Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Said Magalula (katikati), akikata utepe kuzindua Duka jipya la Airtel Tanzania lililopo katika Barabara ya Uhuru jijini Tanga jana. Kushoto kwake ni Mkurugenzi wa Huduma kwa Wateja wa Airtel, Adriana Lyamba na (kulia kwake) ni Afisa wa Huduma kwa Wateja wa Duka hilo, Mwanavita Chiya. 
 Mkurugenzi wa Huduma kwa Wateja wa Airtel, Adriana Lyamba (wa pili kushoto), akifafanua jambo kwa  Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Said Magalula (kushoto), kuhusu bidhaa mbalimbali zinazouzwa katika Duka jipya la Airtel Tanzania lililopo katika Barabara ya Uhuru jijini Tanga, baada ya mkuu huyo wa mkoa kuzindua duka hilo jana. 
  Mkurugenzi wa Huduma kwa Wateja wa Airtel, Adriana Lyamba (kushoto), akifafanua jambo kwa  Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Said Magalula (mwenye miwani), baada ya mkuu huyo kuzindua Duka jipya la Airtel Tanzania lililopo katika Barabara ya Uhuru jijini Tanga jana.
 Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Said Magalula (wa pili kushoto), akikagua Duka jipya la Airtel Tanzania baada ya kulizindua katika hafla iliyofanyika dukani hapo katika Barabara ya Uhuru jijini Tanga jana. Kushoto ni Mkurugenzi wa Huduma kwa Wateja wa Airtel, Adriana. 
 Mkuu wa Mkoa wa Tanga,  Said Magalula (kulia), akiwa na Mkurugenzi wa Huduma kwa Wateja wa Airtel, Adriana Lyamba baada ya mkuu huyo, kuzindua Duka jipya la Airtel Tanzania lililopo katika Barabara ya Uhuru jijini Tanga jana.


KAMPUNI  ya simu za mkononi ya Airtel leo imezindua duka lake jipya
katika mkoa wa Tanga ikiwa ni jitihada zake za kuhakikisha inawapatia
wateja wake nchi nzima huduma bora na za kisasa.

Duka hilo la kisasa,  liko katika maeneo ya tanga mjini, Barabara ya
Uhuru, kwenye jingo la nyumbani hoteli. Huduma zinazotolewa na duka
hilo ni pamoja na kukusanya Ankara, kurudisha namba zilizopotea, mauzo
ya simu hasa smartphone, Airtel money, kusajili namba pamoja na huduma
za kimitandao.

Akiongea wakati wa uzinduzi , Mkurugenzi wa Kitengo cha huduma kwa
wateja wa Airtel, bi Adriana Lyamba alisema” uzinduzi wa duka hili ni
uthibitisho wa dhamira yetu ya kutoa huduma bora na kuwapatia  wateja
wetu uzoefu toufati  katika huduma zetu.  Leo tunawawezesha wateja
wetu na wakazi wa mkoa wa Tanga kupata hudumu muhimu kama vile za
kifedha za Airtel Money kwa usalama zaidi pamoja na kuwaunganisha na
simu za kisasa za smartphone na huduma zetu za intaneti”.

“Sambamba na hilo, duka letu pia litatoa ofa kabambe za simu na vifaa
vya aina tofauti na kuwawezesha wateja wetu kunganishwa na tecknologia
ya simu za mkononi ya kisasa.

Tunaamini vifaa vya kisasa ni sehemu muhimu ya mahitaji ya wateja wetu
kwa sasa,  hivyo kupitia watoa huduma wetu waliobobea kwenye maswala
ya tekinologia tunawewezesha wateja wetu kuchangua vifaa na simu bora
pamoja na kuwaunganisha na huduma za intanet. Ni matumanini yangu kuwa
wateja wetu sasa watapata suluhisho la mahitaji yao ya huduma za simu
kwa urahisi kupitia duka hili.” Aliongeza Lyamba.

Akizindua duka hilo Mkuu wa Mkoa wa Tanga , Magalula Said Magalula
alisema”  Mawasiliano yanachangia kwa kiasi kikubwa katika
kuwaunganisha watu na biashara na kukuza uchumi wa nchi. Nawapongeza
Airtel kwa kuongeza wigo kupitia huduma kwa wateja na kuleta
mabadiliko ya kibunifu. Tunaamini ubunifu huu utawawezesha wakazi
waTanga kupata huduma bora wakati wote,  na kwa hilo Tunawashukuru
sana Airtel.

“Natoa wito kwa wakazi wa Tanga na wateja wa Airtel kutembelea duka
hili  na kufurahia huduma na bidhaa za kisasa ikiwemo huduma ya Airtel
Money inayotoa suluhisho kwa mahitaji yao ya huduma za kifedha,
kufanya malipo na kutuma pesa kirahisi  zaidi”.

Mkuu wa Mkoa aliwahasa makampuni mengi zaidi kuiga mfano wa Airtel
katika kutoa huduma bora na kusema Serikali iko tayari kushirikiana
nao katika kuhakikisha inaboresha maisha ya wakazi na watanzania wa
ujumla katika maeneo mbalimbali nchini.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...