Kamishna wa Polisi Kanda Maalum ya Dar Es Salaam,Suleiman Kova akizungumza na Vyombo vya habari mbalimbali mapema leo, makao makuu ya jeshi la polisi jijini Dar kuhusiana na sakata la viungo vya binadamu vilivyokamatwa jana INGIA HAPA KUONA TUKIO HILO.Kamanda Kova amesema kuwa watu wanane wamekamatwa kuhusiana na tukio hilo.

Kamanda Kova amesema kuwa jopo la Wataalamu saba limeundwa kuchunguza tukio hilo na amethibitisha kuwa viungo vile vilikuwa ni vya maiti,ambavyo hutumika na madaktari kwa elimu ya matibabu na utafiti.  

Pia amekanusha kwamba gari nyeupe la Pick-up (pichani kulia) iliyoonekana kubeba mifuko ya plastiki haikuwa linahusika na tukio hilo, bali baada ya kuliona na kusikia harufu kali ikitoka humo, walioliona likielekea dampo wakadhani ni mojawapo ya magari yanayobeba viungo hivyo. 
"Wananchi wakalifukuza gari na walipomkamata dereva kumlazimisha arudi dampo, akawa hana jinsi ila kwenda kituo ch polisi Bunju kujisalimisha. Zogo likaumuka hapo kituoni kiasi hata polisi wakatumia nguvu za wastani na kuwatawanya.
"Huyu dereva alikuwa kabeba mabaki.... ila siyo ya binadamu... Alikuwa kabeba mabaki ya kuku akitiokea kiwanda cha kuku cha Interchick", alifafanua Afande Kova na kuzua kicheko cha mshangao toka kwa wanahabari.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 22, 2014

    Tuonyesheni picha ya hao mlowakamata maana ni tukio kubwa sana hili linahitaji majibu na linashtua

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 22, 2014

    ukiona picha zitakusaidia nini?

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 22, 2014

    Human bodies should be treated with uttermost respect. Kila maiti anastahili kusitiriwa kwa heshima. That's common knowledge. To have a "higher" learning institution doing that is despicable. Chuo kilichofanya udhalilishaji huu kifungiwe.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 22, 2014

    Sasa kumbe katika tukio hili tahasisi za elimu ya udaktari wa binadamu zinausika ? kwamba ndugu zetu wakipotea basi maiti zao utumika katika utafiti wa madaktari?
    kazi kweli ipo.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 22, 2014

    Jamani imefikia mahali mtu unajuliza utu wa binadamu umekwenda wapi ? What happed to human values ? Heshima haipo kabisa karibu kila mahali. Eti tumeendelea. Amani inatoweka kwa kasi kubwa tena kila nyanja ni hesabieni ipo wapi ? Sehemu chache, kisa watu wapo busy na biashara, kuuwana sasa kunaelekea kuwa kitu cha kawaida kama vile watu kupotea. Kubiwa, kugongwa, kunyanyaswa mashospitalini....aaahhh, tafrani tupu. Sasa niambieni ipo wapi Amani, kila leo Arusha mlipuko, na hamna mtu anashikwa !!!! Mambo ya tindikali, mvurugano katika bunge, ilimradi tunaanza kuonekana hatuna muelekeo. Wadau, haya yote yatatupeleka wapi ? Viongozi wetu hawana muda wala mpango wa kuyatatua, wapo busy na pa diem zao! Tule tusile, tuuwawe tusiuawewe haya wahusu....inge wahusu wangefanya bidii siyo ....kweli changa moto ipo.......tena kali sana. Ni nini hasa kitatuamsha ? Nani aturudisha Amani ? Mimi na wewe....kila mtu afanye kila analoweza kurudisha Amani. Wazazi mpo ? Tuzidi kuwajibika. Walimu mpo tusaidiane na wazazi? Kuna njia mbalimbali za asili kama kufundwa virudishwe, watu tujifunze ku balance vya asili na maadili mazuri ya kisasa. Vinginevyo, tutakuwa wakimbizi wa nani ???????

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 22, 2014

    KAMA KAWAIDA TUKIO HILI LITAISHA KIMYA KIMYA.
    POLISHI HESHIMU MAITI.
    KILA MAITI INATAKIWA KUPEWA HESHIMA.
    TUNAOMBA WAZIRI WA MAMBO YA NDANI AFATILIE SUALA HILI KWA UKARIBU SANA.

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 22, 2014

    Shame on IMTU

    ReplyDelete
  8. AnonymousJuly 22, 2014

    Mimi binafsi naomba serikali itoe majibu sahihi kuhusu jambo hili, kwani kumekuwa na maswali mengi na sintofahamu miongoni mwa Watanzania tulio wengi.

    ReplyDelete
  9. AnonymousJuly 24, 2014

    huu ni unyama na udhalilishaji mkubwa,kama vilikuwa vinatumika katika mafunzo na kazi yake imekwisha kwa nini msivisitiri pahaka husika panapostaili,mnaenda kuvitupa dampo ili iweje? huo ni ukatili.shame on IMTU

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...