Balozi wa Algeria Nchini Saad Balabed akizungumza na waandishi wa habari kuelekea katika Tamasha la uzinduzi wa kitabu cha Safari ya Soka la Tanzania 1926 hadi 2016 ambapo ataitumia pia siku hiyo kusherehekea siku ya Uhuru wa nchi yake pamoja na wachezaji wa zamani wa Simba na Yanga.
 Mkurugenzi wa Taasisi ya Taasisi wa Michezo na Burudani (TSERP) Omari Bahari akitolea ufafanuzi juu ya uzinduzi wa kitabu hicho kitakachozinduliwa Julai 30 katika Tamasha litakalohusisha maveterani wa zamani wa Simba na Yanga pamoja na mabalozi wa nchi mbalimbali watakaoshiriki kimichezo ikiwemo kucheza mechi.
 Balozi wa Algeria Nchini Saad Balabed akiwa katika picha ya pamoja na wachezaji wa zamani wa Simba na Yanga.

Na Zainab Nyamka. 
KATIKA kukuza soka na kumbukumbu ya mchango wa wachezaji wa zamani katika mchezo wa mpira wa miguu  Taasisi ya Utafiti wa Michezo na Burudani (TSERP) imeamua kuandaa uzinduzi wa kitabu kitakachokuwa kinajulikana kwa jina la Safari ya Soka la Tanzania  1926-2016 huku  siku hiyo ikisindikizwa na bonanza litakalowahusisha mabalozi wa nchi mbalimbali wakiumana na kombaini ya maveterani wa  Simba na Yanga huku mgeni rasmi akitarajiwa kuwa Waziri Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Moses Nnauye huku Balozi wa Algeria nchini Tanzania Saad Balabed akitumia siku hiyo kusherehekea sikukuu ya uhuru wa ncho yake kwa kutimiza miaka 54.

Tamasha hilo linatarajiwa kufanyika  Julai 30 katika uwanja wa Taifa huku likisindikizwa na mechi mbalimbali kati ya Magic FM wakiumana na Kikundi cha uchekeshaji, Kampuni  ya Oryx ikipambana na Kombaini ya watuma salamu kutoka Jijini Dar es salaam wakiungana na wa mkoa wa Pwani, pia kutakuwa na mchezo mwingine kati ya Simba na Yanga maveterani. 

Mkurugenzi wa Taasisi hiyo, Omari Bahari amesema kuwa lengo la kufanya tamasha hilo ni kuweza kuwakumbusha wananchi mchango mkubwa uliofanywa na wachezaji wa zamani ambapo umeweza kutufikisha hapa tulipo.

Bahari amesema kuwa, katika kuwaenzi wachezaji hao na jinsi gani walivyojitolea katika mchezo wa mpira wa miguu kutakuwa na picha mbalimbali za vikosi  vya yimu ya Taifa ambapo kimojawapo ni kile cha mwaka 1980 kilichoipeleka nchi yetu katika fainali za mataifa Afrika, pamoja na hilo pia kutakuwa na kikosi ambacho kilicheza mbele ya Hayati Baba wa Taifa Julius Kambarage Nyerere na Raisi wa Sudani wakiwa hawajavaa jezi. Mbali na hilo pia, watajumuisha na picha ya Kikosi cha Simba kilichofika hatua ya Fainali kombe la Shirikisho mwaka 1993 na Yanga wakioingia hatua nya robo fainlai mwaka 1986.

Balozi wa Algeria, Balabed amesema kuwa amefurahi sana kuweza kusherehekea sikukuu ya Uhuru wa  nchi yake kwa kudumisha michezo na akiwa kama balozi hapa nchini kwa takriani mwaka mmoja atahakikisha anasaidiana na Tanzania katika kukuza na kuendeleza mpira wa miguu kama wanavyoshirikiana katika sekta ya elimu. Amesema kuwa katika siku hiyo watafurahi kwa pamoja na watadumisha utamaduni huo kwani anaamini michezo inaunganisha watu wa aina mbalimbali na pia inajenga urafiki.

Mkurugenzi  Mtendaji wa kampuni ya Property Internatonal Limited Masoud Khalfani amesema hatua hiyo ni nzuri sana kwani itawakutanisha wachezaji wote wa zamani na wao wamefurahi kuweza kushirikiana nao ili kufikia lengo la kumbukumbu ya wachezaji wa zamani na wapi wameufikisha mpira hadi hapa ulipo.

 Na moja ya  mavetreani wa timu ya Yanga, Keneth Mkapa amesema kuwa kwanza wamefurahi sana kuweza kucheza mechi hiyo na maveterani wa Simba kwanza itakuwa ni moja ya mechi nzuri na italeta hamasa kwa vijana wanaocheza sasa hivi kwani wataonesha uwezo wa hali ya juu. 

Baadhi ya wachezaji wa zamani waliohudhuria ni Keneth Mkapa, Thomas Kipese, Mohamed Mwameja, Iddy Kibobe, Moses Mkandawile, Mohamed Hussein, Mohamed Mmachinga.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...