Kutoka kushoto Offer Gat, Mwenyekiti wa kundi la Makampuni ya DPO, Eran Feinstein, Mkurugenzi Mkuu wa DPO,  Matteo Stefanel, Mwanzilishi na Mshiriki Msimamizi wa Apis na Kiprono Terigin, Mwekezaji Mshirika wa Apis, wakati wa uzinduzi wa uwekezaji wa Apis katika kampuni iliyozinduliwa upya ya Direct Pay Online. 

Direct Pay Online (DPO) yapata uwekezaji mkubwa kutoka katika Mfuko Kukuza Uchumi wa APIS 

Apis kupitia mfuko wa kukuza uchumi wa Apis Growth Fund 1 yajipatia hisa katika Kampuni ya DPO, ambayo awali ilijulikana kama 3G Direct Pay Limited
DPO Group ni moja ya makampuni yanayoongoza katika malipo ya mitandaoni  katika Afrika Mashariki, na operesheni katika nchi za Kenya, Uganda, Rwanda, Tanzania (ikiwa ni pamoja na Zanzibar), na Zambia

Uwekezaji huu utasaidia dira ya DPO Group ya kujenga mfumo wa kupitisha malipo Afrika nzima 

Nairobi, Kenya 22 Septemba 2016 – Direct Pay Online ( DPO Group) inayoongoza katika kupitisha malipo ya mitandaoni katika Afrika Mashariki, imepokea uwekezaji mkubwa kutoka katika mfuko wa kukuza uchumi wa Apis, mfuko binafsi wa usawa unaosimamiwa na washirika wa Apis LLP ambayo ni msimamizi wa mifuko binafsi unaolenga kutoa huduma za kifedha katika masoko yanayokua ya Afrika na Asia.

DPO Group, ambayo awali ilijulikana kama 3G Direct Pay Limited, ilizindua operesheni mwaka 2006 kwa kuanzia nchini Kenya, na baadaye kupanua biashara hadi nchini Zambia, Uganda, Rwanda na Tanzania, ikiwa ni pamoja na Zanzibar. DPO Group inahudumia zaidi ya wateja 5,000 katika kanda hii, ikiwa ni pamoja na mashirika ya ndege zaidi ya 40, mamia ya hoteli, na maelfu ya mawakala wa usafiri na kampuni za watalii. Kuwepo wigo mkubwa wa wateja kumefanya kampuni ya DPO kuwa moja ya makampuni makubwa ambayo yanafanya biashara za kupitisha malipo mitandaoni katika Afrika Mashariki.

 DPO inafanya michakato ya malipo kwa kadi zote kuu  za malipo, malipo ya pesa kwa simu na pochi za mitandaoni (e-wallet), na ni mtoa huduma hizi pekee katika Afrika Mashariki mwenye vyeti vya hatua ya kwanza ya PCI DSS Level 1, na wenye vyeti usalama wa juu kabisa katika ya sekta kadi za malipo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...