Bi. Bernadette Mathias ambaye kwa kushirikiana na mpiga piano mumewe Profesa Philip Mathias wakitumbuiza kwa wimbo wa "Tanzania, Tanzania nakupenda kwa moyo wote" kwa ufasaha na kusisimua waliohudhuria sherehe za Rais Jakaya Mrisho Kikwete kutunukiwa shahada ya heshima ya udaktari wa Sheria (Doctor of Laws honorific causa) na Chuo Kikuu cha Newcastle nchini Australia Julai 29, 2015.
Home
Unlabelled
Bi. Bernadette Mathias akiimba Wimbo wa Tanzania Nakupenda kwa Kiswahili katika sherehe za kumtunuku JK shahada ya heshima chuo kikuu ya newcastle, australia
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Wow she killed it..........
ReplyDeleteAsante sana Bernadette kwa kutuimbia wimbo Tanzania.
ReplyDeleteUnanikumbusha nyumbani wakati nasoma. Sijui kama mashuleni bado wanafundisha nyimbo kama hizi
Safi, sasa hii ilikuwa wapi jamani?
ReplyDeletehabari haijakamilika
Anon
Wimbo huu "Tanzania, Tanzania nakupenda kwa moyo wote -----"umeimbwa vizuri sana na mama huyu wa Australia na hiyo band ya muziki kuliko hata ambavyo baadhi yetu Watanzania wazalendo tungeweza kuuimba. Swali ni je, wangapi huo wimbo wangeweza au wanaweza kuuimba kwa ufasaha kama mama huyo wa Ausralia? Amempa heshima sana Rais wetu.
ReplyDeleteWimbo huu uko kama wimbo wa huzuni. Wimbo wa "sisi tunataka kuwasha mwenge" ndiyo tunaopaswa kuuimba zaidi. Pia wimbo wa " tazama ramani" nao ni mzuri, na unasisimua kuliko huo alioimba huyo mama.
ReplyDeleteTanzania Tanzania siku zote ni Wimbo mzuri. Bernadette ameimba vizuri na kutukumbusha kuwa tuna wimbo wetu. Mimi najiuliza nini kifanyike ili tung'amue kwamba huu ndito wimbo wa taifa. Yes kuna verses za kuongeza pamoja na chorus. Mungu ibariki tune si ya asili yetu tuachane nao.
ReplyDeleteNingekuwa JK ningempa huyu Trip ya kuja TZ kuiona nchi aliyoiimba na kuona vivuitio vya utalii. Inawezekana kaimba hata TZ kwenyewe hajafika.
ReplyDeleteDADA KAUA KABISA......YAANI MPAKA KACHOZI KAMENIBUBUJIKA...NAKUMBUKA NIMECHELEWA SHULE NIMECHELEWA NAMBA WATU WAPO MSTALINI NATAKA KUINGIA TU KAMWIMBO KANAANZA BASI NAZUGA MPAKA NAKAA KWENYE LINE NAKUANZA KUUIMBA KWA HISIA ..........HAKIKA TANZANIA HII NI MAMA TUMTUNZE
ReplyDelete