Kiungo mshambuliaji, Haruna Moshi ‘Boban’ na kipa, Juma Kaseja ni kati ya wachezaji watakaoiongoza timu ya Dar City kesho Jumapili Aprili 26,2015 kucheza mechi ya kirafiki dhidi ya Kombaini ya Vikawe iliyopo Mkoani Pwani.

Kwa mujibu wa mratibu wa mchezo huo, Athuman Tippo ‘Zizzou’, mchezo umeandaliwa maalum kwa ajili ya kuhamasisha michezo mkoani Pwani.

Tippo alisema kikosi cha Dar City kitajumuisha pia baadhi ya Waandishi wa Habari za Michezo na kubainisha kuwa mechi hiyo itachezwa kesho Jumapili kuanzia saa 10:00 jioni kwenye Uwanja wa Shule ya Msingi Vikawe uliopo Kibaha, Mkoani Pwani.

“Kikubwa tunataka kuhamasisha michezo huko Vikawe na katika kutimiza hilo, tumepanga kucheza mchezo mmoja wa kirafiki na wakazi wa huko kwa kuwatumia wachezaji, waandishi na watangazaji maarufu nchini,” alisema Tippo.

Kikosi cha Dar City kinaundwa na wachezaji kama Manyika Peter, Juma Kaseja , Athuman Idd "Chuji" , Haruna Moshi "Boban",Idd Moshi,Kahabuka, George Magere Masatu, Charles Palapala,Mwinchumu Babel, Tippo Athumani "Zizzou", Shaffih Dauda, Saleh Ally,Kamba Lufo,Mbwiga wa Mbwiguke, Ibrahim Massoud "Maestroal",Clifford Mario Ndimbo, Abou Amokachi,Shearer Pamoja na Juma Assey



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...