Maryam Himid/Saada Saleh-ZJMMC

Waziri wa Habari Utamaduni Utalii na Michezo,Zanzibar,Mh. Saidi Ali Mbarouk amezitaka Taasisi zinazosimamia kupokea Watalii Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Amani Abeid Karume kujenga mashirikiano ili kuondosha usumbufu kwa wageni wanaoingia na kuotoka nchini. Ameyasema hayo alipofanya ziara Uwanjani hapo kwa lengo la kuangalia hali halisi ya Wageni wanaoingia na kutoka nchini.

Waziri Mbarouk amesema suala la Mashirikiano kwa wageni ni jambo muhimu linaloweza kuijengea sifa kubwa Zanzibar kwa wageni ambao wanakuja ambao wataweza kusimulia watakaoporudi ziara zao.

Ametoa wito kwa Taasisi husika kuhakikisha Wageni wanaoingia Zanzibar wanapata huduma stahiki na ili kuepukana na usumbufu wa aina yoyote wanapofika katika Uwanja huo wa Ndege.

Kwa upande wake Daktari wa kituo cha Afya uwanjani hapo Juma muhammed Juma amesema Wanaendelea kulisimamia vyema suala la kuwakagua kwa Vifaa maalumu Wageni wanaoingia kutoka Nchi zilizoathirika na Ugonjwa wa Ebola.

Amezitaja Nchi hizo kuwa ni pamoja na Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo, Liberia na Sera lion ambapo amesema kila abiria kutoka nchi hizo lazima Apimwe ili kuweka kinga ya Ugonjwa wa Ebola nchini.

Hata hivyo Mkurugenzi wa uwanja wa ndege Juma Saleh Juma ameelezea baadhi ya changamoto zinazowakabili uwanjani hapo kuwa ni pamoja na upungufu wa maeneo ya kukaribisha wageni,maegesho ya Magari na Uhaba wa Wafanyakazi wanaozungumza Lunga ya Kitaliano kutokana na Wataliano hao kutumia lugha yao tu.

Katika ziara hiyo Waziri Mbarouk alitembelea maeneo mbali mbali Uwanjani hapo ikiwemo Mapokezi, Maegesho ya Ndege na Magari na sehemu ya Mapumziko ya Abiria.
Waziri wa Habari Utamaduni Utalii na Michezo Zanzibar, Saidi Ali Mbarouk Mwenye Koti Jeupe akipewa Maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa uwanja wa ndege Juma Saleh.Katika ziara hiyo Waziri Mbarouk alitembelea maeneo tofauti ya Uwanja wa Kimataifa wa Abeid Aman Karume. Baadhi ya Wageni kutoka nchi tofauti wakipata huduma kutoka Uhamiaji mara baada ya kuwasili Uwanja wa Abeid Aman Karume. Picha na Yussuf Simai-Maelezo Zanzibar.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Hicho kichwa cha khabari (Heading) nakhisi kama vile kina utata, maana kinasomeka...WAZIRI WA HABARI NA UTALII WA ZANZIBAR afanya KATIKA UWANJA ndege WA KIMATAIFA WA ABEID KARUME. Nimefahamisha kiungwana, mna khiyari kurekebisha au laa!

    Japokuwa msomaji atapitia khabari nzima na kufahamu kilichokusudiwa, lakini kwa mchapishaji/muhariri, huwa haileti maana kuwa na 'speed' without 'accuracy'.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...