Katika Mkutano uliofanyika Nchini India, Mbali na maelezo ya jitihada na dhamira kubwa katika kuwekeza katika maswala ya teknolojia kupitia kampeni yao ya DIGITAL INDIA, Pia nchi imepata kuelezea dhamira yao ya kuwekeza zaidi kwa kutoa misaada ya kimasomo ( Scholarships ) kwa wale watakao kuwa wakisomea masomo yatakayo wezesha kukuza na kufanikisha jitihada zao za Digital India.

Aidha, Kwa Upande mwingine – Wameweza kukubali tatizo linalo ambatana na ukuaji wa technolojia ni uhalifu mtandao huku ikielezwa watumiaji wa simu wamefikia asilimia 97% ya raia wa nchini humo, kitu ambacho kinapelekea matumizi mtandao kuingiwa na dosari ya kipekee.

Itakumbukwa India kupitia taarifa inayosomeka kwa "KUBOFYA HAPA" waziri mkuu wan chi hiyo alihimiza wananchi wake kujikita zaidi katika kutengeneza namna ya kukabiliana na uhalifu mtandao ambapo pia iweze kutumika kutoa misaada kwa nchi nyingine.

Katika Kikao cha siku mbili, Kubwa la kiusalama mtandao ni dhamira kubwa ya moja kati ya washiriki wa mkutano huo kuonyesha dhamira yao kubwa ya kukabiliana na tishio la uhalifu kupitia mitandao ( Hasa Wizi wa fedha kupitia ATM) linalo tikisa mataifa mbali mbali hivi sasa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...