Mkurugenzi Mkuu,Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu Dkt Mwele Malecela akzingumza na waandishi wa habari mapema leo asubuhi kuhusiana na maandalizi ya Kongamano lao la 30 linalotarajia kufanyika kuanzia Oktoba 4 mpaka 6,2016 katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam.

Amesema kuwa katika mkutano huo,Mgeni Rasmi katika ufunguzi wa Kongamano hilo atakuwa Mheshimiwa Mama Samia Suluhu Hassan, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,na kuwa Mada kuu ya Kongamano hilo itakuwa ni “Uwekezaji katika tafiti zenye ubunifu ili kufikia malengo endelevu ya dunia.” ambapo Jumla ya mada 220 zitawasilishwa na kujadiliwa katika Kongamano hili la Siku 3.Pichani kulia ni Mkurugenzi wa Kuratibu na kukuza usafiri/Mtafiti Mkuu kutoka taasisi hiyo,Dkt Julius Massaga . 
Baadhi ya Waandishi wa habari wakimsikiliza Mkurugenzi Mkuu,Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR), Dkt Mwele Malecela alipokuwa akizingumza nao mapema leo asubuhi kuhusiana na maandalizi ya Kongamano lao la 30 linalotarajia kufanyika kuanzia Oktoba 4 mpaka 6,2016 katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam.PICHA NA MICHUZI JR. 

Dkt Mwele alieleza pia Mada zitakazojadiliwa siku ya mkutano huo kuwa zitajikita kwenye maeneo yafutayo:1. Mkakati wa kuboresha afya ya uzazi, ya mama, watoto wachanga na vijana. 2. Magonjwa sugu yasiyoambukiza na changamoto zake,3. Kuendeleza mafanikio yaliyopatikana katika mapambano dhidi ya UKIMWI, kifua kikuu na malaria,4. Usalama wa Maji, Usafi wa mazingira na usafi binafsi,5. Mkakati wa afya moja katika kudhibiti magonjwa ya milipuko,pamoja na 6. Magonjwa ya kitropiki yasiyopewa kipaumbele.

Amesema kuwa Mada hizo zitalenga katika kujadili haja ya kuwekeza katika tafiti za mifumo ya utoaji huduma, magonjwa ya kuambukiza na yasiyoambukiza na tabia na shughuli za kibinadamu zinazochangia kuwepo kwa maradhi. Mikakati ya kufikia Malengo Endelevu ya Dunia itajadiliwa na mapendekezo kuwasilishwa kwa Serikali na wadau wengine.

Amesema kuwa NIMR inaamini kwamba watafiti wana michango mkubwa katika kuleta maendeleo kupitia matokeo ya tafiti mbalimbali wanazofanya juu ya magonjwa ya binadamu. "Ni kwa msingi huo basi, Taasisi inasisitiza kwamba kila mtafiti ana jukumu la kuwasaidia Watanzania kufikia malengo endelevu ya dunia kwa kuepuka magonjwa",alisema Dkt Mwele. 

Dkt Mwele amesema kuwa pamoja na uwasilishwaji na majadiliano katika mada mbalimbali, Taasisi imeandaa:1. Maonesho ya bidhaa zitokanazo na tafiti, taarifa za kitafiti, machapisho, vifaa vya utafiti, vyenzo za kutoa huduma za afya 

2. Mikutano maalum miwili itakayojadili,a. Wanawake katika Sayansi 
b. Mikakati ya kuhamasisha ufadhili wa Tafifi kwa Wadau wa ndani ya nchi 
3. Tuzo kwa wanasayansi katika zikiwemo: (i) Mtafiti Bora wa Afya Afrika; Mtafiti Bora wa Afya Tanzania; Mtafiti Mbunifu wa Mwaka na Mtafiti Bora katika kuchapisha Maandiko ya Kitafiti. Taasisi pia itamzawadia Kiongozi Mashuhuri wa Tanzania aliyetoa mchango mkubwa katika kuinua na kuimarisha tafiti za afya nchini.

Dkt Mwele amezitaja nchi zitakazoshiriki kuwa 300,ambao  wamejisajili kuhudhuria kongamano hilo,Washiriki wanatoka katika nchi zifuatazo: Afrika Kusini, Kenya, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Uganda, Australia, Denmark, Ubeljiji, Uholanzi, Uingereza, Ujerumani, Uswis, Kanada, Sweden, Norway, Marekani, Bangladesh, Thailand na Tanzania 

Taasisi za Tanzania ni pamoja na: Taasisi ya Afya Ifakara, Vyuo Vikuu vya Tiba na Sayansi za Afya vya Muhimbili na Bugando, Chuo Kikuu cha KCMC, Taasisi ya Utafiti wa Tiba ya Kilimanjaro, Chuo Kikuu Dodoma, Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Chuo Kikuu Mzumbe, Chuo Kikuu cha Nelson Mandela cha Sayansi na Teknolojia, Hospitali ya Rufaa KCMC, AMREF Health Africa, Hospitali ya Rufaa Amana na Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Shinyanga.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...