Right is Nahid Hirji, Facebook Head of Growth and Partnerships; David Zacharia, Tigo Head of Data and Devices and Miss Iku Lazaro, Shule Direct Communications Director.
 Kwa mara ya kwanza, wanafunzi Tanzania wanaweza kujipatia nyenzo za kujifunzia masomo ya sekondari bila gharama yoyote kupitia mpango wa Facebook wa Internet.org.

Mfumo wa masomo ya digitali wa Shule Direct ni mpango wa kwanza wa aina yake Tanzania, mfumo huu unawapatia wanafunzi na walimu nyenzo za masomo zenye ubora wa hali ya juu zilizotengenezwa kufuata mfumo wa elimu ya Sekondari ya Tanzania.
 
Watengenezaji wa nyenzo zinazopatikana Shule Direct ni mabingwa katika fani ya elimu, hii inahakikisha kuwa nyenzo zipatikanazo Shule Direct ni sahihi, zinapitiwa na kuhakikiwa mara kwa mara kwa ajili ya maboresho, hivyo zina ubora wa hali ya juu.

Mfumo wa masomo wa kidigitali wa Shule Direct unampa mwanafunzi uhuru wa kujisomea, kujadiliana na kubadilishana mawazo na wanafunzi wenzake wakati wowote na mahali popote.

Kupitia Shule Direct wanafunzi wanaweza kujisomea matini (“notes”), kujibu maswali ya majaribio, pia wanaweza kushiriki mijadala mbali mbali na wanafunzi wenzao na walimu. Mijadala hii inasimamiwa na msimamizi kutoka Shule Direct kuhakiki matumizi salama ya mtandao wa Intaneti na kuwa haki za wanafunzi na watu chini ya umri wa miaka 18 zinahifadhiwa.

Ushirikiano wa Shule Direct na Internet.org ni hatua madhubuti katika kuhakikisha teknolojia iliyopo inatumika kuboresha elimu Tanzania. Ushirikiano huu umekuja wakati muafaka, na ni faida kubwa kwa Shule Direct kwa vile kwa mpango huu nyenzo zetu sasa zitawafikia wanafunzi wengi zaidi.

Internet.org ni mpango wa Facebook ambao unalenga kuwezesha watu wengi zaidi ambao hawana namba ya kuunganishwa na Intaneti, kuweza kupata namna ya kutumia Intaneti, na kujipatia huduma mbali mbali muhimi k.v. tovutu ya Shule Direct na nyinginezo nyingi zipatikanazo kupitia Intaneti.

Mpango huu wa Internet.org unapatikana kwa watumiaji wa mtandao wa Tigo kwa sasa.


Jifunze. Jadiliana. Wakati wowote. Mahali Popote.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...