Mgeni Rasmi Waziri wa Maendeleao ya Mifugo na Uvuvi Mhe. Dkt. Titus Mlengeya Kamani (MB) akikata utepe kuashiria Uzinduzi wa Mradi wa Ufugaji wa Samaki ndani ya Ziwa Viktoria Kiteule cha Bulamba kwa kutumia teknolojia mpya ya vizimba (Cages). Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Tarime Mhe.John Henjewele, Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mara. Kulia ni Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Meja Jenerali Raphael M. Muhuga.
Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Mhe. Dkt. Titus Mlengeya Kamani akipandikiza vifaranga vya samaki ndani ya Ziwa Victoria, mradi unaotekelezwa na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Wilaya ya Bunda, Kiteule cha Bulamba kwa kutumia teknolojia mpya hapa nchini ya kuzalisha samaki kwenye vizimba.
Picha ya vizimba ambavyo ufugaji wa samaki umeanza mara baada ya Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi kuzindua mradi huo na kupandikiza vifaranga vya samaki. Mradi unatekeleza na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Wilaya ya Bunda, Kiteule cha Bulamba kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wakiwemo Economic Social Research Foundation (ESRF), Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) na Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango. Ufugaji wa samaki kwa kutumia teknolojia ya vizimba ndani ya Ziwa Victoria, umekuwa ukitekelezwa pia na wenzetu wa Kenya na Uganda ambao wamepiga hatua kubwa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Tutawezaje kupata mawasiliano ili kwa lengo la taarifa zaidi juu ya uwekezaji wa ufugaji kwa vizimba?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...