Bendi maarufu ya muziki wa dansi barani ulaya Ngoma Africa band maaruka kama FFU-Ughaibuni au viumbe wa ajabu Anunnaki Alien's inayoongozwa na kamanda Ras Makunja,bendi hiyo yenye makao yake kule ujuerumani ,juzi iliuhakikishia ulimwengu tena kuwa mziki wao ni moto wa kuotea mbali! bendi hiyo ilifanikiwa kwa mara nyingine kuyafunika maonyesho ya kimataifa ya International African Festival-Tübingen 2015,yaliofanyika katika viwanja vya Fest Platz,jijini Tübingen,Ujerumani. Bendi hiyo ilipanda jukwaani majira ya saa 4.00 usiku huku uwanja huo ukiwa umezungukwa na ulinzi mkali ! kamanda Ras Makunja akikiongoza jukwaani kikosi chake kilichoshamili vijana wa kazi akina Afande Mo Benda (Soloist) Sajent JoJo Sousa(Drumer) Kopro. Aj Nbongo (Bass) kijana Liga (Rhthym guitar) madansa Jessica Ouyah na Sarah Fina kikosi hiko kilifanya show la kukata na shoka.siku ya jumamosi 26 Julai 2015. wapitie at www.facebook.com/ngomaafricaband wasikilize at www.reverbnation.com/ngomaafricaband
kamanda Ras Makunja akiongoza mashambulizi.
Mshika Mtutu wa Ngoma Africa band akiucharaza kisawasawa.
Nyomi la nguvu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...