Na Woinde Shizza,Arusha.
Kiongozi wa matukio ya ulipuaji wa mabomu na umwagiaji tindikali viongozi wa dini aliyejulikana kwa jina la Yahaya Hassani Omary ameuwawa na jeshi la polisi wakati alivyokuwa akijaribu kukimbia.
Akithitisha kutokea kwa tukio hilo Kamanda wa Polisi mkoani Arusha,SACP Liberatus Sabas (pichani) Alisema kuwa tukio hilo limetokea October 19 majira ya saa tano na nusu katika barabara ya babati mkoani Arusha wakati alipokuwa akijaribu kuwakimbia polisi.
Alisema kuwa mtuhumiwa huyo wa ugaidi alishikiliwa wiki mbili zilizopita huko mkoani Morogoro mara baada ya kutafutwa kwa muda mrefu na hapo jana alikuwa akipelekwa wilayani kondoa mkoani Dodoma kwa ajili ya kwenda kuonyesha sehemu ambazo alikuwa ameficha mabomu mengine.
"mtuhumiwa huyo alikuwa anasakwa kwa muda mrefu bila mafanikio kwani alikuwa hakai sehemu moja ila jeshi la polisi huko mkoani morogoro lilimkamata wiki mbili zilizopita na baada ya kufanyiwa mahojiano alisema ameficha mabomu mengine huko kondoa na jana alikuwa akipelekwa kuonyesha ndipo alipotumia trikizake ambazo amefundishwa za ugaidi kwa kupiga judo na kutaka kuwakimbia askari ndipo akapigwa risasi mbili"alisema Sabas
Alitoa wito kwa wananchi kuendelea kuwafichua waovu ili kuwaza kuteketeza matukio ya uhalifu.
Alikua analipwa mshahara na nani huyo gaidi. ?
ReplyDeleteMtuhumiwa alikuwa anasafirishwa kwenye mkokoteni mpaka akaruka na kuanza kukimbia? Je, hakufungwa pingu ndg. Kamanda? Just curious.
ReplyDeleteJamani ni hakika ni yeye?! Je alishataja wengine?
ReplyDeleteHii ni kama execution ya kukusudia. Huyo ni mshukiwa tu na hajakutwa na hatia na mahakama yeyote. Kumuua mshukiwa asiyekuwa na silaha ni kosa kubwa sana. Hata kama ametaka kukiumbia. Maswali polisi wanatakiwa kujibu ni kuwa; Je mshukiwa wa kosa kubwa kama hilo la ugaidi akasafirishwe bila pingu miguuni au mikononi kiasi kwamba ameweza kuwapiga polisi judo? Sio amepewa mwanya akimbie ili apigwe risasi afe. Human Rights Group fanyeni Uchunguzi huru. Alexbura Dar
ReplyDeleteUna upeo mkubwa sana mkuu. Ndo tanzania yetu hii
Deletewell done!!
ReplyDeletewell done police tz hayo ndio maneno tunataka kuyasikia, watu kama hawa hawatakiwi kwenye jamii yetu, maliza wote kuwe na amani
ReplyDeleteSiasa tupu!
ReplyDeleteWhat are the use of electroshock weapons?
ReplyDeleteSawa
ReplyDeleteAisee tuko nyuma sana kwenye maswala ya law enforcement handling.
ReplyDeleteGod help us