Na Mwandishi Wetu.
MASHINDANO ya mchezo wa Darts Taifa yamezinduliwa rasmi leo jijini Dar
es Salaam katika Hoteli ya Moshi iliyopo Manzese kwa kushirikisha
mikoa mitano ya Tanzania.
Akizindua mashindano hayo Katibu Tawala wa Wilaya ya kinondoni,
Selestine Onditi ”kwanza aliwapongeza viongozi wa chama hicho kwa
juhudi za pekee za kufanya mashindano hayo yafanyike kwa mwaka wa
2015,lakini zaidi aliwashukuru wachezaji kwa moyo wa kupenda
mchezo kujigarimia kuacha kazi zao kutoka mikoani ikiwa pamoja na
wenyeji Dar es Salaam kuja kushiriki mashindano hayo ya Taifa kwa
kujilipia gharama zote za ushiriki hiyo inatia moyo sana kuwa ni dhahiri
mnaopenda mchezo”.
Alisema Onditi michezo ni afya,michezo ni furaha na michezo ni
kufahamiana basi aliwataka washiriki wote watumie nafasi hii ya
kukutana katika kuyafanikisha haya yote.
Onditi alitoa wito kwa wafadhili kuwa wasiegemee kwenye mpira wa
miguu tu kuna michezo mingi kama Darts na mingine wajitokeze
wadhamini kwani kwa kutumia wapenda michezo kama hawa
waliojitolea kutoka mikoani kwa gharama zao kuja kushiriki
mashindano ya Taifa ni nafasi ya pekee wewe mfanyabishara
kutangaza biashara yako.
Mwisho aliwatakia mashiondano mema yenye amani kuwa waanze
salama na wamalize salama na mwisho warejee majumbani salama
salimini.
Nae Mwenyekiti wa Chama cha Darts Taifa, Gesase Waigama alizitaja
zawadi kuwa ni Vikombe na Pesa taslimu kwa mfumo wa mashindano
utakaotumika ni wa Singles(mmoja mmoja), Doubles(wawili wawili) na
Timu.
Mwisho Katibu wa Chama cha Darts Taifa, Kalley Mgonja aliitaja mikoa
iliyofanikiwa kufika jijini Dar es Salaam kwa ushiriki wa mashindano ya
Taifa kuwa ni Mbeya, Morogoro, Dodoma, Arusha na wenyeji Dar es
Salaam.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...