Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 28 mpaka sasa

  1. Acha kuua na kukata mikono ya albino!.

    ReplyDelete
  2. Hate people who killings innocent

    ReplyDelete
  3. Kengereza si hamkitaki jamani, sasa na hapa mnawandikia kwa kingereza wataelewa? wandikieni hicho kiswahili. labda ndio wataelewa

    ReplyDelete
  4. it is true, stop, stop, stop, killing our beloved once.God is watching you stop it.

    ReplyDelete
  5. Ujumbe huo uandikwe kwa kiswahili ndiyo utawafikia walengwa ambao wengi hawajuwi ua hawafahamu hayo yaliyoandikwa.

    ReplyDelete
  6. Mtoto mzuri Maashallah!

    Na tunamuombea Mola ampe maisha marefu yeye na wenzake.

    Ni ukatili usio na kifani hayo wanayofanya hao wapenda utajiri wa kijinga.

    Mwenyezi Mungu atawalaani na kuwaadhibu hapa hapa duniani.

    Tuungane sote kupinga ukatili huu.

    ReplyDelete
  7. MTOTO MZURI HUYO.

    ReplyDelete
  8. Ni kweli kabisa, itumike lgha yetu ili woote waelewe maana sasa, tumeamua kuwalinda hawa ndugu zetu.

    ReplyDelete
  9. So cute, bless her

    ReplyDelete
  10. Tatitizo letu kubwa ni kuogopa Ukweli! Naona wengi hapa wanaogopa aibu hii ya kitaifa ya kuua watu wenye ugonjwa wa ngozi; Wantanzania tumezama sana katika ushebnzi wa kuamini uchawi! Hata wanaosema wamesoma au ni waamini wa madhehebu mbali mbali wengi bado wapo kwenye tamaduzi hizi za kishenzi: Makanisa, Misikiti na nyumaba za waganga wote wananufaika kwa mradi huu wa kishezi, yaani "uchawi". Makanisa na Misikiti wanahubiri zaidi juua ya kinga za Uchawi zaidi ya Neno la Quran Tukufu au Biblia takatifu. Tuanchane na Ushenzi. Tujiakwamue kwa kutoa Elimu mpya kwa watoto wetu.: Maana vijana wa leo na vizee vya juzi vyote vimezama kwenye Uchawi. Nyumba za watawa, Misikiti wote wamo humo kwenye ndimbwi la kuamini uchawi!

    ReplyDelete
  11. Its not Fair, Albino are not meant to spent the rest of their lives worrying or come up with a rescue plan to protect themselves. Their Meant to be productive in the society and pursue their goals and ambitions just like any other human being.

    ReplyDelete
  12. Sasa hivi ukiandika Albino kwenye mtandao jina Tanzania linaibuka aibu aibu aibu

    ReplyDelete
  13. SIWAUWE 'ALBINO' (Sisitozo)

    Natiririkwa machozi, naishiwa na maneno.
    Kisa rangizo za ngozi, kama wazungu mfano,
    Hadharani wazi wazi, mwawacharanga mikono,
    La wote hili jukumu, siwauwe 'ALBINO'.

    Imani zilowatoka, mwawawinda kwa mapanga,
    Viungo vyao mwataka, kuvitolea muhanga,
    Yenu taka kunyooka, acheni huo ni 'wanga'
    La wote hili jukumu, siwauwe 'ALBINO'.

    Siwauwe 'Albino', ulemavu si ugonjwa,
    Si miguu si mikono, wala ngozi sijechanjwa,
    Tuwaenzi kwa mifano, kwa uzima na ugonjwa,
    La wote hili jukumu, siwauwe 'ALBINO'.

    'Albino' tuwalinde, nao pia binadamu,
    Huria nao warande, chochote siwahujumu,
    Tuwe nao tuwapende, sote wana wa 'Adamu'
    La wote hili jukumu, siwauwe 'ALBINO'.

    Wenye imani potofu, mbali mzitokomeze,
    Kutaka umaarufu, wao muwateketeze,
    'Ilahi' hamumukhofu, kesho nini mmweleze?
    La wote hili jukumu, siwauwe 'ALBINO'.

    Acheni nao watambe, fani zote wapendeze,
    Wenye vipaji waimbe, ma 'modo' wajitokeze,
    "Msimu' kura waombe, na mote wajitokeze,
    La wote hili jukumu, siwauwe 'ALBINO'.

    Saba beti zinatosha, natowa msisitizo,
    Wahukumiwe maisha, wenye haka ka mchezo,
    Na adhabu zinotisha, hadi fika wafe nazo,
    La wote hili jukumu, siwauwe 'ALBINO'.

    HK






    ReplyDelete
  14. SWALI MOJA TU JANANI ..je Serikali hasa wizara ya afya mlishawahi kufikiria juu ya kupunguza au hata kufutilia mbali kodi kwenye lotion na mafuta ya kupunguza miale ya jua inayowatesa hawa watanzania?Kwa taarifa yenu nivea kutoka ujeruman yenye uwezo wa kupunguza makali ya miali ya jua kwenye ngozi kikopo kimoja si chini ya 60000 Tshs jamani hebu angalieni hili kwa umakini.

    ReplyDelete
  15. Something should be done lazima Rais sasa hawa watu wanaofanya wenzao biashara tena Kwa kuwaua wanyongwe haraka iwezekanavyo. No excuse.

    ReplyDelete
  16. kachuna jamani kazuri katoto...mungu awalinde

    ReplyDelete
  17. Watu wanafanya kampeni dhibi ya mauaji ya binadamu wenzetu, wengine wamekuja hapa na kampeni dhidi ya lugha. Suala hili linatakiwa kulaaniwa kwa lugha, kabila, dini, rangi zote bila ubaguzi, ili mradi mwishowe watato wetu waishi bila hofu

    ReplyDelete
  18. Tafadhali serikali kuu hiingilie kati hili tatizo ikiwezekana lipelekwe jeshi la ulizi kabisa kwenye maeneo ambayo yamekua sugu. Hawa ni binadamu kama sisi wengine kwa nini wauawe kwa sababu ya ngozi yao. Atakayekamatwa anywenge ili iwe fundisho kwa wengine wenye mawazo potofu kama hayo.

    ReplyDelete
  19. Nadhani imefika wakati Tanzania tuamue rasmi kuweka sheria ya kunyonga hadi kufa mtu yeyote atakayethibitika kuhusika na mauaji ya mlemavu wa ngozi.Hii iwahusu pia wanunuzi wa viungo vya binadamu.Vilevile iwe marufuku kupiga ramli,uganga wakienyeji,pamoja na watu kujiita madokta au maprofesa bila kusomea au kutunukiwa rasmi.China iliamua kuweka sheria kali za kunyonga,mbona ni marafiki zetu wa damu?KIGUGUMIZI KINATOKA WAPI?

    ReplyDelete
  20. Machozi yananitoka kila siku nikiona hizi taarifa, I wish kama ningekua milionea ningewajengea sehemu maalum na ulinzi wao, but why not tz government ?

    ReplyDelete
  21. Yaani, inasikitisha sana. Ila Mungu ni mkubwa sana, sala za watu na machozi yetu hayaendi bure, Mungu ataonesha haki yake. Tuzidi kuwaombea ndugu zetu kwani nao hawakupenda kuwa hivyo walivyo.

    ReplyDelete
  22. Mnapiga kelele bure kiingereza..kiswahili hao waganga wakienyeji lugha zote hizi hawazijui na wala hawana mitandao...mnacho takiwa kufanya nendeni vijijini huko mka toe darasa

    ReplyDelete
    Replies
    1. Mbona unatowa maagizo tu!! Wewe je?

      Delete
  23. Wanunuzi wa viungo vya miili ya hawa albino ni viongozi wenyewe.
    Kwani tujiulize hivi serikali inashindwa kuweka mitego ya kuwakamata hawa wauwaji na wanunuzi kwa ujumla?

    ReplyDelete
  24. Wanaoua hata neno blog hawalijui maana yake!! Let's be more creative in finding better and more effective ways we can influence those that matter na sio wazungu unless ni janja ya kutafuta pesa ya mzungu na uhalali tu kutoka kwao! Just a thought!

    ReplyDelete
  25. Walengwa wa huu ujumbe ni nani???

    ReplyDelete
  26. Mbona BBC waliweza kwenda mpaka huko na kujuwa ukweli na ninani hanahusika na kuonyesha jinsi waganga wanavyousika ktk mahuaji ya ndugu zetu.Lakin serikali himeshindwa kutega mitego na upelelezi kuwabaini hawa wahuwaji wa watoto?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...