Na Frank Mvungi- Maelezo.
Madawati 30,000 mbioni kukamilika ili yaweze kusambazwa katika Mikoa na Halmashauri zote hapa Nchini ikiwa ni utekelezaji wa awamu ya pili ya mpango wa Serikali wa kutengeneza madawati elfu 60 kwa ajili ya shule za Msingi na Sekondari hapa nchini.
Kauli hiyo imetolewa Leo jijini Dar es salaam na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe. Dkt. Hussein Mwinyi wakati wa mkutano na waandishi wa habari.
Akifafanua Dkt. Mwinyi amesema kuwa katika awamu ya pili madawati 20,000  yameshakamilika na yanaweza kuchukuliwa kuanzia sasa kwenda kwenye majimbo yaliyopangiwa kupata madawati hayo.
“Madawati elfu kumi yaliyobaki yatakamilika wakati wowote kabla ya muda wa mwisho uliowekwa”Alisisistiza Dkt. Mwinyi.
Katika kutekeleza mpango huo, awamu yakwanza jumla ya madawati 32,387 yalitengenezwa na yaliyochukuliwa na Wabunge kwa kushirikiana na Halmashauri zao ni 22,721 tu,hivyo madawati 9,666 sawa na asilimia 30% bado hayajachukuliwa na Majimbo husika.
Akitaja Baadhi ya Mikoa iliyonufaika na Madawati hayo Dkt. Mwinyi amesema kuwa ni Tanga madawati 6444, Njombe 3222,Iringa 3709, Mbeya 3759, Songwe 3222, Rukwa 1611, Ruvuma 4833,Visiwa vya Unguja 3200,Pemba 1800.
Akizungumzia Majimbo ambayo hayajachukua madawati yake katika awamu ya kwanza Dkt.Mwinyi amesema ni vyema Viongozi katika Majimbo hayo wakiwemo Waheshimiwa Wabunge wanatakiwa wakachukue madawati hayo kabla ya mwisho wa mwezi huu.
Majimbo ambayo hayajachukua madawati yake katika awamu ya kwanza yametajwa kuwa ni Kilindi,Pangani,Makambako,Ludewa,Wangingombe naMakete..
Majimbo mengine ni Kyela,Rungwe,Busokelo,Songwe,Kwela,Tunduru,Iringa Mjini,Mbeya Mjini,Mbeya Vijijini na Ileje Nkasi Kaskazini na Nkasi Kusini.
Tarehe 11 April,2016 Serikali ilitoa zabuni kwa JKT kutengeneza madawati 60,000 kwa gharama ya Bilioni 3 ambapo bei ya kila dawati ni sh 50,000/,aidha tarehe 13 Julai 2016 JKT ilikabidhi madawati 32,387.

 Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe. Dkt. Hussein Mwinyi akizungumzia utekelezaji wa awamu ya pili ya mpango wa kutengeneza madawati  30,000  unaotekelezwa na JKT ili kukamilisha madawati 60,000 yaliyopangwa na Serikali hali itakayosaidia kuondoa tatizo la madawati katika shule za Msingi na Sekondari hapa Nchini.
Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Brigedia Jenerali Michael Isamuhyo akifafanua kwa waandishi wa Habari  leo jijini Dar es salaam kuhusu Ubora wa madawati yaliyotengenezwa na JKT na kusisitiza kuwa yana ubora unaotakiwa ambapo madawati hayo ni sehemu mpango wa serikali kukabiliana na changamoto ya upungufu  wa Madawati hapa Nchini.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...