MSAJILI wa vyama vya Siasa nchini, Jaji Mstaafu, Francis Mutungi 
Na Chalila Kibuda , Globu ya Jamii.
MSAJILI wa vyama vya Siasa nchini, Jaji Francis Mutungi amesema masuala yote ya  sintofahamu kwa vyama vya siasa yatatuliwa katika meza ya majadiliano na si vinginevyo.
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Jaji Mutungi amesema kuwa kuna taharuki au hofu ambayo inajengwa kwa wadau wa siasa ambayo inahitaji kuwepo mazungumzo kutokana na taratibu zinazohusu utawala bora.
Amesema kuwa utawala bora ni kuheshimu miundombinu iliyowekwa kwa kufuata sheria zake na bila kufanya hivyo miundombinu haitakuwa imetendewa haki kwa watu kufanya chochote bila kuangalia misingi iliyowekwa katika miundombinu hiyo.
Amesema kuwa Baraza la vyama vya siasa limeandaa mkutano wa wadau wa vyama vya siasa pamoja na watu wengine kuweza kuzungumza masuala mbalimbali ambayo yamejitokeza katika kipindi hiki na kupatiwa ufumbuzi wa sintofahamu miongoni mwa  wadau.
Jaji Mutungi amesema kuwa baraza la vyama vya siasa linatarajia kukaa  Agosti 29 na 30 kutaka wadau wote waweze kushiriki ili kutafuta suluhu kwa yale ambayo yamejitokeza sambamba na kuyatafutia suluhu katika kuendelea kulinda amani ya nchi yetu.
Amesema  siku zote watu wanatafuta mwafaka wa jambo lolote katika meza ya mazungumzo na kupata suluhu katika kulinda amani ya nchi yetu.
Aidha amesema suala la Chama cha Wananchi (CUF) anaangalia na kuona jinsi gani anaweza kushauri kutokana na kuwa mlezi wa vyama vyote ambavyo vimepata usajili katika ofisi yake.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. Si kweli kwamba uchaguzi ukiisha marekani eti watu wanaacha mikutano ya siasa. kama hamjui ulizeni watz waishio marekani "tea party" ni nini. Ni republican walizungunguka nchi nzima baada ya obama kushinda. Ili chama kisife wakati wa kusubiri uchaguzi mwengine.

    Kwa tz ambapo vyama vya upinzani bado vichanga lazima paruhusiwe wafanye siasa ili wakuwe na ili ushindani wa kweli uwepo.

    ReplyDelete
  2. mimi nipo marekani ndio lakini marekani siasa zikiish zimeisha wanahamisha mambo yote congress.na kama unasema walizunguka nchi nzima kwa obama basi ilitokea kwa ajiri ni mweusi mbona huko nyuma hawakufanya je umefanya utafiti wa kutoshaÉkinachotokea Tanzania ni chadema wamekuwa very schocked na utendaji wa magufuri walitaka mtu lazy.kumbuka walilelewa vibaya enzi za kikwete.wanatakiwa wabadilishe mind seti huu ni utawala mwingine.mimi nafikiri wangetumia jina jingine kuandamaana hakungekuwa na shida ila neno dikteta kila mtu mwenye akili zake anashangaa hii kweli magufuri ni dikteta.maana ya dikteta wanaijua kweli...mmmh naombea tanzania yetu iwe na amani na wanasiasa wasituletee machafuko.jana umeona ndani ya cuf.sasa je chama na chama lazima mkanganiko uwepo ila meza ya mazungumzo iwepo raisi ni wa watu wote.kwahiyo ni vema kukaa chini na chadema kuongea sio kila mtu mmbabe

    ReplyDelete
  3. We jamaa, data ya kuwa kina Sara Palin na wengine kurunguka nchi nzima wakihubiri Obama awe One term only inatosha kuonyesha kwamba bado mahubiri ya siasa yanaendelea mtaani. Mbona Obama hakuwakataza na kuwaambia kuwa tayari kuna congress na senate acheni siasa? Inaonyesha uhuru wa siasa lazima uheshimiwe. Kama katiba haisemi kusubiri uchaguzi basi siasa saa yeyote ruksa.

    ReplyDelete
  4. Unajuwa kusema watu wasifanye siasa wafanye kazi si kosa. Lakini kuna jumamosi na jumapili watu wanaweza fanya siasa na wasiingilie muda wa kazi za serikali. Kama katiba inatoa haki basi haki wapewe ila wabunge wa ccm wapitishe sheria ya kuzuia mikutano basi kila mtu ataitii sheria hiyo.

    ReplyDelete
  5. Jaji kasema sheria zipo ili zifuatwe. Na wote. Kama kuna sheria inatoa uhuru wa mikutano ya hadhara basi raisi na wenzie watii sheria hiyo. Kama sheria hiyo haipo basi chadema watii amri halali ya raisi.

    ReplyDelete
  6. Jaji, utawala bora ni serikali kutawala vizuri zaidi kisheria. Suala la watu kutii sheria sio la utawala bora ni la mahakama na polisi kusimamia. mahakama itoe kauli nani ana haki kati ya raisi au chadema. Manake lazima kuna mmoja yuko sahihi na mwengine anakosea hapa. Haiwezekani wote wawe sahihi.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...