Waziri wa Fedha na Mipango, Philip Mpango (Katikati) akiwakabidhi Naibu waziri wa katiba na sheria, Amon Mpanju(kulia) na Mtendaji mkuu wa Mahakama Hussein Kattanga cheki ya shilingi Bilioni 12 na milioni mia tatu ikiwa ni kutimiza ahadi  ya Rais Dkt. John Pombe Josef Magufuli aliyoahidi siku alipokuwa mgeni rasmi siku ya Mahakama hapa nchini ikiwa ni siku tano tuu tangu siku ya kuahidi.
Waziri wa Fedha Mipango, Philip Mpango (Katikati) akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, kuhusiana na kutimiza ahadi aliyoiahidi Rais  Dkt. John Pombe Josef Magufuli alipoahidi katika maadhimisho ya siku ya mahakama hapa nchini. Kulia ni Naibu waziri wa katiba na sheria, Amon Mpanju na kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Servacius Likwelile. 
Mtendaji mkuu wa Mahakama Hussein Kattanga (kushoto)akimshukuru Rais  Dkt. John Pombe Josef Magufuli kwa kutimiza ahadi yake aliyoiahidi siku ya maadhimisho ya siku ya mahakama. kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Servacius Likwelile.
Picha na Avila Kakingo wa Globu ya Jamii.

 Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii 
WIZARA ya Fedha na Mipango imetoa sh.bilioni 12.3 kwa ajili shughuli za mahakama ikiwa ni sehemu ya ahadi ya  Rais Dk. John Pombe Magufuli aliyoiahidi katika kilele cha maadhimisho ya  siku ya mahakama.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango amesema fedha hiyo imetolewa kwa kutimiza ahadi ya Rais ya uendeshaji wa shughuli za mahakama.

Mpango amesema kuwa ahadi ya Rais ilikuwa ni ya siku tano ambazo zimetimia kwa kutoa hundi ya sh.bilioni 12.3 ambazo zitakwenda kufanya kazi iliyokusudiwa.

Amesema kuwa Wizara ya Fedha na Mipango kutokana na ahadi hiyo imefanya kuweka wazi juu ya fedha hizo kwa waandishi wa habari.

Nae Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria, Amon Mpanju amesema lengo ni kuongeza kasi kwa mashauri yaliyopo kuondoshwa  pamoja na waliokwepa kodi  yashughulilikiwe.

Ahadi ya Rais ilitolewa baada ya maombi ya Jaji Mkuu, Othman Chande katika maadhimisho ya  kuanza kwa mwaka wa mahakama kudai kuwa wana uhaba fedha za maendeleo  katika kuweza kuendesha shughuli za kimahakama.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Hongera sana Rais wetu. Uwezo huu umetokana watu kulipa kodi. Kama kuna uwezekano VAT ipungue kidogo na kufanyike kampeni kubwa ya kuhamasisha ulipaji wa kodi. Kampeni hii ilenge kukusanya tr 2 kwa mwezi. Kila mtu lazima alipe kodi. Watu wakiona matumizi mazuri ya ela watalipa kodi. Fedha zikienda elimu watu waambiwe kuwa ni kodi zao. Zikienda kuboresha afya watu waambiwe kuwa ni kodi zao. Kwa taarifa hizi watu watashawishika kulipa kodi. Watu lazima walipe kodi.

    ReplyDelete
  2. Mheshimiwa Magufuli sasa nimeamini wewe ni mteule wa Mungu, na siku ukifa utafanywa na kusimikwa rasmi kuwa Rais wa malaika. Kila lakheri.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...