·        Airtel yatoa ajira kwa wanafunzi wenye vipaji katika vyuo vikuu

Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel imedhamini kongamano la ajira  kwa vijana wa chuo kikuu linaloandaliwa na AIESEC Tanzania  lenye lengo la kuwaweka pamoja waajiri (makapuni) na waajiriwa watarajiwa (wanafunzi)  kwa lengo la kuwapatia Fursa zitakazowasaidia katika kuendesha shughuli za kiuchumi.

Kila Mwaka AIESEC huandaa kongamano la ajira kwa vijana linaloshirikisha wanafunzi zaidi ya 1500 kutoka katika vyuo vikuu mbalimbali nchini. Kuanzia mwaka jana Airtel  imejikita na kushiriki  katika kongamano hilo ikiwa ni sehemu ya kuendeleza dhamira yake ya kuwawezesha vijana wanaohitimu vyuoni kupata ajira.

Akiongea kuhusu mpango huo, Meneja Rasilimali watu wa Airtel , Gabriella Kaisi alisema”Tunayofuraha kuwa sehemu ya mpango huu kwa kushirikiana AIESEC Tanzania lengo likiwa ni kuwafikia na kuwaajiri vijana wenye vipaji kutoka katika vyuo vikuu mbalimbali nchini. Tunaamini kila kijana ana nafasi ya kufikia ndoto zake  na ndio mana tunatoa fursa  kwa vijana kufanya kazi pamoja nasi. 

Mwaka jana tuliwawezesha vijana watatu wahitimu kutoka vyuo vikuu vya IFM pamoja na chuo kikuu cha Dar es salaam kupata ajira katika ofisi zetu za Airtel. Vijana hao ni pamoja na Abubakar Nassor ambaye anafanya kazi katika kitengo cha masoko James Kwayu yuko katika kitengo cha Huduma kwa wateja na Gerald Msafiri anafanya kazi katika kitengo cha mauzo.

Vijana hawa watapata nafasi ya kwenda kufanya kazi nje ya nchi katika makao makuu ya Airtel  nchini Kenya na India  kwa muda wa mienzi miwili kuanzia mwezi wa Mei hadi Julai 2016. Watakaporudi watapangia kufanya katika vitengo tofauti ili kupata uzoefu na mwanga zaidi aliongeza Kaisi

Akiongea kuhusu program hiyo, moja kati ya waliofaidika na mpango katika kitengo cha masoko, Abubakar Nassor alisema” najisikia furaha kuwa mwanachama wa AIESEC Tanzania kwani kumeniwezesha kupata fursa hii adimu ya ajira, uzoefu katika kazi na nafasi ya kujifunza katika kampuni kubwa ya simu duniani. Nimejipanga vyema kujifunza zaidi katika miezi 2 nitakayokuwa  nchini India na Nairobi,   nahaidi kuitumia fursa hii vyema ili kuweza kuzifikia ndoto zangu

Mwaka huu Airtel imejipanga kuendelea kuwafikia vijana wengi zaidi kwa kutoa ajira kwa vijana wengine watano ambao watafanya vizuri na kufaulu mitihani mbalimbali inayoendelea kwa sasa.  Airtel itatangaza majina ya wanafunzi wengine watakaofudhu na kuchaguliwa kwa mwaka huu mara baada ya hatua za uajiri zitakapokamilika.

Meneja Rasilimali watu wa Airtel, Bi, Gabriella Kaisi (kulia) akiwapongeza James Kwayu (katikati) na Abubakar Nassor ambao ni wanafunzi wa vyuo waliofaidika na aiira katika kampuni ya Airtel kupitia ushirikiano kati ya Airtel na chama cha wanafunzi vyuoni Tanzania AIESEC wenye lengo la kuwawezesha vijana walioko vyuoni kupata ajira katika makampuni mbalimbali kila mwaka.
Meneja Rasilimali watu wa Airtel , Bi, Gabriella Kaisi akimkabithi cheti cha pongezi Abubakar Nassor baada ya kufaulu mitihani na kuajiriwa na Airtel katika kitengo cha huduma kwa wateja kupitia ushirikiano kati ya Airtel na AIESEC Tanzania (chama cha wanafunzi vyuoni) wenye lengo la kuwawezesha vijana waliokoa vyuoni kupata ajira katika makampuni mbalimbali kila mwaka. 
Meneja Rasilimali watu wa Airtel , Gabriella Kaisi akimkabithi cheti cha pongezi James Kwayu baada ya kufaulu mitihani na kuajiriwa na Airtel katika kitengo cha huduma kwa wateja kupitia ushirikiano kati ya Airtel na AIESEC Tanzania (chama cha wanafunzi vyuoni) wenye lengo la kuwawezesha vijana waliokoa vyuoni kupata ajira katika katika makampuni mbalimbali kila mwaka
Meneja Rasilimali watu wa Airtel , Gabriella Kaisi (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na James Kwayu na Abubakar Nassor ambao ni wanafunzi wa vyuo waliofaidika na ajira kupitia ushirikiano kati ya Airtel na AIESEC Tanzania (chama cha wanafunzi vyuoni) wenye lengo la kuwawezesha vijana waliokoa vyuoni kupata ajira katika makampuni mbalimbali kila mwaka.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 04, 2016

    Airtel endelea kuwaelekeza mahali palipo na fursa vijana wanaouliza waanzie wapi.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...