Na Avila kakingo,Globu ya Jamii.
WAIGIZAJI wa kikundi cha Origino Komedi  wamewaasa vijana kutumia vipaji vyao ili kutengeneza maisha yao kuwa  mazuri na sio kufikiri kuwa vijana wengi hushikwa mkono na mtu ili kufanikiwa.

Origino Komedi wazunguma mapema leo katika hafla fupi ya makabidhiano ya matrekta hayo na kampuni ya Matrekta ya Kilimo aina ya Sonalika kutoka kampuni ya Farm Equip Tanzania jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi Mkuu Mtendaji wa kampuni ya Farm Equip Tanzania,Arif Sheink amesema kuwa  vijana  wameamua kufanya jambo la maana kwa jamii ,"kwani wamenunua matrekta kwa ajili ya kilimo,vijana wengi wamekuwa wakinunua magari ya kifahari  bila kujua kunakesho na keshokutwa kwa maendeleo yao",alisema Bwa Arif.

Nae Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda amewapongeza vijana wa kundi hilo kuwa kufanya maamuzi sahihi na ya maendeleo kwa kununua Matrekta hayo kwaajili ya kilimo,amesema kuwa uamuzi wao ni mzuri hata kwa jamii kwani pia kwa namna moja ama nyingine itasaidia kuongeza ajira kwa vijana,kwakuwa kilimo kinahitaji watu wengine na sio wao wenyewe watakao weza kuendesha Matrekta hayo mashambani.

Kundi hilo la Origino Komedi  linaundwa na vijana 7 ambao ni Alex Chalamila(Mackregani),Josef Shamba(Vengu),Mjuni Sylivery(Mpoki,nyani Mzee),Lucacy Mhavile(Joti), Isaya Mwakilasa(Wakuvanga),Emmanuel Mgaya(Masanja mkandamizaji) na Davidi Seki.

 Waigizaji hao wameahidi kuyapeleka Matrekta yao kubeba takataka katika Wilaya ya Kinondoni, ambapo Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda atazindua  kampeni ya Ona aibu, ambayo itahamasisha usafi katika Wilaya ya Kinondoni.
 Mwigizaji wa Origino Komedi ,Mjuni Sylivery(Mpoki,nyani Mzee),akipewa maelekezo ya kuendesha Trekta mara Baada kukabidhiwa ufunguo wake na  Fundi Mkuu wa Kampuni ya Farm Equip Tanzania , Yunusu Nsekela wakati wa kukabidhiwa Matrekta kwa ajili ya kilimo jijini Dar es Salaam leo.
 Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda akizungumza katika makabidhiano ya Matrekta ya Kilimo kati ya Mkurugenzi Mkuu Mtendaji wa kampuni ya Farm Equip Tanzania,Arif Sheink na Waigizaji wa kundi la Origino Komedi, leo jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya Matrekta ya Kilimo ambayo waigizaji wa Kundi la Original Comedi wamekabidhiwa leo jijini Dar es Salaam. Picha na Avila Kakingo,Globu ya Jamii.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...