Wanachama wa Mtandao wa Habari za Kijamii Tanzania (Mhakita), wakifanya usafi katika Hifadhi ya Taifa ya Mikumi, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya tamasha la Ujirani Mwema, wilayani Kilosa mkoani Morogoro, hivi juzi. Picha na Mpigapicha Wetu.

KIASI cha sh milioni 25 hutumika kila mwaka katika hifadhi ya Taifa ya Mikumi iliYopo wilayani Kilosa mkoani Morogoro kwa ajili ya shughuli za usafi wa mazingira na kuhudumia wanyama wanaogongwa katika barabara kuu iendayo Iringa na Morogoro inayopita katika hifadhi hiyo. 

 Kaimu mkuu wa hifadhi hiyo Dattomax Selanyika ,alisema hayo jana wakati akizungumza na waandishi habari waliotembelea katika hifadhi hiyo na kupata fulsa ya kufanya usafi wa mazingira kwa lengo la kupinga masuala ya ujangili kupitia mtandao wa habari za kijamii Tanzania MHAKITA.

 Alisema kati ya fedha hizo milioni 12.5 hutumika kwaajili ya uokotaji wa takataka zinazotupwa na wasafiri wanaotumia barabara hiyo. ‘’ Usafi huo hufanywa na vibarua kuanzia eneo la Doma hadi Mikumi umbali wa kilomita 50, na shughuli hiyo hufanywa mara tatu kwa wiki’’ alisema Selanyika.

 Aidha alisema katika maeneo yaliowekwa matuta ili magari yaweze kupunguza mwendo kutokana na kuwa ni vivuko vya wanyama pamegeuzwa ndio sehemu ya kutupa takataka kwa wasafiri hao. Alisema utupaji wa takataka katika hifadhi hiyo una madhara makubwa kwa wanyama kwani baadhi ya takataka husababisha wanyama kupoteza maisha wakizila. 

 Hata hivyo alisema kumekuwa na tabia ya baadhi ya madereva kwenda mwenzo kasi katika hifadhi, hiyo kinyume na sheria na kwamba kusababisha kuwagonga wanyama. Kwa upande wake mkuu wa idara ya ikologia wa hifadhi hiyo Crispin mwinuka alisema idadi ya wanyama wanaogongwa katika hifadhi hiyo wamekuwa wakiongezeka mwaka hadi mwaka ambapo katika kipindi cha miaka 2009 hadi 2013 jumla ya wanyama 604 waligongwa katika barabara hiyo na kupoteza maisha.

 Alisema mwaka 2012 wanyama waliogongwa walikuwa 111 huku mwaka 2014 walikuwa 132. Pia alisema katika kipindi hicho hicho jumla ya kilogramu 21,907.80 zilitupwa katika hifadhi hiyo na kusababisha hifadhi hiyo kuingia hasara kubwa katika kuokota taka hizo. Aliwataka wasafiri wanaotumia barabara hiyo kujenga tabia ya kuweka vifaa vya kuhifadhia takataka katika vyombo vya usafiri ili kuepusha tatizo hilo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...