Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe akizungumza na maelfu ya Waumini wa Karismatiki Katoliki, Jimbo la Dar es Salaam katika maombi maalumu kwa ajili ya kuliombea Taifa yaliyofanyika Kituo cha Karismatiki, Ubungo jijini Dar es Salaam. 
Waziri Chikawe ambaye alikuwa mgeni rasmi katika maombi hayo aliyataka Makanisa nchini kudumisha amani na utulivu na kuendelea kuliombea Taifa na kuepuka kuingia katika migogoro mbalimbali ambayo itasababisha taifa kuingia katika uvunjifu amani makanisani. 
Aidha, Chikawe aliongeza kuwa migogoro katika Makanisa na Madhehebu mbalimbali nchini imekuwa mingi katika kipindi hiki ambapo migogoro hiyo inasababishwa na ubinafsi wa viongozi, kutofuata Katiba na Ubadhirifu wa mali za Kanisa. 
Kutokana na migogoro hiyo Chikawe alisema “Serikali haitavumilia vitendo vya uvunjifu wa amani makanisani na ikibidi itafuta usajili wa madhehebu na makanisa yenye migogoro ili kuepusha shari”.
 
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (wapili kushoto) akiungana na maelfu ya Waumini wa Karismatiki Katoliki, Jimbo la Dar es Salaam katika maombi maalumu kwa ajili ya kuliombea Taifa. Maombi hayo yalifanyika katika Kituo cha Karismatiki, Ubungo jijini Dar es Salaam.
Picha na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...