Mbunge wa jimbo la Vunjo mkoani Kilimanjaro na Mwenyekiti wa chama cha TLP, Dkt. Augustine Lyatonga Mrema akihutubia katika mkutano wa hadhara jimboni kwake  jana kwa ajili ya kuhamasisha uchaguzi wa serikali za mitaa na pia kuelezea utekelezaji wa miradi ya Maendeleo.

Katika jimbo hilo la Vunjo kumekuwepo na Mvutano mkubwa wa kuliwania katika uchaguzi mkuu wamakani ambapo kwa vyama vya CCM tayari kijana Innocent Shirima ameshatangaza nia kama alivyofanya  Mh. James Mbatia wa NCCR-Mageuzi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. Du! Bonge la umati!

    ReplyDelete
  2. Chezea Mzee wa kilachalacha

    ReplyDelete
  3. Kikao cha wanaukoo nini?

    ReplyDelete
  4. Watu wamejaa mpaka wanakanyagana. Anakubalika sana huyu

    ReplyDelete
  5. Hao inaelekea ni washkaji wake wa siku nyingi sana, ha ha ha ha haaaaa, hayo ndio matunda ya kuwasaliti wanainchi, wenzake wakati wanasusia vikao vya bmk yeye aliwaponda sasa karudi kwa wanainchi hawataki hata kumwona, ukipanda mkaratusi usitaraji kuvuna zabibu, Mzee Lyatonga umechafua hali ya hewa jimbo unalikosa hivi hivi mwakani

    ReplyDelete
  6. Anavuna alichopanda unafiki kwa unafiki uzuri kwa uzuri,ushauri wa bure Mrema rudi CCM huwezi kuhubiri uccm ukiwa upinzani watu weshafunguka macho

    ReplyDelete
  7. Mrema pumzika waachie vijana utaaziriwa

    ReplyDelete
  8. Ila hapo pia kuna SOMO, huenda hao wachache wakawa na maana kuliko umati unaojitokeza kwenye mikutano ya vyama vingine vya upinzani namaanisha hao pengine ndio waliojiandikisha, wanaushawishi kwenye kaya watokazo na wanadi sera wazuri mwisho wapigaji kura, tofauti na wanaojaa kwenye mikutano mingine wao wako kinyume

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...