Ofisa Elimu Taaluma Manispaa ya Ilala, Rehema Msogoloni (wa pili kulia) akisaidiana na Mkurugenzi wa Uhusiano na Sheria wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Steve Kilindo (wa pili kushoto), kufunua kitambaa ikiwa ni ishara ya makabidhiano ya kisima cha maji kilichojengwa kwa msaada wa TBL katika Shule ya Uhuru Mchanganyiko, Dar es Salaam jana. Kushoto ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Winners iliyosimamia ujenzi huo, Balozi mstaafu Herman Mkwizu na Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Anna Mshana.
 Wanafunzi wenye ulemavu wa Shule ya Uhuru Mchanganyiko, Abisina Rashid (kulia) na Rozalia Polycarp (wa pili kulia), wakishiriki katika uzinduzi wa kisima cha maji kwa kufungua maji baada ya Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), kukabidhi msaada wa kisima hicho kwa shule hiyo Dar es Salaam jana. Kisima hicho kitakachohudumia pia Shule ya Sekondari Benjamin Mkapa ujenzi wake ulisimamiwa na Kampuni ya Winners. Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Winners iliyosimamia ujenzi wa kisima hicho, Balozi mstaafu,Herman Mkwizu, Mkurugenzi wa Uhusiano na Sheria wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Steve Kilindo (wa pili kushoto),Ofisa Elimu Taaluma Manispaa ya Ilala, Rehema Msogoloni na Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Anna Mshana.
 Ofisa Elimu Taaluma Manispaa ya Ilala, Rehema Msogoloni (wa pili kulia) akisaidia kumtwisha ndoo ya maji Zarina Kigoma baada ya Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), kukabidhi msaada wa kisima cha maji kwa Shule ya Uhuru Mchanganyiko, Dar es Salaam jana.Anayeshangilia kushoto ni Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Anna Mshana.Kisima hicho kitakuwa kinahudumia pia Shule ya Sekondari ya Benjamin Mkapa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 29, 2015

    Ndugu Michuzi shukrani kwa kutuhabarisha kupitia blogu yako. Mimi naomba unifikishie maoni yangu po pote pale unapofikiri panahusika ili kama jamii tubadilishe utamaduni. Pamoja na ukweli kwamba katika karne ya 21 tunapaswa kuwa tumekwenda zaidi ya visima, hatuna budi kuwapongeza wanajamii na mashirika/makampuni yanayojitolea kuwachimbia visima wananchi wasiokuwa na maji safi (maji salama ni suala jingine). Lakini jambo ambalo huwa linanitia kichefuchefu ni kuona maafisa au viongozi wakiwatwisha ndoo za maji akina mama kama ishara ya kuzindua visima. Katika karne hii ya 21 basi wangekuwa wabunifu kidogo angaa wakatengenezesha mkokoteni wa kubeba ndoo mbili na kuzindua kwa kuonesha huyo mwanamama akisukuma mkokoteni badala ya kuendelea kumwona kuwa ni kiumbe cha kubebeshwa maji kichwani. Na pia inaweza kuonesha ufanisi kuwa badala ya huyo mwanamama kufanya safari mbili kwenda kisimani basi atafanya safari moja - anatumia muda huo mwingine kufanya shughuli nyingine. Tuache kuwatwisha akina mama ndoo za maji.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...