Mwanamuziki wa Muziki wa kizazi kipya  Maarufu  kama bongo fleva KLEYAH ambaye anakuja kwa kasi katika Tasnia hiyo  hatimaye amezindua nyimbo yake mpya inayokwenda kwa jina la MZOBE MZOBE wimbo aliomshirikisha msanii maarufu  maarufu kutoka THT Barnaba Boy CLASSIC nyimbo ambayo inatabiriwa kufanya vizuri katika soko la musiki wa Tanzania.
KLEYAH ambaye ni Mhitimu wa shahada ya mawasiliano kutoka chuo kikuu cha cha Phoenix nchini marekani na baadae kufanya kazi katika shirika la kimataifa la UNDP kabla ya  kuacha na kuamua kurejea nchini kwa ajili ya kuendeleza na kukuza sanaa yake Tayari amefanikiwa kufanya kazi na watayarishaji na wasanii wakubwa ambapo mwaka 2014 alifanikiwa kufanya nyimbo mbili ambazo zilirekodiwa nchini Kenya na mtayarishaji maarufu nchini humo Lucas Bikedo pamoja na kufanyia Video kwa watayarishaji maarufu nchini Kenya kwa sasa OGOPA DJS.
Katika nyimbo yake mpya ambayo ilizinduliwa Tarehe 6 Mwezi November na kuchezwa katika vituo mbalimbali vya Radio nchini Tanzania na Africa mashariki kwa ujumla na hatimaye leo umefanyika uzinduzi wa Video yake ya wimbo wa MSOBE MSOBE unataraji kutambulishwa katika vituo mbalimbali vya Televission kwa ajili ya kumtambulisha msanii huyo ambaye anaonekana kuja kwa kasi katika sanaa hii ya music wa kizazi kipya.
Akizungumza nara Baada ya uzinduzi wa Video yake msanii KLEYAH amesema kuwa kwa sasa mipango yake ni kuendelea kufanya kazi pamoja na watayarishaji wakubwa nchini Tanzania pamoja na wasanii maarufu ili kukamilisha album yake ambayo amepanga kuizindua mwezi July mwaka 2016 album ambayo ametamba kuwa itasheheni aina mbalimbali za misic ili kuwafurahisha mashabiki wanaofwatilia kazi zake.
Ameongeza aliamua kufanya music kwa kuwa ni kitu ambacho kipo ndani ya moyo wake  huku akieleza kuwa kusoma na baadae kufanya music ni jambo la kuigwa na wasanii wa Tanzania kwani itamsaidia msanii kutoboa tu si ndani ya nchi lakini Barani Africa na duniani kwa ujumla 
Pia waweza kumfuata kwenye:
Instagram@kleyahmusic
facebook@kleyahmusic
vevo na utube ni kleyahvevo


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...