Kampuni ya Mitandao ya simu za Mkononi ya Tigo imejitolea kushirikiana na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwenye sekta ya uwekezaji katika masuala ya mitandao ya mawasiliano sambamba na kusaidia huduma za Kijamii kwa wananchi wa Visiwa vya Unguja na Pemba.

Makamu wa Rais wa Kampuni hiyo yenye Makao Makuu yake Mjini Stokholmes Nchini Sweeden Bwana Arthur Basting alieleza hayo wakati akizungumza na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi Ofisini kwake katika Jengo la Msekwa ndani ya Viunga vya Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mjini Dodoma.

Bwana Arthur Basting ambae anasimamia Kampuni Tigo Barani Afrika alisema Uongozi wa Taasisi hiyo imejikita kutoa ushirikiano huo ikizingatia zaidi umuhimu wa mawasiliano ya Teknolojia yaliopo hivi sasa Ulimwenguni kote.

Bwana Arthur alisema Uongozi wa Kampuni ya Tigo unafurahia kuona kwamba Teknolojia ya Mawasiliano kupitia simu za Mikononi hivi sasa imeenea na kupokelewa vyema na wananchi wa Bara la Afrika.

Naye Meneja Uendeshaji wa Kampuni ya Tigo Hapa Tanzania Bibi Sylvia Balwire alimueleza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif kwamba Kampuni hiyo tayari imeanza mipango maalum ya kusaidia huduma za Kijamii katika maeneo mbali mbali hapa Nchini.

Akitoa shukrani zake Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi aliuomba Uongozi wa Kampuni ya Tigo kuongeza nguvu zake zaidi katika kusaidia miradi ya Kijamii ambayo bado inaonekana haijawa na nguvu za kujiendesha yenyewe.

“ Hadi wakati huu tunaozungumza zipo skuli zetu nyingi hazijawa na vikalio, huduma za maabara na Maktaba, hata vifaa katika vituo vyetu vya Afya. Uwepo wenu kama wawekezaji unaweza pia kuyaangalia maeneo hayo muhimu kwa ustawi wa Jamii yetu “. Alisema Balozi Seif.
Makamu wa Rais wa Kampuni ya Tigo yenye makao Makuu yake Nchini Sweeden Bwana Arthur Basting akisalimiana na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi Ofisini kwake Jengo la Msekwa ndani ya Viunga vya Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mjini Dodoma. Kati kati yao Ni mshauri wa Kampuni hiyo Balozi Ami Mpungwe.
Makamu wa Rais wa Kampuni ya Tigo Bwana Arthur Basting akimueleza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif nia ya Kampuni hiyo ya kutaka kushirikiana na SMZ Katika miradi ya mitandao ya mawasiliano.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akiwa katika picha ya pamoja na ujumbe wa Kampuni ya Tigo aliokutana nao kwenye ofisi yake iliyop[o jengo la Msekwa ndani ya Bunge la Jamuhuri ya Muungano Mjini Dodoma. Kulia ya Balozi Seif ni Makamu wa Rais wa Kampuni ya Tigo Bwana Arthur Basting na kulia yake ni Meneja Uendeshaji wa Tigo Tanzania Bibi Sylvia Balwire, Mshauri wa Kampuni hiyo Balozi Ami Mpungwe na Meneja Mkuu wa Tigo Nchini Tanzania Bwana Diego Gutierrez. Picha na Hassan Issa wa – OMPR – ZNZ.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...