THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

NEWS ALERT: ASKARI POLISI WATATU WAUWAWA USIKU HUU HUKO MBAGALA MMBANDEJIJINI DAR ES SALAAM


Taarifa iliyotufikia usiku huu inaeleza kuwa, kuna tukio la kuuwawa kwa Askari Polisi, lililotokea huko Mbagala jijini Dar.
Inadaiwa kuwa askari hao walikuwa wakibadilishana lindo katika Benki ya CRDB tawi la Mbagala Mmbande na mara wakaibuka watu wanaodhaniwa kuwa ni Majambazi na kuanza kuwashambulia kwa risasi na baada ya shambulizi wanadaiwa kuondoka na pikipiki wakielekea maeneo ya Mvuti.
ASKARI WALIOFARIKI ni
E5761 CPL YAHAYA
F4660 CPL HATIBU NA
G9544 PC TTITO.
Inasemekana kuwa tukio hilo limetokea mnamo saa 1: 30 ni katika tukio la UVAMIZI WA BANK CRDB MBANDE na inadaiwa kuwa wahalifu hao waliondoka na silaha moja aina ya SMG.
Tukio hili limetokea wakati askari wakibadilishana lindo. Mmoja aliyefariki alikuwa anaingia, mmoja alikuwa anatoka na mwingine alikuwa dereva.
Inadaiwa kuwa majambazi hayo  hayakuingia ndani ya benki. 
Gari la Polisi (Leyland Ashok) limeharibiwa  kwa risasi.
Kamanda wa polisi kanda maalum ya Dar es salaam Simon Sirro amethibitisha na kusema: "Ni kweli kumetokea tukio la uvamizi hapa mbagala lakini kwa taarifa kamili ntazitoa kesho kwakuwa bado nipo eneo la tukio kwa ajili ya uchunguzi zaidi".Waziri Ummy Mwalimu aweka jiwe la msingi awamu ya pili ya jengo la hospitali ya Agakhan, aitaka ijenge ingine Dodoma

Serikali imeuomba uongozi Wa Agakhan kujenga hospitali nyingine kubwa katika mkoa Wa Dodoma ili kuendana na agizo la Rais Wa awamu ya tano Dkt.John Magufuli na kuboresha huduma bora za afya Mkoani humo. 
 Akizungumza hayo wakati wa ufunguzi wa awamu ya pili ya jengo la hospitali ya Agakhan Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia , Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu amesema kuwa Agakhan wanatakiwa wajenge hospitali nyingine kubwa mkoani Dodoma ili kueneza Huduma bora za kiafya. 
 "Kutokana na Agizo la Rais Wa awamu ya tano Dkt. John Magufuli la kuhamia Dodoma inabidi na nyinyi mjenge hospitali kule" alisema Mhe. Ummy. Mhe. Ummy ameongeza kuwa kwa kujengwa hospitali hiyo Serikali itakua iokoa shilingi billion 20 mpaka 25 kwa ajili ya wagonjwa kwenda kutibiwa nje ya nchi. 
 Aidha Mhe.Ummy amesema kuwa anaushukuru uongozi Wa Agakhan kwa kuanza kujenga jengo ilo linalogharimu Billioni 112 ili kuondoa kero kwa wagonjwa Wa magonjwa yasioambukiza na kurahisiaha huduma na matibabu bora kwa wagonjwa nchini.
 Mbali na hayo Mwenyekiti wa kamati ya bodi hospitali ya Agakhan Bi. Zahra Aga Khan amesema kuwa wanampango Wa kumaliza jengo hilo kwa ajili ya kutoa Huduma bora za kiafya nchini ili kutokomeza maradhi ya mara kwa mara. 
 "Tuna morali kubwa ya kumalizia jengo hili ili tuweze kuboresha Huduma ya afya nchini kwa kutoa tiba zenye uhakika na za kisasa" alisema Bi Zahra
Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii, Wazee, Jinsia na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu wa tatu kulia akitia udongo kwenye kichanja cha nondo kuashiria kuzindua rasmi ujenzi wa awamu ya pili wa jengo la hospitali ya Agakhan katika uzinduzi huo uliofanyika leo jijini Dar es salaam, na wa pili kushoto ni Mwenyekiti wa kamati ya bodi hospitali ya Agakhan Bi. Zahra Aga Khan.


BREAKING: US BLOGGER AIBUKA, AMSAKA JOHN MASHAKA KWA UDI NA UVUMBA

Ankal Wasalaam,
 Wadau wote wa Blogu ya jamii, natumai mu wa wazima wa Kheri. Mimi mzima, na naendelea na kazi yangu ya u professor, nikifundisha masomo ya “Political Economics” hapa nchini Uingereza. Hii ni baada ya kumaliza Phd yangu pale Oxford University mwaka 2014 ambako nilikuwa Mwafrika wa kwanza kuvunja rekodi kwa kuandika thesis iliyokubalika na vyuo vikuu vikubwa duniani. Nadhani wasomi wengi wa hii blogu wananifahamu vizuri sana, kwa sababu bila mimi, hata John Mashaka asingeupata umaarufu alioupata. 
Niseme kwa kifupi nilimjenga John Mashaka, kwa kumsaidia sana kwenye utafiti kipindi akiwa chuo kikuu. Ingawa kila mtu ana kipaji chake cha kuzaliwa, ambayo nakiri kwamba Ndugu John anacho na ni Genius, ila pia lazima asaidiwe. Nimemsaidia mimi. Niko tayari zaidi kwenda kumsaidia Dr. Magufuli kujenga uchumi wa Tanzania.
Pamoja na wadau wengine, naungana nanyi kumuita John Mashaka atoke mafichoni na kurudi kwenye hii blogu ili mijadala ya kisomi iendelee. Nadhani Tanzania kama taifa hipo katika kipindi kigumu. Kipindo cha mpito ambapo mawazo chanya kama yangu, John Mashaka na genge lake wanaweza kuchangia. Nikiwa Professor anayeheshimika dunia nzima, kushirikiana na wakina Ndugu John Mashaka Hildebrand Shayo na wengineo kutawasaidia hata wao kukua zaidi na kujulikana kimataifa, licha ya kuleta mawazo chanya na mbadala katika ujenzi wa taifa letu.
Niko tayari kuendeleza mijadala ikiwa John Mashaka atajitokeza

Wenu katika Ujenzi Wa Taifa
Prof. US-Blogger, Bsc, Msc, PhD (Oxford)
Oxford University, Department of Economics
Political Economics
London, United Kingdom


SINTOFAHAMU YA VYAMA VYA SIASA INATATULIWA KWA KUKAA NA KUZUNGUMZA PAMOJA-JAJI MUTUNGIMSAJILI wa vyama vya Siasa nchini, Jaji Mstaafu, Francis Mutungi 
Na Chalila Kibuda , Globu ya Jamii.
MSAJILI wa vyama vya Siasa nchini, Jaji Francis Mutungi amesema masuala yote ya  sintofahamu kwa vyama vya siasa yatatuliwa katika meza ya majadiliano na si vinginevyo.
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Jaji Mutungi amesema kuwa kuna taharuki au hofu ambayo inajengwa kwa wadau wa siasa ambayo inahitaji kuwepo mazungumzo kutokana na taratibu zinazohusu utawala bora.
Amesema kuwa utawala bora ni kuheshimu miundombinu iliyowekwa kwa kufuata sheria zake na bila kufanya hivyo miundombinu haitakuwa imetendewa haki kwa watu kufanya chochote bila kuangalia misingi iliyowekwa katika miundombinu hiyo.
Amesema kuwa Baraza la vyama vya siasa limeandaa mkutano wa wadau wa vyama vya siasa pamoja na watu wengine kuweza kuzungumza masuala mbalimbali ambayo yamejitokeza katika kipindi hiki na kupatiwa ufumbuzi wa sintofahamu miongoni mwa  wadau.
Jaji Mutungi amesema kuwa baraza la vyama vya siasa linatarajia kukaa  Agosti 29 na 30 kutaka wadau wote waweze kushiriki ili kutafuta suluhu kwa yale ambayo yamejitokeza sambamba na kuyatafutia suluhu katika kuendelea kulinda amani ya nchi yetu.
Amesema  siku zote watu wanatafuta mwafaka wa jambo lolote katika meza ya mazungumzo na kupata suluhu katika kulinda amani ya nchi yetu.
Aidha amesema suala la Chama cha Wananchi (CUF) anaangalia na kuona jinsi gani anaweza kushauri kutokana na kuwa mlezi wa vyama vyote ambavyo vimepata usajili katika ofisi yake.


TRL YAFANYA MABADILIKO YA RATIBA YA SAFARI ZA ABIRIA KWENDA BARA NA KUONGEZA MOJA KUANZIA SEPTEMBA 01 , 2016

 Uongozi wa Kampuni ya Reli Tanzania (TRL) umeamua kuongeza safari ya tatu ya treni ya abiria ya kawaida kwenda bara  ambayo itaondoka  Dar es Salaam kila Jumapili, safari ya kwanza itakuwa Jumapili hii ya  Septemba 04, 2016 saa 9 alasiri. 
Taarifa imeainisha kuwa treni hiyo ya huduma ya kawaida itakuwa na mabehewa  12 kutokea   Dar  es  Salaam ikiwa na mabehewa manane ya daraja la 3, mawili daraja la pili kulala na mawili daraja la kwanza. Katika  stesheni za Morogoro na Dodoma yataongezwa  mabehewa mawili mawili ya daraja la 3.
Aidha treni ya Deluxe imebadilishwa siku ya kuondoka badala ya Jumapili kwa sasa kuanzia Septemba Mosi, 2016 itakuwa inaondoka siku ya Alhamis saa 2 asubuhi kutoka kituo kikuu cha Dar es Salaam. 
Halikadhalika mabadiliko haya pia yataongeza safari za treni ya kwenda Mpanda kutoka Tabora badala ya 2 za sasa zitakuwa 3 kwa wiki ambazo ni Jumatatu, Jumatano na Jumamosi..
Wakati huohuo  Uongozi wa TRL umefanya uamuzi wa kihistoria wa kupeleka huduma za kuuzwa  tiketi za safari zake  mjini Kasulu ambapo kuanzia Septemba Mosi itafungua kituo cha Reli ambacho kitafanya kazi ya kuto huduma hiyo kwa  wasafari wanaotoka Kasulu mjini na maeneo ya jirani . Kwa uamuzi huo TRL imetoa nafasi za tiketi za  behewa moja la daraja la 3. Mpango pia uko mbioni  wa  kufungua kituo kama hicho siku zijazo mjini Kibondo hali itakaporuhusu kulingana na mahitaji halisi ya abiria. 
Taarifa imesisitiza kuwataka wasafiri na wananchi kwa jumla nchini  hususan wale wa Mpanda na Kibondo kutumia fursa ya kuongezewa safari na huduma kuletewa karibu kwa kufuata sheria , taratibu na  kanuni ili hatua iliyochukuliwa na TRL iwe na tija iliokusudiwa.
Aidha taarifa zaidi zinaarifu kuwa hatimaye TRL imefanikiwa kuongeza mabehewa mawili zaidi ya treni ya Pugu na kufikia idadi ya behewa 18 hadi jana Agosti 22, 2016. Ni matarajio ya Uongozi ifikapo Agosti 31, 2016 treni hiyo ya Jiji  itakuwa na mabehewa 20 iloahidi ili kupunguza msongamano unaosababishwa na abiria kuwa wengi katika safari mbili za awali katika awamu zote 2 ya asubuhi na ya jioni. 

Imetolewa na Afisi ya Uhusiano kwa Niaba ya :
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TRL,
Nd Focus Makoye Sahani,
Dar es Salaam,
Agosti 23, 2016.


RAIS DKT. MAGUFULI APOKEA HATI ZA UTAMBULISHO KUTOKA KWA MABALOZI WA NCHI MBALIMBALI IKULU JIJINI DAR LEO

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea Hati za Utambulisho kutoka kwa Balozi wa Italia hapa nchini Roberto Mengoni Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimshukuru Balozi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Watu wa Korea hapa nchini Kim Yong Su mara baada ya kupokea Hati zake za Utambulisho Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Balozi wa Somalia hapa nchini Mohammed Hassan Abdi mara baada ya kuwasili Ikulu kwa ajili ya kuwasilisha Hati zake za Utambulisho.
Rais Dkt. John Pombe Magufuli akipokea Hati za Utambulisho kutoka kwa Balozi wa Ireland hapa nchini Paul Sherlock Ikulu jijini Dar es Salaam.


TAIFA STARS KUCHEZA NA THE SUPER EAGES SEPTEMBA 3 BADALA YA SEPTEMBA 2, 2016 HUKO NIGERIA

Shirikisho la Mpira wa Miguu Nigeria (NFA), limesogeza mbele kwa siku moja mchezo kati ya timu ya taifa ya Nigeria ‘The Super Eagles’ na Tanzania ‘Taifa Stars’ ambako sasa utafanyika Septemba 3, 2016 badala ya Septemba 2, 2016 iliyotangazwa awali. 
Na Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Charles Boniface Mkwasa kesho anatarajiwa kutangaza kikosi ambacho atakiandaa maalumu kwa mchezo huo. Mkwasa amesema kwamba anatarajia kuita wachezaji 20 ambao atasafiri nao kwenda Nigeria kwa ajili ya mchezo huo.
Kwa taarifa zaidi, fuata link hapo chini


WAZIRI PROF.MBARAWA AKUTANA NA MKURUGENZI MTENDAJI WA BENKI YA MAENDELEO YA AFRIKA kanda ya Afrika Mashariki Dkt. Nyamajeje Weggoro

 Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (wa tatu kulia), akimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), kanda ya Afrika Mashariki Dkt. Nyamajeje Weggoro (wa tatu kushoto), alipomtembelea ofisini kwake Jijini Dar es salaam.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (wa kwanza kulia), akifafanua jambo kwa wajumbe kutoka Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), kanda ya Afrika Mashariki walipomtembelea ofisini kwake Jijini Dar es salaam.


Amref TZ, HABARI Newsletter & 2015 Annual Report


Mkuu mpya wa Wilaya ya Arusha Mhe. Gabriel Daqarro ala kiapo kuanza kazi

 Mkuu wa wilaya ya Arusha Mhe. Gabriel Daqarro akila kiapo kwenye sherehe fupi za kumwapisha zilizofanyika leo jijini Arusha na kusimamiwa na mkuu wa mkoa huo Mhe. Mrisho Gambo
 Mkuu wa mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo akisaini hati ya kiapo cha Mkuu wa wilaya mpya ya Arusha,Gabriel Daqarro(kulia)wanaoshuhudia ni Katibu Tawala mkoa,Richard Kwitega na Afisa wa Itifaki,Mukhsin Khasim.
 Viongozi mbalimbali katika Jiji la Arusha wakifatilia tukio hilo.
 Mkuu wa wilaya ya Arusha Mhe. Gabriel Daqarro akitoa shukrani zake baada ya kuapishwa.
Mkuu wa wilaya ya Arusha Gabriel Daqarro akitoa shukrani zake baada ya kuapishwa katika picha ya pamoja na viongozi waandamizi a mkoa wa Arusha baada yasherehe za kula kiapo.


MPINGA CUP 2016 YAPAMBA MOTO, WAENDESHA BODABODA WANUFAIKA KWA MAFUNZO NA VIFAA VYA MICHEZO

 Mratibu wa Mashindano ya Mpinga Cup 2016 , A.S.P Mbunja Matibu, akikagua timu za kundi B zinazoshiriki kwenye Michuano hiyo, kwa Madereva wa Bodaboda, yaliyofanyika kwenye uwanja wa Magereza Ukonga mwishoni mwa Wiki iliyopita, Lengo kuu la Mashindano hayo ni kutoa elimu ya Usalama Barabarani kwa Waendesha Pikipiki (Boda boda).
Picha zote na Traffic MakaoMakuu

 Mkaguzi wa Polisi Hamisi Membe akifundisha waendesha pikipiki (Bodaboda), kuhusu Alama za Usalama Barabarani, wakati wamashindano ya Mpinga Cup 2016 yanayoshirikisha Madereva wa Bodaboda, yaliyofanyika kwenye uwanja waMagerezaUkongamwishoni mwajuma, Lengo kuu la Mashindano hayo ni kutoa elimu ya Usalama Barabarani kwa Waendesha Pikipiki (Boda boda).(
 Mrakibu wa Polisi Methew Msuyale (kushoto) akikabidhi Fulana  kwa kiongozi wa timu mojawapo zilizoshiriki kwenye hatua ya Mtoano kutoka kundi B kwenye ya Mpinga Cup 2016, iliyochezwa kwenye uwanja wa Magereza Ukonga Mwishoni mwa wiki iliyopita. Lengo kuu la Mashindano hayo ni kutoa elimu ya Usalama Barabarani kwa Waendesha Pikipiki (Boda boda).
  Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani (T) DCP Mohammed Mpinga akikagua timu katika  mashindano ya Mpinga Cup 2016 inayohusisha waendesha Pikipiki Mkoani Ilala, Dar es Salaam, Lengo kuu la Mashindano hayo ni kutoa elimu ya Usalama Barabarani kwa Waendesha Pikipiki (Boda boda).
 Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani (T) DCP Mohammed Mpinga akiwataka na kuwaelimisha waendesha pikipiki (Boda Boda) kuzingatia, kuzifuata na kuziheshimu Sheria za Usalama Barabarani ili kuweza kupunguza wimbi la ajali za waendesha Pikipiki hapa nchini. Kupitia mashindano ya Mpinga Cup 2016 inayohusisha waendesha Pikipiki Mkoani Ilala, Dar es Salaam, Lengo kuu la Mashindano hayo ni kutoa elimu ya Usalama Barabarani kwa Waendesha Pikipiki (Boda boda).DC STAKI ATENGA SIKU YA JUMATATU KUSHIRIKI SHUGHULI ZA MAENDELEOMkuu wa Wilaya ya Same Mkoani Kilimanjaro Mhe Rosemary Staki Senyamule akishiriki shughuli za maendeleo kwa kufyeka baadhi ya vichaka
 Mkuu wa Wilaya ya Same Mkoani Kilimanjaro Mhe Rosemary Staki Senyamule akizungumza na viongozi wa Kijiji na Kata ya Gonja Maore na baadhi ya wajumbe wa kamati ya siasa Wilaya


Dc Senyamule akishiriki zoezi la kupanga matofali yaliyofyatuliwa na wananchi wenyewe kwa ajili ya miradi ya maendeleo Wilayani humo.


Na Mathias Canal, 
Kilimanjaro

Mkuu wa Wilaya ya Same Mkoani Kilimanjaro Mhe Rosemary Staki Senyamule ametenga Siku moja katika Juma ili kushiriki shughuli za maendeleo kwa kushirikiana na wananchi.

Huu ni utaratibu ambao Mkuu huyo wa Wilaya ameuanzisha kwa muktadha wa kuchochea ari katika utendaji Kazi na uwajibikani kwa kila mwananchi ili kuimarisha na kusukuma kwa vitendo juhudi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Joseph Pombe Magufuli kwa vitendo na utekelezaji wa utendaji kazi ili kuakisi dhana nzima ya serikali hii ya awamu ya tano ya Hapa Kazi Tu.
"Nimeamua kutenga siku hii ya jumatatu kwani naamini italeta hamasa kwa wananchi kupenda kazi za maendeleo, itawatia moyo na kuona kuwa serikali ipo karibu nao ". Alisema Staki
Akizungumzia kuhusu kuanza kwa vitendo utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi Dc Staki amesema kuwa asilimia kubwa ya watanzania wanaoishi kwa mazoea ya kuyumbishwa na siasa zisizo na manufaa kwao lakini huu si wakati tena wa kurudi nyuma badala yake watanzania wote wanapaswa kushirikiana katika kufanya Kazi na kulifanya Taifa Letu kufika mbali zaidi kimaendeleo.
Hii imekuwa ziara ya mwanzo ya Mkuu huyo wa Wilaya ya Same Mhe Rosemary Staki kwa kushiriki kufanya kazi za Jamii akiwa na dhamira ya kuwatia Moyo wananchi ili kupunguza lawama zisizo na lazima kwa serikali na badala yake kujituma katika kufanya kazi.
Ziara hiyo katika kushiriki Kazi za jamii imefanyika katika kijiji cha Mheza na Maore vilivyopo kata ya Gonja Maore huku wananchi wakijitokeza kwa wingi kuishauri na kushirikiana na serikali.
Kwa upande wawananchi wa maeneo hayo walionyesha kufurahishwa na utaratibu huo ambao haujawahi kufanyika na kiongozi yeyote katika Wilaya ya Same tangu kuumbwa kwa msingi ya ulimwengu.
Wananchi hao wamemuakikishia Mkuu hiyo wa Wilaya hiyo kuwa watashirikiana nae katika shughuli za maendeleo kwani kwa kiasi kikubwa udini na uzembe wa watendaji wengi umesababisha kuendelea kuzorota kwa maendeleo ya Wilaya, Mkoa na Taifa kwa ujumla.
Pamoja na hayo pia Dc Staki Ametoa onyo kwa wananchi hususani Vijana ambao ni wavivu katika kushiriki shughuli za Jamii kuchukuliwa hatua Kali za kinidhamu kW kila mwananchi atakayeshindwa kutekeleza wajibu wake.


Madawati 30,000 mbioni kukamilika ili yasambazwe katika Mikoa na Halmashauri zote Nchini

Na Frank Mvungi- Maelezo.
Madawati 30,000 mbioni kukamilika ili yaweze kusambazwa katika Mikoa na Halmashauri zote hapa Nchini ikiwa ni utekelezaji wa awamu ya pili ya mpango wa Serikali wa kutengeneza madawati elfu 60 kwa ajili ya shule za Msingi na Sekondari hapa nchini.
Kauli hiyo imetolewa Leo jijini Dar es salaam na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe. Dkt. Hussein Mwinyi wakati wa mkutano na waandishi wa habari.
Akifafanua Dkt. Mwinyi amesema kuwa katika awamu ya pili madawati 20,000  yameshakamilika na yanaweza kuchukuliwa kuanzia sasa kwenda kwenye majimbo yaliyopangiwa kupata madawati hayo.
“Madawati elfu kumi yaliyobaki yatakamilika wakati wowote kabla ya muda wa mwisho uliowekwa”Alisisistiza Dkt. Mwinyi.
Katika kutekeleza mpango huo, awamu yakwanza jumla ya madawati 32,387 yalitengenezwa na yaliyochukuliwa na Wabunge kwa kushirikiana na Halmashauri zao ni 22,721 tu,hivyo madawati 9,666 sawa na asilimia 30% bado hayajachukuliwa na Majimbo husika.
Akitaja Baadhi ya Mikoa iliyonufaika na Madawati hayo Dkt. Mwinyi amesema kuwa ni Tanga madawati 6444, Njombe 3222,Iringa 3709, Mbeya 3759, Songwe 3222, Rukwa 1611, Ruvuma 4833,Visiwa vya Unguja 3200,Pemba 1800.
Akizungumzia Majimbo ambayo hayajachukua madawati yake katika awamu ya kwanza Dkt.Mwinyi amesema ni vyema Viongozi katika Majimbo hayo wakiwemo Waheshimiwa Wabunge wanatakiwa wakachukue madawati hayo kabla ya mwisho wa mwezi huu.
Majimbo ambayo hayajachukua madawati yake katika awamu ya kwanza yametajwa kuwa ni Kilindi,Pangani,Makambako,Ludewa,Wangingombe naMakete..
Majimbo mengine ni Kyela,Rungwe,Busokelo,Songwe,Kwela,Tunduru,Iringa Mjini,Mbeya Mjini,Mbeya Vijijini na Ileje Nkasi Kaskazini na Nkasi Kusini.
Tarehe 11 April,2016 Serikali ilitoa zabuni kwa JKT kutengeneza madawati 60,000 kwa gharama ya Bilioni 3 ambapo bei ya kila dawati ni sh 50,000/,aidha tarehe 13 Julai 2016 JKT ilikabidhi madawati 32,387.

 Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe. Dkt. Hussein Mwinyi akizungumzia utekelezaji wa awamu ya pili ya mpango wa kutengeneza madawati  30,000  unaotekelezwa na JKT ili kukamilisha madawati 60,000 yaliyopangwa na Serikali hali itakayosaidia kuondoa tatizo la madawati katika shule za Msingi na Sekondari hapa Nchini.
Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Brigedia Jenerali Michael Isamuhyo akifafanua kwa waandishi wa Habari  leo jijini Dar es salaam kuhusu Ubora wa madawati yaliyotengenezwa na JKT na kusisitiza kuwa yana ubora unaotakiwa ambapo madawati hayo ni sehemu mpango wa serikali kukabiliana na changamoto ya upungufu  wa Madawati hapa Nchini.


SIMU TV: HABARI KUTOKA TELEVISHENI


SIMU.TV: Msajili wa vyama vya siasa nchini Jaji Francis Mutungi, amesema kamati ya baraza la vyama vya siasa nchini litakutana mwishoni mwa mwezi huu kujadili hali ya kisiasa nchini; https://youtu.be/71XK4DcWvBc

SIMU.TV: Wilaya ya Karagwe mkoani Kagera, imepiga marufuku shughuli zote za uvuvi katika mto kagera mpaka hali ya kiusalama itakapothibitika kutulia;https://youtu.be/wEPexa49Zic

SIMU.TV: Watu wanne wamejeruhiwa baada ya kutokea kwa mapigano kati ya wakulima na wafugaji wilayani Mbalali mkoani Mbeya; https://youtu.be/OFWxKr6lxnI

SIMU.TV: Waziri wa maji na umwagiliaji mhandisi Gerson Lwenge akiwa mkoani Kigoma, amewataka wahandisi wa ngazi za wilaya na mkoa kusimamia kwa umakini miradi ya maji;https://youtu.be/vSTKGVoqa_0

SIMU.TV: Wizara ya kilimo mifugo na uvuvi imefuta mfumo wa utoaji vocha kwa wakulima kupitia mawakala binafsi na badala yake kazi hiyo zimekabidhiwa kampuni za serikali kupitia kamati za ulinzi na usalama; https://youtu.be/KMLWctq_b-g

SIMU.TV: Waziri wa Elimu Prof Joyce Ndalichako, ameitaka tume ya taifa ya sayansi na teknolojia nchini COSTECH kuwa na matumizi mazuri ya pesa za utafiti;https://youtu.be/8-7ssyJaUTY  

SIMU.TV: Kikosi cha usalama barabarani kanda maalumu ya Dar Es salaam, kimekusanya fedha zaidi shilingi milioni 161 kutokana na makosa ya barabarani kwa siku za Jumapili na jana Jumatatu; https://youtu.be/1zU5Mfs0tFU

SIMU.TV: Benki ya Afrika imefungua tawi lake wilayani Babati mkoani Manyara ili kuweza kuwafikia wateja wake walioko wilayani humo; https://youtu.be/mwx3gTmFy8U  

SIMU.TV: Timu ya Yanga imekamilisha ratiba ya michuano barani Afrika kwa kipigo cha magoli 3-1 katika mchezo wake dhidi ya TP Mazembe uliopigwa leo jijini Lubumbashi;https://youtu.be/d38dUiow2c8  

SIMU.TV: Timu ya Taifa ya vijana Serengeti boys inatarajia kuweka kambi yake nje ya nchi kuweza kujiandaa kikamilifu na mchezo wake kati ya Congo au Namibia;https://youtu.be/utySjyQEHEQ

SIMU.TV: Timu ya African Lyon imesema bado inaendelea vizuri na mazoezi kwa ajili ya kujiweka sawa na michezo yake inayofuata baada ya kutoka sare katika mchezo wake wa kwanza dhidi ya Azam Fc; https://youtu.be/lSpY8aHQEyE

SIMU.TV: Baadhi ya wajasiliamali wadogo kutoka mikoa ya kanda ya ziwa wameanza kutengeneza mipira ya miguu baada ya kupewa mafunzo na taasisi ya teknolojia kampasi ya Mwanza; https://youtu.be/3BlEBwIa3Ng


WAZIRI MKUU MAJALIWA AKAGUA UJENZI WA DARAJA KWENYE MTO KAVUU, WILAYA YA MLELE, MKOA WA KATAVI

Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa na Mkewe Mama Mary Majaliwa  wakiwapungia wananchi wa kijiji cha Majimoto wilayani Mlele kabla ya kuhutubia mkutano wa hadhara kijijini hapo leo  Agosti 23, 2016.
Ujenzi wa daraja la mto Kavuu wilayani Mlele ambalo Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa alikagua ujenzi wake  leo Agosti 23, 2016.
Waziri Mkuu Mhe Kassim Majaliwa akikagua ujenzi wa daraja la mto Kavuu wilayani Mlele Agosti 23, 2016.
PICHA NA OFISI YA WAZIRI MKUU


TEASER JOTO LA ASUBUHI AUGUST 24 JUMATANO


COME TO TANZANIA AND WITNESS ANNULAR SOLAR ECLIPSE on September 1, 2016

Tanzania Tourist Board wishes to welcome everyone from all over the world to come to Tanzania and witness the solar eclipse which according to astronomy experts Tanzania in particular Rujewa district in Mbeya region located in Southern Tanzania will be the best site for viewing this fascinating event where the sun’s disk will change to a ring.
This major astronomical event will occur on September 1 this year from 10:17am to 1:56pm, centered over Tanzania and is expected to attract eclipse chasers from around the world and across the country.
People in Tanzania will witness first-hand the sun go evening-dim at midday as more than 90% of the sun will be covered by the moon in a partial solar eclipse leaving the sun as a thin crescent.
The annual eclipse will be seen as a thin bright ring on that day for hundreds of thousands of people living within a 100 kilometre band crossing Southern Tanzania from Congo into Katavi, Mbeya, Ruvuma, to Masasi and out to Mozambique.
Experts say that the next eclipse in Tanzania is expected to occur after 15 years. So this is a great opportunity that one shouldn’t miss.