Akijivinjari ndani ya jiji la Dar es salaam kwenye foleni mida ya mchana ndani ya gari lake jeupe aina ya Mercedes S550, Jacqueline Ntuyabaliwe, mrembo mwembamba mwenye miaka 38, akiwa ameduwaa akiiangalia picha ya samani za kulia chakula kwenye simu yake. Kwa kutumia kidole chake chembamba, kwa madaha, anaiwasha simu yake ili kunionesha picha ambazo anaziangalia.

 “Hii ni moja ya seti ya samani zetu,” anasema, huku akionesha kwa kidole picha ya seti ya samani 5. Ni moja ya bidhaa zinazotegenezwa na Molocaho by Amorette, kiwanda cha kutengeneza samani ambacho amekianzisha hivi karibuni. “Hii samani imetengenezwa kwa mabaki ya mbao ya boti ya mizigo iliyochakaa kutoka Bahari ya Hindi katika mwambao wa pwani ya Tanzania,” akisema mjasiriamali  mwenye kujituma.

Samani za kulia chakula, ananiambia, ameombwa na familia moja kutoka Ulaya ambayo ilitembelea duka lake la samani hivi karibuni Dar es salaam wakati wa likizo majuma kadhaa yaliyopita na anakaribia kuzisafirisha kwa wateja wake wapya wa Ulaya. Lakini anakwenda kwanza mara moja kwenye kiwanda chake kuzikagua mwenyewe hizo samani kwa mara ya mwisho kabla hazijasafirishwa ili kuhakikisha zinatengenezwa vizuri.

Jacqueline Ntuyabaliwe, mwenye kiu ya mafanikio ni mwanamke makini sana. Licha ya kuwa na shughuli nyingi pia (ni balozi wa kiafrika wa shirika la kulinda wanyama pori duniani WildAid na huudhuria baadhi ya mikutano ya bodi; mama mwenye watoto wawili mapacha wa kiume; mke wa mmoja ya wafanyabiashara wenye mafanikio makubwa barani Afrika na anasimamia mfuko wa hisani kwa ajili ya elimu), Ntuyabaliwe huhakikisha anakagua mwenyewe kila samani inayotengenezwa na kampuni yake kabla haijauzwa au kusafirishwa kwenda nje.

“Napenda vitu vyenye ubora wa hali ya juu!” anasema kwa hisia aliyekuwa malkia wa urembo Tanzania na mwanamuziki, akivuta pumzi kuonesha msisitizo. Kila kitu tunachotengeneza Molocaho lazima kiwe na ubora wa hali ya juu,” anasema. “Tunashindana na makampuni makubwa sana duniani kwa hiyo kama hatutazingatia ubora, itabidi tufunge virago vyetu turudi nyumbani.”


SOMA ZAIDI HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...