya issues za jamii. Hivyo kaza buti, usipendee upande wowote! Tanzania tunakosa uvumilivyu, sielewi ni kwanini mtu akitoa maoni yake anaishia kukejeliwa na kutukanwa. Yote yaliyoandikwa hapa yanaonyesha chuki kwa bwana Lisu ambaye ni mtanznia na mwakilishi wa jimbo la watnzania. Lisu kasoma vipengele vya katiba ya Zanzibar. Ni vizuri tukatumia hoja na sio nguvu kupata mwafaka wa hili swala muhimu la muungano badala ya kupotosha ukweli. cyber space ni kubwa mno. Yote yanayoandikwa hapa yatakuwepo milele daima. Viongozi wetu waondokane na ile tabia ya kutumie "ujinga" wa watanzania kuongoza. Lisu anapata hoja nyingi na wafuasi wengi kwasababu anatumia mikataba iliyoandikwa na watanzania na wazanzibar kujenga hoja zake.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Inahitaji uwe umekunywa mvinyo kutetea hadharani baadhi ya matukio na vituko vilivyotokea huko Bungeni Dodoma. Nimesikiliza hadi video za YouTube. Nimesikia maneno makali sana kama wajumbe kuitwa Interahamwe. Walozoea vya kunyonga...Mwl Nyerere alikuwa ....na mengine mengi. Na hayo yanasemwa na watu wanaofikiria kuwa siku moja watapewa nchi. Hawa wakienda Ikulu si hati ya Muungano wataichoma moto? Maana hawaitambui!!! Hawa wanakataa tu hoja je watakubali kutumia nguvu kuulinda Muungano wakiwa ikulu? Mtanzania yeyote hawezi kukubali jambo linaloashiria kupotea amani utulivu na mshikamano wa JMT.

      Delete
  12. Kila binadamu anakuwa na mapungufu. Watu wakI criticize mapungufu sio matusi. Yes the Union has bewn there for 50 yrs but it is a weird and unique one. Why the government is scared to run a referendum? Give power to the people to decide. If Zanzibarians don't want th e union why force them? People should be educated the benefits of the Union and then let them vote through the referendum.

    ReplyDelete
  13. Mwanasiasa mwenye tamaa ya madaraka ndio anataka Muungano ufe ili aweze aje kuwa Rais wa Zanzibar, Tanganyika au Tanzania lakini SISI WANANCHI WA KAWAIDA HATUTAKI MUUNGANO UFE ATA SIKU MOJA NA TUTAUPIGANIA KWA VYOVYOTE!

    Hao wanasiasa tunajua wametumwa na tutawanyamazisha wote hadi wale waliowatuma. Tutalinda nchi yetu, watu wake na rasilimali zake na hamtozipata ovyo ovyo kama Kongo na Iraq ata siku moja.

    Mwenye macho aone na amke sasa toka usingizini. Kwanini hawa watu wamekuja sasa wakati tuna Gas reserve kubwa? Kawaulizeni hayo maswali kina Lisu, Lipumba na vibaraka wengine wanaotumiwa!!

    Mr Michuzi usibanie ujumbe huu ili wananchi wa kawaida waone madudu ya Upinzani na Vibaraka waliohaidiwa madaraka na utajiri toka kwa masters wao.

    ReplyDelete
  14. WATANZANIA TULIO NJE YA WAJUMBE WA KATIBA TUNAWATEGEMEA KUPATA TUNDA ZURI KUOKA KWAO.
    LAKINI TABIA WALIYOIONYESHA NI AIBU TUPU.
    LUGHA CHAFU
    HAWANA HESHIMA
    WANAFANYA KAMPENI
    KIBURI
    DHARAU
    N.K

    ReplyDelete
  15. wapinzani wanalazimisha serikali tatu ili kwanza wauvunje Muungano wakudhani kwamba watagawana nchi ili waitawale. Tamaa ya madaraka. wanasaidiwa na Kagame kuivuruga nchi kwa vile Kagame ana hasira na wale intarahamwe waliokuwa Congo ambao askari wa Tanzania walienda kuwazuia askari wa Rwanda wasipigane nao.N a hiyo ndiyo siri ya profesa Lipumba kuwaita wenzie intarahamwe. Lipumba akiwa overexcited huwa anaropoka neno lolote lile. Sasa this time kajiaibisha maana ametoboa siri ya kufadhiliwa kwao na Kagame maana Kagame yeye anawaita watanzania itarahamwe kwa kitendo cha kwenda kuwatoa askari wa Rwanda Kongo.

    ReplyDelete
  16. Kwa maana nyengine ya tafsiri ya Lipumba kijuu juu ni nikuwa Lipumba,limepumbaa katika medani ya uwanja wa siasa.Wanasema wanafalsafa kuwa knowledge is power,Lipumba anayo knowledge lakini knowledge yake si power,maana application of knowledge is power.Maana anashindwa kui apply knowledge yake katika kuipatia mstakabala mwema Tanzania na badala yake anavuruga. Sasa jee akaenda Ikulu itakuwaje watanganyika?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...