Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dakta JOHN MAGUFULI amewahimiza viongozi wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania- BAKWATA- waendelee kuombea amani katika taifa na kukemea ipasavyo vitendo vya uhalifu katika jamii ya Kitanzania.
Kauli hiyo ya Rais imetolewa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania SAMIA SULUHU HASSAN kwa niaba ya Rais katika tafrija ya futari iliyoandaliwa na Baraza Kuu la Waislamu Tanzania- BAKWATA- katika uwanja wa shule ya sekondari ya KINONDONI MUSLIM jijini Dar es Salaam.
Rais Magufuli amesema jamii yeyote inayolelewa na kukua katika misingi ya kufuata maandiko ya Mwenyezi Mungu ni vigumu kujiingiza kirahisi katika vitendo vinavyomchukiza Mungu vikiwemo vitendo vya uhalifu.

Rais MAGUFULI pia amewatakia kheri waumini wote wa dini ya kiislamu kote nchini katika mfungo wa mwezi Mtukufu wa Ramadhani.
Kwa upande wake, Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh ABUBAKAR ZUBEIR ameipongeza serikali kwa hatua inazochukua katika kukabiliana na vitendo vya uhalifu hapa nchini na kusisisita kuwa Viongozi wa BAKWATA na wataendelea kushirikiana na serikali katika kukemea vitendo viovu katika jamii kama hatua ya kuhakikisha vitendo vya uhalifu vinakoma hapa nchini.

Mufti wa Tanzania pia ametoa rai kwa waislamu wote nchini wadumishe umoja,upendo na mshikamano miongoni mwao katika Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani na hata baada ya mfungo kama kitabu kitukufu cha QUR’AN kinavyoelekeza.

Imetolewa na
Ofisi ya Makamu wa Rais.
26-Jun-16

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu  Hassan akizungumza wakati wa tafrija ya Futari iliyoandaliwa na Baraza Kuu la Waisalm wa Tanzania (Bakwata) iliyofanyika kwenye uwanja wa shule ya sekondari ya Kinondoni Muslim ambapo alimuwakilisha Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na kuwahimiza viongozi wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) waendelee kuombea amani katika Taifa na kukemea ipasavyo vitendo vya uhalifu katika jamii ya Kitanzania.
Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Abubakar Zubeir akizungumza wakati wa tafrija ya futari iliyoandaliwa na Baraza Kuu la Waislamu wa Tanzania ambapo alisema uongozi wa sasa wa BAKWATA umedhamiria kudumisha umoja,upendo na mshikamano baina ya Waislamu wote nchini, Tafrija hiyo ambayo mgeni rasmi alikuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan aliyemuwakilisha Mheshimiwa Rais wa Jamhuri Muungano wa Tanzania.
Sehemu ya wageni waliohudhuria tafrija ya futari iliyoandaliwa na Baraza Kuu la Waislam katika viwanja vya Shule ya Sekondari ya Kinondoni Muslim  jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Jopo la Masheikh Sheikh Suleiman Amran Kilemile akitafsiri moja ya aya ya Quran inayojenga na kuimarisha umoja na mshikamano kwa waislam.
Sheikh Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Shekh Alhad Mussa Salum akitoa utambulisho wa wageni wa jumuiya mbali mbali za waislam waliohudhuria tafrija ya futari iliyoandaliwa na Baraza Kuu la Waislamu Tanzania na kuhudhuriwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan.
Viongozi wa Wanawake Waislamu Tanzania wakisikiliza kwa makini nasaha  za viongozi mara baada ya kufuturu katika tafrija ya futari iliyoandaliwa na Baraza Kuu la Waislamu Tanzania.


BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...