Mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom kuwania ubingwa wa Tanzania Bara kati ya Yanga na Simba iliyochezwa  (Oktoba 18 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam imeingiza sh. 427,271,000.

Washabiki 49,542 walikata tiketi kushuhudia mechi hiyo ambapo viingilio vilikuwa sh. 7,000, sh. 10,000, sh. 20,000 na sh. 30,000. Asilimia 18 ya Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) iliyolipwa ni sh. 65,176,932 wakati asilimia 5 ya gharama ya tiketi kwa CRDB ni sh. 21,363,550.

Kwa upande wa Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) ambayo ni sh. 1,000 kwa kila tiketi, timu mwenyeji Yanga imepata sh. 17,339,700, Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 7,431,300 na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) sh. 24,771,000.

Mgawo mwingine wa mapato hayo ni Uwanja sh. 43,678,277.67, gharama za mchezo sh. 24,751,024.01, Bodi ya Ligi sh. 23,295,081.42, TFF sh. 17,471,311.07, DRFA sh. 10,191,598.12, timu mwenyeji Yanga sh. 100,460,038.64 na timu ngeni Simba sh. 71,341,186.86.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Kwa hali hii vilabu lazima viendelee kuumia, Makato ni makubwa mno. Pesa iliyolipwa kwa vilabu vyote viwili ni chini ya 50%!!

    ReplyDelete
  2. Stupid mind,too much deductions

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...