Na Myovela Mfwaisa TCA.

FILAMU  ya kitanzania ya Dogo Masai iliyotengenezwa na kuongozwa na muongozaji Timoth Conrad ‘Tico’ imeibuka kidedea baada ya kushinda katika tuzo za Silcon Valley African Film Festival (SVAFF) kama Filamu Bora kutengenezwa Afrika (The best African Production Movie ) tuzo hizi zimetolewa California Marekani.

Mtayarishaji wa filamu hiyo Timoth kupitia kampuni yake ya Timamu African Media amesema ushindi huo ni wa Tanzania ndio maana hata kama hakupewa Support na taasisi yoyote kutoka Serikalini lakini amefurahia kulitangaza Taifa kwa juhudi zake binafsi.

“Nimepokelewa hapa California kama mfalme kwa ajili ya kuwania tuzo kubwa na yenye thamani kubwa, hapa nimeongelea fahari ya Taifa langu Tanzania, ni ushindi mkubwa sana nimepeperusha Bendera ya Tanzania,”

“Ninayo furaha kubwa sana kushinda tuzo hii kupitia filamu yangu ya Dogo Masai, tuzo hii kwangu ni ya pili, baada ya tuzo ya Mdundiko kushinda, na tumeona ni bora kutumia gharama kutafuta tuzo kubwa kwetu hatuna tuzo,”anasema Tico.

Filamu ya Dogo Masai imeshinda baada ya kuzibwaga sinema kutoka  South Africa, Malawi, Egypt,  Nigeria, pamoja na Uganda. Ni ushindi wa Afrika Mashariki kwani ilikuwa ni Tanzania na Uganda ndio walifanikiwa kuingia katika tuzo hizo kubwa, bado kuna sababu ya kujivunia kama ushindi wa kishindo.

Changamoto kubwa ni kwa Basata ambao inasemekana wamekuwa wakizuia watayarishaji wasiandae kwa sababu zao ambazo hazijengi tasnia zaidi ya kudumaza, leo mtanzania anakwenda Marekani na kuibuka mshindi akitangaza Bendera ya Tanzania.
Ushindi wa filamu ya Dogo Masai ni ushindi mkubwa kwa Tanzania ni kitu cha kujivuania na iwe njia kwa watayarishaji wengine kushiriki katika tuzo mbalimbali za filamu hata Oscar, huu ni mwanzo mzuri kwa kazi za Tanzania.

Tico anawashukru wasanii wote walishiriki na kufanikisha utengenezaji wa filamu ya Dogo Masai, familia yake rafiki yake Dorice, timu nzima ya Timamu Casting Agency na kila mtu aliyeshiriki kwa mawazo na ushauri na anasema kuwa milango imefunguka kwani filamu yaDogo Masai imeingia katika kugombea tuzo nyingi.

Dogo Masai pia  imechaguliwa kuingia kwenye tuzo nyingine ya Rome Independent Film Festival (RIFF) za nchini Italy, na tayari kuna dalali za kuibuka na ushindi kwani watengenezaji wa filamu wamekuwa wakiiongelea katika mitandao mbalimbali, tuzo hizo zinatarajiwa kufanyika mwakani mwezi wan ne Dogo Masai ni balozi kuitangaza Tanzania.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Basata ndio wanaouwa sanaa ya tanzania sababu si wabunifu wamekaa tu maofisini kupokea mshahara wa bule bila kufanya kazi ya kuinua sanaa yetu

    ReplyDelete
  2. WOW, THAT IS BEAUTIFUL, I LOVE THIS GUY.

    ReplyDelete
  3. Hongera sana Mungu akubariki kwa kuitangaza Tanzania yetu. Siyo Tanzania hatuna wabunifu tunao sana na wengi bali tunawakatisha tamaa wakati wanapojitoa kwa hali na mali. sasa kitu kama hiki Basata mnajisikiaje? sisi watanzania tumefurahi sana na itabidi wakati mwingine mgharamie ya msupport

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...