Meneja Mauzo wa Taasisi ya Kifedha ya Bayport Financial Services Kanda ya Ziwa, Lugaano Kasambala, akimpa pole Ester Jonas, mama wa Yohana Bahati, mtoto mwenye ulemavu wa ngozi albino, aliuawa mkoani Mwanza, hivi karibuni. Mama huyo anatibiwa katika Hospitali ya Bugando baada ya kupata mareraha katika tukio la kuvamiwa na kuporwa mtoto wake. Kulia kwa Kasambala ni Mbunge wa Viti Maalum, Al Shaimar Kweigyir mwenye miwani waliyeambatana katika safari hiyo kwa ajili ya kuwapa pole na kuwafariji.

Na Mwandishi Wetu, Mwanza
MBUNGE wa Viti Maalum, Al Shaimar Kweigyir kwa ushirikiano na Taasisi ya Kifedha, inayojihusisha na mikopo ya Bayport Financial Services yenye Makao yake Makuu jijini Dar es Salaam, Tanzania, walifanya ziara ya siku mbili jijini Mwanza kwa ajili ya kutembelea familia mbili zilizopoteza watoto wao wawili ambao ni walemavu wa ngozi.

Familia hizo ni ya Ester Jonas, mama wa marehemu Yohana Bahati na ile ya Sofia Juma mama wa mtoto Pendo Emmanuel, wote wakiwa ni watu wenye ulemavu wa ngozi, huku familia zote mbili zikipewa Sh Milioni 2 kila moja.
Mbunge wa Viti Maalum, Al Shaimar Kweigyir mwenye miwani akimfariji mama wa Yohana Bahati (Ester Jonas) aliyelazwa Hospitali ya Bugando, Mwanza, pamoja na kumpaa mafuta ya kupaka kwa ajili ya watoto wake wawili ambao nao ni albino,. Kushoto kwa Mh Shaimar ni Meneja Mauzo wa Bayport Financial Services Kanda ya Ziwa, Lugano Kasambala na wafanyakazi wengine wa Bayport waliombatana pamoja kwenye msafara huo wa kutoa pole.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Jamani mimi nawapongeza sana kwa kuwafariji wafiwa na majeruhi wa tukio hili la kuuawa kwa albino. Lakini kuliko kuwapa pesa watafutiwe mahali pazuri penye ulinzi na usalama wajengewe nyumba na kupewa mitaji. Kuwapa pesa wataendelea kuishi mazingira hatarishi na kuendelea kupoteza familia zao kila kukicha. Serikali ijaribu kuwahamisha hao watu. Kama serikali imeshindwa kuna mashirika mbalimbali, makanisa mbalimbali tuungane sote kwa pamoja hata ikiwezekana tuombe misaada nje ili kuwanusuru hawa watu. Watoke mashambani huko waje mijini kwenye usalama zaidi. Lo! inauma sana

    ReplyDelete
  2. Taifa letu limejaa udhaifu raia wake wanauliwa kama kuku hakuna usalama kwa raia wote hasa wenye ulemavu huu wa ngozi ndio imekuwa kawaida serekali imeshindwa kuwapa ulinzi huu ndio ukweli na ni aibu hivi sasa yuna eleweka au kusifika dunia nzima kwa kuuwa maalbino magazeti yote makubwa ya duniani na mitandao hiyo ndio habari kwa sasa serekali wako bize na uchaguzi nafikiri.

    asante
    mdau
    kilioni.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...