Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Kamishina Msaidizi wa Polisi (ACP) EMMANUEL G. LUKULA
Na Sylvester Onesmo wa Jeshi l
a Polisi Mkoa wa Dodoma.Jeshi la Polisi mkoani Dodoma limetoa tamko la kuzuia maandamano ya Chama cha CHADEMA hapo tarehe 18/09/2014 na kuwataka wananchi kuyapuuza.
Akiongea na waandishi wa habari, Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Kamishina Msaidizi wa Polisi EMMANUEL G. LUKULA (ACP) alisema kuwa; Kufuatia Viongozi wa CHADEMA kutaka kufanya maandamano kuelekea viwanja vya Ofisi za Bunge Mkoani Dodoma kwa ajili ya kupinga Bunge la Katiba siku ya tarehe 18/09/2014 linaloendelea, kuwa maandamano hayo ni batili na akiwataka wananchi wakazi wa Dodoma kuyapuuza kwa kuwa yanakiuka Sheria iliyoliweka Bunge hilo.

Kamanda LUKULA  alitaja sababu za msingi za kuzuia maandamano hayo kuwa ni:-
1. Siku ya maandamano ya tarehe 18/09/2014 ni siku ya kazi ikiwa ni pamoja na muda wa maandamano hayo ni masaa ya kazi saa 04:00 asubuhi hadi saa 06:00 mchana yataathili ufanisi wa watu waliopo makazini/maofisini.
2. Bunge maalumu la Katiba linaloendelea kwa sasa lipo Kisheria na hakuna tamko lolote lililotolewa na Mahakama yoyote kulisitisha, hivyo moja ya kazi ya Jeshi la Polisi ni kulinda Sheria na wale wanaofuata sheria. Hivyo kufanya maandamano yanayopinga Bunge la Katiba ni kukiuka Sheria iliyoliweka Bunge hilo.
3. Kuna kesi Mahakamani ya kupinga Bunge hilo kuendelea, hadi sasa shauri hilo linaendelea Mahakamani. Hivyo kwa CHADEMA kuandamana ni kuingilia Uhuru wa Mahakama.
4. Baadhi ya Wilaya barua za kufanya maandamano zimechelewa kufika kwa Wakuu wa Polisi Wilaya kabla ya saa 24 kisheria.

Aidha Kamanda Lukula  alitoa wito kwa wananchi wa Dodoma kupuuza maandamano yoyote ya kupinga uwepo wa Bunge la Katiba kwani ni batili. Aidha aliwashauri viongozi wa CHADEMA Mkoa na Wilaya za Dodoma wayasitishe maandamano hayo na wasipo ridhika, wakate rufaa kwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi kwa maelekezo zaidi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...