Na Woinde shizza, Arusha 
 Hakimu David Mwita wa Mahakama ya mwanzo ya Maji ya Chai mkoani Arusha ameahirisha hadi  Desemba 24, 2014  kesi inayomkabili Mbunge wa Jimbo la Arumeru  Mashariki Mh. Joshua Nassari (pichani), kwa tuhuma za kuharibu mali ya umma  yenye dhamani ya shilingi laki mbili, pamoja na kumteka mtu na kumtishia kwa bunduki tukio ambalo anatuhumiwa kufanya Desemba 15, mwaka huu 
Mahakama hiyo imemuachia Mbunge huyo baada ya kutimiza masharti ya dhamana,  ikiwa ni wadhamini watatu ambao wana mali zisizohamishika zenye thamani ya shilingi milioni moja na nusu kila mmoja. 
 Akiongea mara baada ya kuairisha kesi hiyo wakili wa mbunge huyo wa Arumeru mashariki Bw. James Ole Milya alisema kuwa amesikitishwa sana na tukio la mahakama hiyo kumpa mashariti makubwa mteja wake kwani kesi yake ilikuwa haihitaji mashariti makubwa hivyo . 
 Aidha alisema kuwa mbali na kupewa mashariti hayo angependa kesi hiyo ipelekwe katika mahakama ya wilaya ili yeye kama wakili wa mbunge huyo aweze kumtetea kwani katika mahakama ya mwanzo hairuhusu kuweka wakili. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...