Baadhi ya wateja wakiwa ndani ya Airtel smartphone Bazaar ili

kusmartiphonica na simu za kisasa kwa bei poa.

Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel leo imetangaza offa kabambe ya
simu za kisasa itakayopatikana katika viwanja vya nane nane kuanzia
siku ya Ijumaa tarehe 31 julai 2015, kwa muda wa siku 10
Akiongea kuhusu ofa hiyo Meneja Masoko wa Airtel Bi Aneth Muga
amesema, Airtel inaendelea kuwapati wateja wake mawasiliano bora na
kuwaunganisha na simu za kisasa zilizounganishwa na vifurushi vya bure
vya internet katika msimu huu wa nanenane".

" Napenda kuwajulisha watanzania wote na wakazi wa Morogoro kuwa
Airtel   sasa tumewafikia na kusogeza huduma zetu karibu nao katika
viwanja vya nanenane ambapo tutakuwa na offa nyingi ikiwemo simu za
kisasa ya aina ya Airtel red itakayounganishwa na huduma za internet
bure kwa mwaka mzima kwa gharama ya shilingi 75,000.

Sambamba na Airtel Red pia tunazo simu za aina nyingi  ambazo ni
pamoja na simu ya Huawei , Techno, Samsaung. Simu hizi zinamuwezesha
mteja kuzitumia katika kufanya shughuli mbalimbali ikiwemo kutunza
rekodi zao, inatumika kama kamera ya kupiga picha pamoja na mambo
mengine mengi.

Tunatoa wito kwa wateja wetu watembelee banda la Airtel  katika
viwanja ya Nanenane na kupata nafasi ya kununua simu hizi za kijanja
kwa gharama nafuu "aliongeza Muga.

Airtel Smartphone Bazaar bado pia iko jijini Dar es Salaam katika
maduka yote ya Airtel. Khalikadhalika wateja wote bado pia wananafasi
ya kusmatiphonica kwa kutembelea maduka ya Airtel nchi nzima.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...