Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea, Mathias
Chikawe (kushoto) akimkabidhi Kapteni wa Timu ya Mpira wa Miguu ya Ubungo Stars ya
Kata ya Namapwia, wilayani Nachingwea, Hassan Abbas zawadi ya mpira wa miguu baada ya
timu hiyo kuongoza Ligi katika Kata hiyo. Timu nne zilishiriki mashindano hayo ya Kata na
kufanikiwa kutengeneza timu moja ambayo itashiriki katika mashindano ya Tarafa ya Ruponda
na baadaye kufika ngazi ya wilaya ambapo mshindi wa wilaya anatarajiwa kupewa zawadi nono
ya Sh 500,000 itakayotolewa na Mbunge wa jimbo hilo. Hata hivyo, Chikawe alitoa jezi seti 170
pamoja na mipira 100 kwa ajili ya timu 170 za mpira wa miguu zilizopo katika jimbo hilo.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea, Mathias
Chikawe (kushoto) akimkabidhi Diwani wa Kata ya Namapwia, wilayani Nachingwea, Sefu
Mwenyewe fedha kwa ajili ya mshindi wa pili pamoja na wasimamizi wa ligi hiyo. Katika
mashindano hayo ya ligi yaliyomalizika hivi karibuni, Timu ya Ubungo Stars iliibuka kidedea
katika kata hiyo na kufanikiwa kupewa zawadi ya mpira wa miguu. Timu nne zilishiriki
mashindano hayo kufanikiwa kutengeneza timu moja ambayo itashiriki katika mashindano ya
Tarafa ya Ruponda na baadaye kufika ngazi ya wilaya ambapo mshindi wa wilaya anatarajiwa
kupewa zawadi nono ya Sh 500,000 itakayotolewa na Mbunge wa jimbo hilo. Hata hivyo,
Chikawe alitoa jezi seti 170 pamoja na mipira 100 kwa ajili ya timu 170 za mpira wa miguu
zilizopo katika jimbo hilo.
Kapteni wa Timu ya Mpira wa Miguu ya Timu ya Ubungo Stars, Kata ya Nawapwia, Hassan
Abbas akimshukuru Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la
Nachingwea, Mathias Chikawe (kushoto) kwa mchango wake mkubwa ambao ameutoa kwa ajili
ya kuzisaidia timu 170 za mpira wilayani Nachingwea na pia kuwawezesha kwa muda mrefu
kushiriki katika michezo ambapo inawasaidia kutokuingia katika matukio ya uhalifu mitaani.
Waziri Chikawe ameanzisha ‘Chikawe CUP’ ambapo kwasasa mashindano hayo yapo katika
ngazi ya Kata mbalimbali ambapo mshindi atapatikana baada ya kufikia ngazi ya wilaya. Timu
ya Ubungo Stars ndio iliongoza katika mashindano ya Kata ya Namapwia baada ya kuzishinda
timu 3 zilizopo katika kata hiyo. Hata hivyo, Chikawe alitoa jezi seti 170 pamoja na mipira 100
kwa ajili ya timu 170 za mpira wa miguu zilizopo katika jimbo hilo.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea, Mathias
Chikawe (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na wachezaji wa timu ya Ubungo Stars ya Kata
ya Namapwia wilayani Nachingwea baada ya timu hiyo kuwa mshindi wa kwanza baada ya
kuzishinda timu tatu zilizopo katika kata hiyo. Waziri Chikawe aliipa zawadi ya mpira timu hiyo
na kuwashauri wazidi kusongo mbele ili timu hiyo ifike hatua ya Wilaya ili wapewe zawadi ya
Sh500,000 kwa timu itakayonyakua kombe hilo. Hata hivyo, Waziri Chikawe alitoa jezi seti 170
pamoja na mipira 100 kwa ajili ya timu 170 za mpira wa miguu zilizopo katika jimbo hilo. Picha
zote na Felix Mwagara.
Mheshimiwa shukran sana. Bado Viatu.
ReplyDelete