Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania(TCAA) imeendelea kutoa mafunzo kwa watumishi wake  yanayolenga kuboresha utendaji  na utoaji wa huduma zinazokidhi matarajio ya wateja  na kuachana na mtindo wa kutoa huduma  hizo kwa mazoea.

Mafunzo hayo yanayofahamika kama ‘Culture Change’, yanaendeshwa kwa awamu ambayo yalianza na wajumbe wa bodi, wakurugenzi, wakuu wa vitengo na sasa yanatolewa kwa maafisa waandamizi wa  na kisha  kwa watumishi wengine wote wa TCAA lengo ikiwa ni kuboresha huduma za Mamlaka kwa wateja.

Mkurugenzi Mkuu wa TCAA, Hamza Johari amesema kuboresha huduma kwa wateja wa Mamlaka ni miongoni mwa vipaumbele vya Mamlaka hiyo kwa sasa, ili kuwezesha ukuaji wa sekta ya usafiri wa anga Tanzania na kuchangia kikamilifu katika ukuzaji wa uchumi.

Amesema ni muhimu kuwekeza katika mafunzo yanayolenga kuboresha watumishi ambao ni raslimali muhimu sana katika mafanikio ya taasisi  au kampuni yoyote ile. “Utafiti unaonyesha mafanikio ya taasisi kwa kiasi kikubwa yanachangiwa na mtazamo chanya wa watumishi kuhusu mahala wanapofanyia kazi ambapo uzoefu na elimu vinachangia kwa kiasi tu mafanikio hayo” ameongeza Hamza.

Pamoja na mambo mengine mafunzo hayo yanalenga kuchagiza watumishi wa Mamlaka kutoa huduma zenye viwango vya juu, kuimarisha ushirikiano miongoni mwao, kuwa na mtazamo chanya kuhusu kazi zao, kuachana na utamaduni wa kulalamika badala yake kutafuta suluhu kwa pamoja kutatua  changamoto za mahala pa kazi .
Meneja Raslimali Watu, Viola Masako (mwenye kipaza sauti) akiwakaribisha watumishi (hawapo pichani) katika mafunzo ya ‘culture change’. Wengine kutoka kushoto ni Mkurugenzi Mkuu TCAA, Hamza Johari na Mkurugenzi Huduma za Mamlaka, Mbottolwe Kabeta
Maafisa waandamizi wa TCAA wakifuatilia mafunzo yanayoleanga kuboresha utendaji kazi na utoaji wa huduma kwa wateja, katika ukumbi wa mikuano wa Mamlaka, Banana- Ukonga

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...