Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na kupiga picha ya pamoja na na viongozi wa Bendi ya Msondo ngoma Ikulu jijini Dar es Salaam leo mchana.Viongozi hao walimtembelea Rais Kikwete  kufanya naye mazungumzo kuhusu masuala mbalimbali ya tasnia ya muziki nchini. Bendi hiyo kongwe imetimiza miaka 50 mwezi huu. Picha na Freddy Maro

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Hongera!

    lakini siku hizi mmeishiwa "gas ya kupiga genre ya mziki wenu na kucheza dansi.

    Tumieni umahiri wenu kwa kubadili genre; badilsheni nyimbo zenu ziingie kwenye genre ya jazz!

    Mtawza kushindana vizuri na wazee wenzenu wa Jazz: cape Town Jazz Festival; Brazil Jazz, Ottawa Jazz, na jazz nyinginezo!

    Mmenisikia na kunisoma vizuri?

    ReplyDelete
  2. hawa ndiyo watu wanaopiga muziki asili wa Tanzania na ulioenda shule si hawa waigaji wa kwaito na kujiita wanamuziki kwa kupiga muziki wa computer. Muziki wa bendi ndiyo muziki wetu Tanzania hii mingine ya wauza unga ni magirini tu na ndiyo maana haina radha. Bigup Msondo na bendi zote za Tanzania.

    ReplyDelete
  3. Msondo Ngoma Band vipi kufanya video ya muziki wa dansi, maana nyie ni mojawapo za bendi kongwe ktk bara la Afrika, lakini sioni video yoyote iliyoandaliwa vyema na kutundikwa YOUTUBE.

    Ankali, washika-dau na ma-sponsor hasa wale wa 'Konyagi'' huu ndiyo muda muafaka kushikana mikono na kuandaa video kali na yenye quality kuanzia mazingira-back-ground, sound quality na muonekano wa video-HD.

    Kwa namna hiyo sote tutafaidika ikiwa mapsonsor, wadau wa muziki wa dansi tukiamua kufanya kweli kuiweka bendi yeti kongwe kwenye ramani ya dunia kupitia YOUTUBE.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...