Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Samuel Sitta akiongea na waandishi wa Habari huku akiwaasa kuacha chuki katika masuala yanayohusu mchakato wa Katiba.
Mjumbe wa Kamati Namba Nne ya Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Christopher Ole Sendeka akiongea na wandishi wa Habari kuhusu kazi na majukumu ya Kamati yake leo 28 Agosti, 2014.
Mjumbe wa Kamati Namba Tatu ya Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Dkt. Francis Michael akiongea na wandishi wa Habari kuhusu kazi na majukumu ya Kamati yake leo 28 Agosti, 2014.
Mjumbe wa Kamati Namba Moja ya Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Ummy Mwalimu Ally akiongea na wandishi wa Habari kuhusu kazi na majukumu ya Kamati yake leo 28 Agosti, 2014.
Mjumbe wa Kamati Namba Kumi na Moja, Mhe. Hamad Massauni akiongea na wandishi wa Habari kuhusu kazi na majukumu ya Kamati yake leo 28 Agosti, 2014. (Picha zote na Benedict Liwenga, Maelezo-Dodoma)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Waandishi chuchumilieni na mpate kitu kiitwacho verification of evidence of news items ili mpate truth as opposed to mere belief and faith anf belief. Kumbukeni kupata knowledge based on observation and experience or facts.

    Zaidi, achaneni na u-"clerkism"au u"stenographerism".

    Mwisho, sijui hawa waandishi wetu wa habari wamewahi kusoma nakala za gazeti la Mambo Leo? Gazeti hili, lilianzishwa na Wakoloni; lakini waandishi wake walikuwa makini kweli, japo hawakufundishwa uandishi - wengi walikuwa ni makarani, walimu na mapolisi.

    Ningependekeza wanafunzi wetu wa uandishi wa habari wawe wanazipitia nakal zake na kuzichambua.

    Ni uandishi mzuri.
    Ni historia nzuri, ikiwa ni pamoja na kujaa historia ya Makabila.
    Ni upanuzi wa elimu, na mashahiri yake mazuri.
    Ni habari za kutoka mikoani (majimboni).
    Na kadhalika.

    Najua nakala zake zimejaa hapo Maktabani Dar es Salaam, Wizara ya Habari na hata pengine kwenye Jumba la Makumbusho. Nendeni mkazichunguze nakala zake!

    ReplyDelete
  2. Ujanja mwingi mbele kiza, Usitukane wakunga na uzazi ungalipo, Usitupe jongoo na mti wake,Lisilo faa leo litakufaa kesho, Ukiishi nyumba ya vioo usigombane na kichaa,Kiswahili kimejaa misemo mingi ya busara ambayo inatufunza kila siku sisi Watanzania ila tatizo ni moja tu hatupendi lugha yetu tanu ya Kiswahili......

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...