Katika kuhakikisha wakazi wa Temeke na Ilala wanapata huduma kwa karibu,Kampuni ya mawasiliano ya Vodacom leo imefungua duka jipya katika jengo la Quality Centre Uchumi  lililopo katika barabara ya Nyerere ambalo ni moja ya kituo kikubwa cha biashara jijini Dar es Salaam likiwa na maduka makubwa,ukumbi wa sinema,sehemu za burudani na maofisi.

Duka hili jipya lenye mazingira rafiki kwa wateja litakuwa linatoa huduma mbalimbali kwa wateja wa Vodacom ikiwemo huduma  kwa mawakala wa Mpesa na uuzaji wa bidhaa  za Vodacom na litawawezesha wateja wa  barabara ya Nyerere,Keko,Ilala,Chang’ombe na Temeke kupata huduma kwa karibu.

Ofisa Mkuu wa Idara ya Uuzaji na usambazaji  wa Vodacom Tanzania Hassan Saleh, alisema ufunguzi wa duka hili la kisasa  ni mwendelezo wa malengo ya Vodacom kuendeleza  kuboresha maisha morani kwa kila mtanzania kwa kupata huduma za kampuni hiyo zenye ubora na kuwafikia wateja kwa urahisi zaidi popote pale walipo.

“Uzoefu na utafiti umetuonyesha kuwa wananchi wanataka ubora,kama mtandao unaoongoza nchini tumejizatiti kuhakikisha tunafanya ubunifu wa hali ya juu wa kiteknolojia ili kutumia mtandao wa simu kuboresha maisha ya wananchi ikiwemo kutoa huduma bora na ndio maana tunazidi kufungua maduka kama haya kwa ajili ya kuwasogezea karibu wananchi huduma bora,na ninawahakikishia kuwa popote wateja wetu walipo tutawafikia”Anasema Saleh.

Naye Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala,Jerry Silaa,aliipongeza Vodacom kwa kufungua duka katika eneo hilo lenye wananchi wengi na kuongeza kuwa anaamini litawaokolea muda waliokuwa wanatumia kufuata huduma za Vodacom mbali na kuwasihi kutumia huduma ya M Pesa kwani ni huduma iliyo bora na yenye usalama zaidi.

Vodacom ina mtandao wa maduka  82 na wakala mbalimbali wakuuza bidhaa zake nchini na  duka lililofunguliwa leo ni la sita kufunguliwa katika wilaya ya Temeke.Hivi karibuni inatarajia kufungua maduka katika maeneo ya Mbagala,Buguruni,Sea Cliff na Bagamoyo.
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala,Jerry Silaa wa kwanza toka kulia pamoja na Meneja wa duka hilo Irene Njovu na Ofisa Mkuu wa Mauzo na Usambazaji wa Vodacom Tanzania Hassan Saleh wakikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa duka jipya na la kisasa la Vodacom Tanzania,lililopo Quality Centre katika barabara ya Nyerere ambalo ni moja ya kituo kikubwa cha biashara jijini Dar es Salaam.
Mwandishi wa habari wa Gazeti la Majira Rayusa Yassini aliefika katika uzinduzi wa duka jipya na la kisasa la Vodacom lililopo Quality Centre katika barabara ya Nyerere jijini Dar es Salaam.Akimiminiwa kinywa cha mvinyo na Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala,Jerry Silaa(kushoto)ikiwa ni moja ya ishara ya uzinduzi wa duka hilo.Wanaoshuhudia wa pili toka kushoto ni Meneja wa duka hilo Irene Njovu na kulia ni Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania,Rosalynn Mworia.
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala,Jerry Silaa(kushoto)na Mwandishi wa habari wa Gazeti la Majira Rayusa Yassini aliefika katika uzinduzi wa duka jipya la kisasa la Vodacom lililopo Quality Centre katika barabara ya Nyerere jijini Dar es Salaam wakigonganisha glasi zenye mvinyo ikiwa ni ishara ya uzinduzi wa duka hilo. Wanaoshuhudia wa pili toka kushoto ni Meneja wa duka hilo Irene Njovu na kulia ni Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania,Rosalynn Mworia.
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala,Jerry Silaa(katika) akiangalia moja ya Simu zinazouzwa katika duka jipya la na la kisasa la Vodacom lililopo Quality Centre katika barabara ya Nyerere jijini Dar es Salaam,mara baada ya kuzindua rasmi duka hilo kushoto ni Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania,Rosalynn Mworia na kushoto kwa Meya ni Ofisa Mkuu wa Idara ya Uuzaji na Usambazaji wa Vodacom Hassan Saleh na kulia ni Mkuu wa Idara ya Uuzaji na usambazaji bidhaa wa kampuni hiyo Upendo Richard.
Baadhi ya waandishi na wafanyakazi wa Vodacom Tanzania wakiwa katika uzinduzi wa duka la Vodacom Tanzania, lililopo Quality Centre katika barabara ya Nyerere jijini Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...