Na Mwandishi Wetu,
SERIKALI ya Tanzania imeelezea utayari wake wa kupiga jeki na kuwajumuisha wafanyakazi wa afya ya jamii katika nguvukazi ya sekta ya afya (national health workforce) ya taifa ili kuboresha afya ya jamii hususani katika maeneo ya vijijini.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa semina ya wadau wa mradi wa mafunzo ya wafanyakazi wa afya ya jamii (Community Health Worker Learning Agenda Project - CHW-LAW) jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji (idara ya uzazi na afya ya mtoto) katika Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Bi Georgina Msemo alisema ni muhimu kuwajengea uwezo wafanyakazi wa afya ya jamii ili kukidhi mahitaji ya kijamii. 

Akimwakilisha Mkurugenzi wa Huduma za Kinga katika Wizara ya Afya, Dkt Neema Rusibamayila, Msemo aliwaasa wadau kufanya tafiti ya kisayansi ili kukabiliana na hali ya upungufu wa wafanyakazi wa afya ya jamii, ambao umekuwa ni kikwazo kikubwa katika utoaji wa huduma za kiafya nchini. 

Msemo alipongeza hatua ya wadau hao kwa kuzungumzia masuala ya wafanyakazi wa afya ya jamii pamoja na kuja na mradi utakaowezesha wafanyakazi hao kupata mafunzo ya kila mara ili kuboresha utendaji wao katika utoaji wa huduma ya afya ya jamii. 
Mchunguzi Mkuu mradi wa mafunzo ya wafanyakazi wa afya ya jamii, Profesa Japhet Killewo akizungumza na wadau wa sekta ya Afya ya Jamii (hawapo pichani) wakati wa ufunguzi wa semina ya Wadau wa  Juu Agenda ya Mradi wa Mafunzo kwa Wafanyakazi wa Afya ya Jamii jijini Dar es Salaam Jumanne. 
Mkurugenzi Mtendaji (idara ya uzazi na afya ya mtoto) katika Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Bi Georgina Msemo akizungumza na wadau wa sekta ya Afya ya Jamii (hawapo pichani) wakati wa ufunguzi wa semina ya Wadau wa  Juu Agenda ya Mradi wa Mafunzo kwa Wafanyakazi wa Afya ya Jamii jijini Dar es Salaam Jumanne.
Wadau wa sekta ya Afya ya Jamii katika picha ya pamoja wakati wa ufunguzi wa semina ya Wadau wa  Juu Agenda ya Mradi wa Mafunzo kwa Wafanyakazi wa Afya ya Jamii jijini Dar es Salaam Jumanne. Picha na mpiga picha wetu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...