Iringa. Timu ya soka ya waandishi wa habari za michezo nchini, Taswa FC imetinga kwa vishindo michuano ya soka ya Asas Dairies Limited inayoendelea mkoani Iringa baada ya kushinda mechi zake zote za hatua ya makundi. 
Taswa FC ilichezo mechi yake ya kwanza dhidi ya Mkwawa Senior na kuicharaza kwa mabao 5-0 katika mchezo wa kundi A. Mchezo huo uliochezwa kwenye uwanja wa Samora, ulikuwa mkali na wa kusisimua na Taswa FC ilifunga mabao yake kupitia kwa Zahoro Mlanzi aliyefunga mabao matatu kutokana na pasi safi kutoka kwa Muhidin Sufiani, Ibrahim “Maestro”Masoud na Edo Kumwembe. 
Mabao mengine ya Taswa yalifungwa na Ali Mkongwe baada ya pasi safi ya Mohamed Akida na Nico Ndifwa baada ya pasi ndefu ya Elius Kambili. Mkwawa Senior ilishinda kuipita ngome ya Taswa FC chini ya Wilbert Molandi, Athuman Jabir na Mbozi Katala. 
Katika mchezo wa pili, Taswa FC iliifunga Pawaga mabao 3-0 yaliyofungwa na Saidi Seif, Nico Ndifwa na Athuman Jabir. Katika mchezo wa kundi B, Iringa Veteran ilifunga Mkwawa Junior mabao 6-1 yaliyofungwa na Lisa Mwalupindi aliyefunga mabao matatu, Mzee Mbata na Haji Mambo. 
Mwenyekiti wa Taswa FC, Majuto Omary aliipongeza timu yake kwa ushindi huo ten bila kufungwa na kuahidi kutwaa ubingwa huo. Kutokana na matokeo hayo, Taswa itacheza na Mkwawa Junior katika nusu fainali ya kwanza iliyopangwa kuanza saa 2.00 asubuhi kwenye uwanja huo huo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...