Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia wakati wa hafla ya Utoaji Tuzo za Umahiri wa Uandishi wa Habari, iliyofanyika jana usiku April 24, 2015 kwenye Ukumbi wa Mlimani City, jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi mfano wa Hundi ya Sh. Milion tatu na Laki Nane (M.3.8) mshindi wa jumla katika kinyang’anyiro cha Tuzo za Umahiri wa Uandishi wa Habari (EJAT), Mwandishi wa habari wa Gazeti la Mwananchi, Mkinga Mkinga, wakati wa hafla hiyo ya utoaji tuzo iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Mlimani City, jijini Dar es Salaam, jana usiku Aprili 24, 2015. Kushoto ni Rais wa Baraza la Habari Tanzania, Jaji Mstaafu Robert Mihayo na Generali Ulimwengu.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi mfano wa Hundi ya Sh. Milioni kumi (M. 10) Mwandishi wa habari wa siku nyingi mkongwe, Generali Ulimwengu, wakati wa hafla hiyo ya utoaji tuzo iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Mlimani City, jijini Dar es Salaam, jana usiku Aprili 24, 2015. Kushoto ni Rais wa Baraza la Habari Tanzania, Jaji Mstaafu Robert Mihayo na (kulia) ni Mke wa Generali Ulimwengu.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi Tuzo mshindi wa pili wa jumla katika kinyang’anyiro cha Tuzo za Umahiri wa Uandishi wa Habari (EJAT), Mwandishi wa habari wa Gazeti la The Citizen, Lucas Liganga, wakati wa hafla hiyo ya utoaji tuzo iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Mlimani City, jijini Dar es Salaam, jana usiku Aprili 24, 2015.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...