Mazishi ya Mzee John Fedha Macha (pichani), Mfanyabiashara maarufu na mmiliki wa Bamboo Bar ya Kinondoni (jirani na makaburi ya Kinondoni)  jijini Dar es salaam, ambaye alifariki dunia Jumatatu Julai 21,  2014 katika hospitali ya TMJ Mikocheni alikokuwa akitibiwa, yanatarajiwa kufanyika siku ya Ijumaa Julai 25, 2014 kijijini kwake Kirua Vunjo, Moshi, mkoani Kilimanjaro. 
Kwa mujibu wa ratiba iliyopatikana na Globu ya Jamii, Shughuli za kuaga mwili wa marehemu zitafanyika nyumbani kwake Kunduchi (jirani na Bahari Beach Police Post) jijini Dar es salaam, kuanzia saa tano asubuhi.
Baada ya chakula na kuaga,  mwili wa marehemu utapelekwa katika kanisa lililopo jirani na kwake kwa misa. Kisha safari ya kuelekea Moshi itaanza. 

Marehemu Mzee John Fedha, aliyekuwa mwanachama wa Klabu ya michezo ya TAZARA ya Kinondoni, atakumbukwa sana kwa ucheshi wake pamoja na uwezo mkubwa wa kufanya bishara ya supu na nyama choma.

Globu ya Jamii inaungana na familia, ndugu jamaa na marafiki wa marehemu katika kuomboleza kifo cha rafiki yetu, kaka yetu na mwanamichezo mwenzetu, Mzee John Fedha. 
Sisi tulimpenda sana, lakini Mwenyezi Mungu kampenda zaidi
Jina la Bwana na Lihimidiwe
AMIN

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 23, 2014

    R.I.P John Fedha, tutakumbuka ucheshi wako na bidii yako katika kuhakikisha wateja wanapata huduma bora.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 23, 2014

    RIP John Fedha

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...