Picture1-swahili
Hospitali ya Apollo iliyoko nchini India imefanikiwa kuwatenganisha mapacha wa kike wa Tanzania Abriana na Adriana waliokuwa wameunganika chini ya kifua na tumboni  katika upasuaji uliofanyika tarehe 17 Novemba 2014 nchini humo. Mapacha waliounganika kwa mtindo huu hujulikana kwa watalaam kama Thoraco Omphalopahus na upasuaji uliofanyika na hospitali Apollo ulikuwa wenye mafanikio na wa aina yake.
Mapacha Abriana na Adriana awali ya upasuaji huo walikuwa wameunganika kuanzia chini ya kifua na tumbo, hali kadhalika walikuwa wakitumia mvungu mmoja wa moyo na maini yaliyounganika.  Changamoto ya upasuaji wa mapacha hawa kwa madaktari ulikuwa  utenganishaji bila kuwavujisha damu nyingi ambayo waliweza kukabiliana nayo ipasavyo.
Upasuaji huo ulifanywa na jopo la watalaamu 50 waliobobea katika taaluma mbali mbali za tiba ya afya ya kabla na baada ya upasuaji ambao uliendelea kwa masaa 11.  Watalaamu walifanikiwa kutenganisha viungo vilivyokuwa vimeungana. Mapacha hawa walipona na kupata ahueni kwa haraka hivo kusaidia zoezi zima la uponyaji baada ya upasuaji.
Picture2-swahili
Hali kadhalika, hatua nyingine ya muhimu katika upasuaji huo ilikuwa kurudisha viungo husika mahala pake baada ya kuvitenganisha. Akizungumzia kuhusu hili Dkt. K S Sivakumar Plastic & Reconstructive Surgeon anasema, “Baada ya upasuaji, moyo wa moja ya mapacha ulitakiwa kurudishiwa mahali pake ili kuzuia mbenuko na uharibifu pamoja na maini yaliyokuwa yameungana. Ilichukua majopo mawili ya wataalum kwa masaa nne kukamilisha ufungaji wa maini, moyo, na utumbo katika mahala pake.”

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Tumshukuru Mwenyenzi Mungu kwa uweza wake mkuu -
    Tuwashukuru Madaktari pia kwa Kazi ngumu lakini yenye mafanikio. Tuwaombee Kila la kheri na Baraka za Mwenyenzi Mungu katika kila jema walifanyalo na hasa katika kuokoa maisha ya wanaadamu Wenzao.
    Hizi ni habari nzuri sana kaka Michuzi Asante kutufikishia!
    Tuwaomee wazazi na watoto afya njema.

    ReplyDelete
  2. Mungu awape maisha marefu...

    ReplyDelete
  3. Nasisi tujitahidi ili tufike hapo sio Kila kitu nnje ya nchi... kwa nini tushindwe???????
    Ni aibu kwa mwafrica Kila kitu ulaya au India..

    RasVin,,
    Germany

    ReplyDelete
  4. MCHANGO MKUBWA SAANA WA MADAKTARI KATIKA KUOKOA NA KUWEZESHA MAISHA YA WANADAMU WENZAO.MUNGU AWABARIKI SANA.MCHANGO HUU ULIO NA MAJITOLEO MAKUBWA YAPITAYO KIPIMO CHA MALIPO NI THAWABU WANAYIPATA KWA MOLA.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...