Airtel Public Relations Manager Jackson Mbando speaks to the media at a press conference to announce the forthcoming Manchester United International Soccer Clinic to be held in Dar es Salaam from 23rd-27th April under the tutelage of coaches from Manchester United Soccer Schools.  He is flanked by the Tanzania Football Federation (TFF) President Jamal Malinzi .The event was held at the Airtel Tanzania Headquarters, 18th April 2014. 
 Tanzania Football Federation (TFF) President Jamal Malinzi speaks to the media at a press conference to announce the forthcoming Manchester United International Soccer Clinic to be held in Dar es Salaam from 23rd-27th April under the tutelage of coaches from Manchester United Soccer Schools.  He is flanked by Airtel Public Relations Manager Jackson Mbando.The event was held at the Airtel Tanzania Headquarters, 18th April 2014.

========  =======  ========
Washiriki wa kliniki ya Airtel Rising Stars kutua Dar Jumatatu
·      Ni kutoka nchi 12 Afrika
·      Waziri Bernard Membe mgeni rasmi siku ya ufunguzi
·      Kliniki kuendeshwa na makocha kutoka Manchester United

Dar es Salaam, Ijumaa 18 Aprili, 2014.  Wachezaji wa soka chini ya umri wa miaka 17 kutoka nchi 12 barani Afrika wanatarajiwa kuwasili jijini Dar es Salaam Jumatatu Aprili 21 kushiriki kliniki ya soka ya kimataifa.  Hii ni mara ya pili Tanzania imepewa heshima ya kuwa mwenyeji wa kliniki ya kimataifa baada ya ile iliyofanyika kwenye uwanja wa wa kisasa wa Taifa mwaka 2011.

Kliniki ya mwaka huu itakayofanyika kwenye uwanja wa Azam, Chamazi, nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam inakutanisha wachezaji chipukizi, wasichana na wavulana, kutoka nchi za Kenya, Uganda, Malawi, Sierra Leone, Burkina Faso, Chad, Congo Brazzaville, DRC, Niger, Madagascar, Gabon, Seychelles na mwenyeji – Tanzania. Mafunzo hayo ya siku tano mfululizo chini ya makocha wazoefu kutoka klabu maarufu duniani ya Manchester United yana lengo la kuwapa vijana mbinu mbalimbali za kisoka hasa katika eneo la ushambuliaji.

Kliniki hii ya kimataifa inashirikisha vijana waliofanya vizuri mwaka jana katika mashindano ya Airtel Rising Stars kwenye nchi zao pamoja na washindi wa mashindano ya kimataifa yaliyofanyika nchini Nigeria ambapo timu ya wasichana ya Tanzania ilitwaa uchampioni wa fainali hizo hizo.

Hafla ya uzinduzi wa kliniki hiyo imepangwa kufanyika siku ya Jumatano kwenye uwanja wa Azam na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mheshimiwa Bernard Membe atakuwa mgeni rasmi.  Membe anatarajiwa kuwahamasisha vijana kujituma ili kuweza kuendeleza ipasavyo vipaji vyao vya soka.

Hafla hiyo ya uzinduzi pia inatarajiwa kuhudhuriwa na mabalozi kutoka nchi zinazoshiriki kwenye kliniki hiyo itakayojumuisha mafunzo ya uwanjani na ya darasani. Vipindi vyote hivyo vitafanyika pale pale Azam Complex.

Program ya Airtel Rising Stars ni mpango wa maendeleo ya soka kwa vijana chini ya umri wa miaka 17 barani Afrika ukidhaminiwa na kampuni ya simu za kiganjaji ya Airtel na kuungwa mkono na Manchester United. Lengo lake ni kusaidia kuibua vipaji vya soka kutoka ngazi ya chini (grassroots) hadi Taifa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...