Meneja Uhusiano wa DSTV Barbara kambogi akizungumza na
waandishi wa habari hawapo pichani juu ya moto wa la Liga utawashwa ndani ya
Super Sport 3(SS3)katika hafla iliyofanyika katika Hoteli ya New Afrika leo
jijini Dar es Salaam.Kulia Meneja Uhusiano wa DSTV Barbara kambogi na Afisa masoko wa Multichoice Tanzania, Furaha Samaly.
Meneja uendeshaji wa DST,Ronald Shelukindo akizungumza na waandishi wa habari juu chanmeli mpya ya michezo katika kingamuzi cha Multchoice,katika hafla iliyofanyika leo katika Hoteli ya New Afrika jijini Dar es Salaam.Kushoto ni Meneja Uhusiano wa DSTV Barbara kambogi.
Sehemu ya waandishi wa habari wakifatilia taarifa katika uzinduzi wa channel katika hafla iliyofanyika leo katika Hoteli ya New Afrika jijini Dar es Salaam. Picha Emmanuel Massaka, Globu ya jamii.
Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii
WATAZAMAJI wa Supersport watakuwa nafasi pekee kushuhudia
mechi kwenye ubora wa HD pamoja na michuano ya Ligi kuu ya Uingereza (EPL),Ligi
ya Hispania (La liga),Ligi ya Mabingwa wa Ulaya
(UEFA),Ligi ndogo za Ulaya (Europa),Mechi za FIFA za kirafiki za
kimataifa na Klabu bingwa ya Dunia ,Kombe la Ujerumani ,Kombe la Mfalme
Hispania (Copa Del Rey) na Kombe la FA.
Akizungumza na waandsihi wa habari leo Meneja Uhusiano wa Multchoice,Babra
Kambogi amesema wateja wa DStv wateja wa DStv wakae tayari kwenye msimu wa
mabingwa ulimwenguni ambapo Barcelona wanajiandaa kutawala dunia kwa mara
nyingine huku Manchester United wakihitaji kurudisha kiti chao cha ubingwa
Uingereza.
Amesema katika msimu huu zaidi ya mechi 900 za kimataifa zitaonyeshwa
kimataifa na wateja wa DSTV Compact Plus wataweza kufurahia baadhi ya mechi zaidi 450 live
huku wateja wa Dstv premium watazawadiwa mechi zote.
Babra amesema wateja wa Dstv vituko vya michuano yote ya
ligi kuu Uingereza vitaletwa kupitia Suparspot (SS5) kinochopaatikana katika
kifurushi cha Premium na SS5 itakuwa ndio nyumba ya soka la Afrika kwa Ligi kuu
ya Uingereza.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...